Jeshi Linapaswa Kusimamia Ulinzi na Kulinda Usalama, suala la Maandamano Kauli ya Chalamila Inautata

Makamura

JF-Expert Member
May 19, 2022
356
550
Jeshi La Ulinzi na Usalama ni kwaajili ya wananchi. Kauli ya Jeshi kufanya usafi baada ya tangazo la maandamano ni mara ya pili sasa, hii ni kwaajili kuwapa hofu wananchi katika kuandamana.

Tunajua Maandamano yanamadhara yake makubwa lakini Jeshi la Ulinzi na Usalama tunaomba msimame kulinda wananchi ili madhara hayo yasijitokeze.

Maandamano ni haki ya kikatiba lakini Tunashindwa kuona kwa upana madhara yanayoweza kujitokeza ni makubwa lakini kama ulinzi na usalama ukizingatiwa na Jeshi letu Jema, basi naamini mambo hayaenda tofauti na kuleta madhara.
 
Jeshi la Tanzania kuna wakati linashindwa kujipambanua kuwa ni jeshi lisilojihusisha na siasa kama linavyojinasibu.

Kitendo cha kukubali kufanya usafi siku ambayo ilisikika chama fulani kitafanya jambo ambalo ni halali kikatiba ila linaonekana kinyume na chama kilicho madarakani ni kukubali kutumika na chama hicho kama silaha ya chama
 
Back
Top Bottom