johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,978
- 141,994
Wakili Boniface Mwabukusi na mwanaharakati Mdude_Nyagali ambao walikuwa na mkutano na waandishi wa habari leo jijini Mbeya wamekamatwa na jeshi la polisi.
Wawili hao walikuwa wakizungumzia maandalizi ya maandamano ya kupinga mkataba wa bandari na madai ya kupatikana kwa katiba mpya. ambapo mara baada ya mkutano na waandishi wa habari, jeshi la polisi lilifika na kuwakamata wazungumzaji hao pamoja na waandishi wa habari wanne.
Habari za hivi sasa zinaeleza, hao wote waliokamafwa wamefikishwa katika kituo kikuu cha polisi Mbeya ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mbeya.
Wakili Boniface Mwabukusi na mwanaharakati Mdude_Nyagali wamekuwa wakipinga mkataba wa bandari na kufikia hatua ya kuitisha maandamano kupinga mkataba huo.
Waandishi wa habari waliokamatwa ni Ipyana Samson, Ahadi Mtweve, Isack Kyando nami Josea Sinkala.
Itakumbukwa Oktoba 22, 2023 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma mikataba mitatu ya uwekezaji na uendelezaji wa bandari ya Dar es Salaam lisainiwa kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya DP World mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan
Chanzo: Jambo TV