Naibu Waziri Sagini: Wananchi wanaojichukulia Sheria mkononi kwa kigezo cha hasira kali kukiona

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
0fb1bf28-ffef-4361-9f6f-0ab91cfb2188.jpeg

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, akisalimiana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita ACP Safia Jongo, wakati alipotembelea na kukagua Kituo kidogo cha Polisi Bwanga Wilayani Chato katika Mkoa wa Geita Septemba 20, 2023.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, ameliagiza Jeshi la Polisi kutumia Sheria na taratibu zilizopo kudhibiti mtu yeyoye mwenye viashiria au lengo la kuvuruga amani hapa nchini.

Waziri Sagini ametoa maagizo hayo alipotembelea na kukagua Kituo kidogo cha Polisi Bwanga Wilayani Chato katika Mkoa wa Geita ambapo alipokelewa na Mwenyeji wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, ACP Safia Jongo.
c5d17d98-14fe-4ad8-a5ba-5948f387a6f4.jpeg

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (Mb), akipokea taarifa ya kituo na hali ya Askari toka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita ACP Safia Jongo, wakati alipotembelea na kukagua Kituo kidogo cha Polisi Bwanga Wilayani Chato katika Mkoa wa Geita, Septemba 20, 2023.

ba062cf5-afa2-48a6-92bf-7223c469db85.jpeg

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea na kukagua Kituo kidogo cha Polisi Bwanga Wilayani Chato katika Mkoa wa Geita, Septemba 20, 2023.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na sisi wasaidizi wake hatutomvumilia mtu yeyote mwenye lengo la kuvuruga amani na usalama wa nchi yetu tutamshughulikia vilivyo bila kujali ni nani,” amesema Sagini.

Naibu Waziri Sagini amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoani Geita kwa kufanikiwa kudhibiti vurugu zilizoanzishwa na vijana dhidi ya Jeshi hilo kufuatia kuingilia kati kuokoa maisha ya raia aliyekuwa anashambuliwa na Wananchi kwa kutuhumiwa kuiba vifaa vya mziki msibani katika eneo la Bwanga Mkoani humo.

Pia ametoa rai kwa Wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwa kudhuru maisha ya wenzao kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai na kuwataka kuimarisha shughuli za polisi jamii kwa lengo la kuimarisha usalama, kudhibiti uhalifu na kuepuka kujichukulia sheria mkononi.
e22a63cd-c9d1-4ce6-95cb-5f23fa675430.jpeg

Sehemu ya Askari wa Kituo kidogo cha Polisi Bwanga Wilayani Chato katika Mkoa wa Geita, wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini, wakati alipotembelea na kukagua Kituo hicho Septemba 20, 2023.

Aidha, amemtaka Kamanda wa Polisi na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama Mkoani humo kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa maisha ya watu na mali zao.

Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita ACP Safia Jongo, amemshukuru Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kufika kituoni hapo huku akimuhakikishia kuwa hali ya usalama mkoani humo ni shwari na wale wote wenye kuleta viashiria vya uvunjifu wa amani watashughulikiwa.
512ccd1a-0470-42a1-9bd8-634771d71eeb.jpeg

Askari wa Kituo kidogo cha Polisi Bwanga Wilayani Chato katika Mkoa wa Geita, wakionesha ukakamavu mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini, wakati alipotembelea na kukagua Kituo hicho Septemba 20, 2023.
 
View attachment 2756067
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, akisalimiana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita ACP Safia Jongo, wakati alipotembelea na kukagua Kituo kidogo cha Polisi Bwanga Wilayani Chato katika Mkoa wa Geita Septemba 20, 2023.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, ameliagiza Jeshi la Polisi kutumia Sheria na taratibu zilizopo kudhibiti mtu yeyoye mwenye viashiria au lengo la kuvuruga amani hapa nchini.

Waziri Sagini ametoa maagizo hayo alipotembelea na kukagua Kituo kidogo cha Polisi Bwanga Wilayani Chato katika Mkoa wa Geita ambapo alipokelewa na Mwenyeji wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, ACP Safia Jongo.
View attachment 2756068
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (Mb), akipokea taarifa ya kituo na hali ya Askari toka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita ACP Safia Jongo, wakati alipotembelea na kukagua Kituo kidogo cha Polisi Bwanga Wilayani Chato katika Mkoa wa Geita, Septemba 20, 2023.

View attachment 2756069
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea na kukagua Kituo kidogo cha Polisi Bwanga Wilayani Chato katika Mkoa wa Geita, Septemba 20, 2023.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na sisi wasaidizi wake hatutomvumilia mtu yeyote mwenye lengo la kuvuruga amani na usalama wa nchi yetu tutamshughulikia vilivyo bila kujali ni nani,” amesema Sagini.

Naibu Waziri Sagini amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoani Geita kwa kufanikiwa kudhibiti vurugu zilizoanzishwa na vijana dhidi ya Jeshi hilo kufuatia kuingilia kati kuokoa maisha ya raia aliyekuwa anashambuliwa na Wananchi kwa kutuhumiwa kuiba vifaa vya mziki msibani katika eneo la Bwanga Mkoani humo.

Pia ametoa rai kwa Wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwa kudhuru maisha ya wenzao kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai na kuwataka kuimarisha shughuli za polisi jamii kwa lengo la kuimarisha usalama, kudhibiti uhalifu na kuepuka kujichukulia sheria mkononi.
View attachment 2756070
Sehemu ya Askari wa Kituo kidogo cha Polisi Bwanga Wilayani Chato katika Mkoa wa Geita, wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini, wakati alipotembelea na kukagua Kituo hicho Septemba 20, 2023.

Aidha, amemtaka Kamanda wa Polisi na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama Mkoani humo kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa maisha ya watu na mali zao.

Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita ACP Safia Jongo, amemshukuru Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kufika kituoni hapo huku akimuhakikishia kuwa hali ya usalama mkoani humo ni shwari na wale wote wenye kuleta viashiria vya uvunjifu wa amani watashughulikiwa.
View attachment 2756079
Askari wa Kituo kidogo cha Polisi Bwanga Wilayani Chato katika Mkoa wa Geita, wakionesha ukakamavu mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini, wakati alipotembelea na kukagua Kituo hicho Septemba 20, 2023.
NB: Na wanaobambikia kesi raia kukiona cha mtema kuni!!
 
Huyo Naibu aanze na wezi wenzake wa Kalamu. Maana ifike mahali na wao waanze kushughulikiwa na raia moja kwa moja. Sheria imeshindwa kuwashughulikia kabisa
 
Nadhani hapo keyword ni Sheria mkononi..., hayo mengine ni immaterial...; Iwe mwananchi, raisi au huyo mwenyewe aliyetoa hii statement (hakuna mwenye haki ya kujichukulia sheria mkononi)...

Na hicho watakachokiona ni kwa mujibu wa Sheria ama ?
 
Back
Top Bottom