Naam, nimerudi mjini.
Nimejaribu kuuliza uliza watu wangu wa karibu hapa wananiambia kuwa jamaa wanafanya mazoezi ya kawaida. Mabomu yaliyopigwa NMB inasemekana wala sio vurugu, ila ni wenzao (waliokuwa wamevalia kiraia) wanafanya kama wanaandamana huku wamebeba mabango wakiimba (tunatakaa, haki zetuuu) huku wakiwarushia mawe, then hawa wenzao waliovalia sare za jeshi wenye silaha wakafanya kama wanatuliza ghasia sasa kwa kupiga risasi chini, kama kuwaonya wasisogee (lakini kiuhalisia hawa sio waandamanaji bali ni wanajeshi wenzao waliovalia kiraia) na ilikuwa na kama kuonesha namna ambavyo jeshi/polisi wanavyotakiwa kupambana na raia wasio na silaha. Nasema ni kama mazoezi maana kuna hadi wenzao wanachukua video za tukio na mita chache kutoka hapo NMB kuna Bar maarufu inaitwa Yapenda Mtini walipofika eneo hili hawa 'waandamanaji' wawili kati yao wakajiangusha as if wamezirai ikaja ambulance yao kuwabeba. Sasa kuna waliowadodosa kati ya wanajeshi wanaowajua wakawaambia ni mazoezi tu maana muda mrefu wamekuwa mbali sana na raia hapa.
Lakini sasa ambacho sijaelewa ni kwamba kwenye mageti ya kuingilia taasisi kubwa kubwa kama za kiserikali ama za kijamii kuna wanajeshi wanawazuia watu kuingia mfano geti la kuingia Chuo cha Uuguzi, Homso, Kanisa la Lutheran n.k sijajua pengine ambako sijapapita.
BTW; nafikiri kama kuna maelezo tafauti na haya tutajulishwa tu na wenye taarifa tofauti ama kupitia vyombo vya habari.
Adios Amigo.