Jeshi la Polisi Mwanza fanyeni ukaguzi wa magari ya shule ili mabovu muyaondoe barabarani

Kangosha

Member
Sep 18, 2023
19
45
Kwa mara kadhaa nimekuwa nikikutana na magari specific kwa ajili ya kubeba wanafunzi jijini Mwanza yakiwa mabovu haswaaa.

Saa nyingine nakuwa najiuliza hivi Trafic barabarani hawayaoni?'. Unakuta gari hata indicator hazifanyi kazi ila lipo barabarani.

Kuna siku gari ya wanafunzi ilikuwa inakatiza kulia pasipo hata kuwasha indicator almanusura inisababishie ajali. Ilibidi nirudi kumfuata yule dereva kumuuliza dhumuni la kukatiza bila ishara ndio akaniambia kuwa indicator hazifanyi kazi.

Niombe jeshi linalohusika na kusimamia usalama barabarani liangalie magari yote mabovu yanayobeba watoto wetu ili yakarabatiwe ama yazuiwe kutembea kabisa. La sivyo ipo siku itatokea majanga kama vile ambavyo yamewahi kutokea huko nyuma kwa magari yanayobeba wanafunzi kupata ajali na kuua watoto wetu.
 
Back
Top Bottom