Jeshi la Polisi Dar es Salaam latoa angalizo kwa wanaotaka kufanya uhalifu wakati wa Pasaka

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kusimamia mifumo ya kiusalama ya kuzuia matukio ya kihalifu, kwa ujumla hali ya Dar es Salaam ni shwari. Hata hivyo Polisi hawatasita kuendelea kufuatilia na kuwakamata watu wanaopanga njama na kutenda matendo ambayo ni kinyume na sheria za nchi.

Jeshi linaendelea kutahadharisha juu ya kuwepo kwa mtizamo kuwa kila inapokaribia sikukuu mbalimbali ikiwemo (Pasaka) baadhi ya watu hujenga fikra za kujihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kisingizio kuwa wanatafuta pesa za sikukuu.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam halikubaliani na hali hiyo. Ufuatiliaji wa mambo mbalimbali ya usalama upo katika kiwango cha juu na yeyote atakayejihusisha na vitendo vya kihalifu atakuwa amejiweka katika msuguano mkali na mifumo ya kisheria na atakamatwa, atahojiwa kwa kina na baadae atafikishwa kwenye nyombo vingine vya kisheria kulingana na ushahudi utakao kuwa umekusanywa.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, SACP Muliro Jumanne amesema wanawashauri watu kuachana na vitendo vya kihalifu na linaendelea kuwashukuru wananchi wanaochukia uhalifu na kuendelea kutoa taarifa mapema ili wahalifu waweze kushughulikiwa haraka kwa mujibu wa sheria.
 
Hivi wametoa taarifa yeyote kwa yule jamaa yao aliekimbilia SA na kuacha Ada huko CCP Moshi...
 
Back
Top Bottom