Jeshi la Polisi lazuia mkutano wa Mbowe, atakiwa kuripoti Polisi Kinondoni

Mwanzoni nilijua kuwa mtu ndo anatakiwa kuwa na hofu na serikali. Lakini serikali saiv ndo ina hofu na watu.

Mawazo hayajawahi kupelekwa Osterbay - Nyerere

Sent using Jamii Forums mobile app
Mfumo wa undeshaji shuguli za kijamii unamlazimisha Mtendwaji afanye shuguli zake vile wewe unavyotendwa.Ukiwa unaendesha shuguli zako kwa kibri na fitina na wenzako watakufanyia vivyo hivyo. Tegemea mengi ya kumdhalilisha Mbowe kwani yeye ndivyo anavyo wafanyia wenzake.
 
Sasa kwanini muliruhusu vyama mbadala au mlikuwa mnawadanganya wafadhili?
Boss sina la kukusaidia maana naona uko mbingu nyingine!
Vyama vingine walioruhusiwa kwani waliambiwa nao wanatawala nchi? Mwambieni asubili awe rais ndo atoe hotuba za kitaifa. Sasa hivi ahutubie wanachama wake, Tafadhari!
 
Boss sina la kukusaidia maana naona uko mbingu nyingine!
Vyama vingine walioruhusiwa kwani waliambiwa nao wanatawala nchi? Mwambieni asubili awe rais ndo atoe hotuba za kitaifa. Sasa hivi ahutubie wanachama wake, Tafadhari!
Sasa kwenda kinyume na katiba na sheria eti kuwa ni chama tawala?
 
Na yeye mbambikieni mtori unaosadikika kuwa na gram 23.5 za Heroine ili mfurahi
 
mbowe anazingua nitaanza kumuamini RC Makonda sasa, kwani siku 14 zimeisha?? aliwatangazia wabunge wa chadema kwamba wakae dodoma wote wala wasitoke hadi siku zipite wapimwe wajiridhishe...sasa huko dar amefikaje kama sio UHUNI HUU?. Yeye ndio angekua mstari wa mbele kutii kauli yake

Namshauri RC Makonda asweke watu ndani hata masaa matano tu yanatosha, atakuwa amewasaidia kuelewa japo kidogo tu hayo maneno yao. Akamate awasweke ndani hata wakitoka siku hiyo hiyo watakuwa wameshapata usumbufu ambao wamejitakia wenyewe
 
Mh. Mbowe ni lazima aungwe mkono na watanzania wote sababu ndiye kiongozi no moja wa upinzani wa kweli nchini kwetu.

Najaribu tu kufikiri kama CDM isingekuwepo nafikiri hata Rais ansingekuwa huyu tulienaye sasa, kazi iliyofanyika 2015 ilikuwa pevu..CCM kuna wakati pumzi ikawaishia kabisa!! Na kama tume ingekuwa huru tungekuwa tunaongea mengine wakati huu.

Watanzania tutajuta, kilio cha kusaga meno kama CDM itasema sasa YATOSHA tuwaache watawale watakavyo...pamoja na hao wapinzani mapandikizi wao.

Anyway, kupanga ni kuchagua....sasa Je moto uwake kudai Tume Huru kabla ya uchaguzi Mkuu? Au tukubali kurejea chama kimoja 2020?
 
Wewe ukiambiwa unatakiwa kuripoti polisi sasa hivi utaendelea na mkutano? Tupo kwenye uongozi mbovu sana wa nchi na inabidi watu waombe Mungu sana manake tunaelekea sipo.
Hapajaharibika kitu.
Si akitoka huko polisi ataanda mkutano mwingine ili awasilishe ujumbe, kwani haraka ni ya nini!

Mhimu ni ujumbe anaotaka kuwafikishia wananchi aufikishe.
Polisi wakiendelea kuzuia, itafahamika ni kusudio la kuzuia ujumbe usifike kwa wananchi. Hapo atakuwa na haki ya kutafuta njia mbadala ambayo polisi hawana uwezo wa kuzuia ujumbe kwenda kwa wananchi.
 
Hapajaharibika kitu.
Si akitoka huko polisi ataanda mkutano mwingine ili awasilishe ujumbe, kwani haraka ni ya nini!

Mhimu ni ujumbe anaotaka kuwafikishia wananchi aufikishe.
Polisi wakiendelea kuzuia, itafahamika ni kusudio la kuzuia ujumbe usifike kwa wananchi. Hapo atakuwa na haki ya kutafuta njia mbadala ambayo polisi hawana uwezo wa kuzuia ujumbe kwenda kwa wananchi.
Si umeona mpaka jioni hii polisi wameshindwa kusema kwanini wamemzuia kamanda Mbowe asifanye mkutano na waandishi wa habari. Kweli magu mwoga wa CDM. Kitajulikana tu peoples..............!
 
Tuliosema warudishe posho wabunge wa chadema waliojifanya wako Lockdown hatukukosea wako Dar wanajirusha Mbowe huyo yuko Dar hayuko dodoma

Hapa Dar kuna kipi kipya cha kujirusha tena kwa mtu aliyekulia hapa mjini? Labda washamba ndio wataacha majukumu yao kuja kujirusha hapa Dar.
 
Wananchi wanachezewa akili,,,akili za mwafrika anazijua mwenyewe,,,hata akiongozwa na punda kwake sawa tu,,,japo ccm wana madhaifu yao lakini chadema haiko kwa ajili ya wananchi bali wanajinufaisha wenyewe na kuwazuga wa2 wake,,,,viongozi wengi wamekimbia, lowasa, sumaye, slaa, na wabunge na madiwani chungu mnzima wamekimbia na kurudi ccm.


Acheni udin na ukabila ndio mutafika munakotaka


Hivi kuna ndugu zangu wasukuma wamepewa kanafasi pale??? Hata kaudiwani tu!! Sidhani. Waabeja sana
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ameshindwa kwenda kuzungumza na waandishi wa habari baada ya magari ya polisi kumzuia asitoke nyumbani kwake.

Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni leo alitangaza kuzungumza na waandishi wa habari majira ya saa 5:00 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, kupitia ukurasa wake wa twitter imeeleza kuwa baada ya polisi hao kumzui ametakiwa kwenda kuripoti kwa kwa Mkuu wa Upelelezi Kinondoni.

Mdee amesema kuwa Mbowe ameshikiliwa kwenye kituo cha polisi cha Oysterbay.

Screenshot_20200515-003948_Opera%20Mini.jpeg
 
Back
Top Bottom