Jeshi La Kujenga Taifa Latangaza Nafasi za Mafunzo

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
eshi la Kujenga Taifa JKT limetangaza nafasi za kujiunga na mafunzo ya kujitolea kwa mwaka 2023 kwa Vijana wa Tanzania Bara na Visiwani kuanzia August 28,2023 na watakaofanikiwa wataripoti kwenye makambi kuanzia Septemba 26 hadi 29, 2023

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Tawi la JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena kwa niaba ya Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele ambapo amesema utaratibu wa kuomba na kujiunga unaratibiwa na Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambako Mwombaji anaishi.

Akisisitiza namna ya kujiunga ametoa rai kwa watanzania kuepuka Matapeli “Inasisitizwa nafasi hizi zinatolewa bure hakuna malipo yoyote yatakayoambatana na nafasi hizi hivyo Wazazi na Walezi wote nchini waepukane na Matapeli wanaojitokeza kwamba nafasi hizi zinauzwa”

Kuhusu sifa Brig. Jen. Mabena amesema nafasi hizo zimezingatia Vijana wenye taaluma za Uhandisi wa Ujenzi (Civil Engineers),Ufugaji, Umwagiliaji, Uvuvi, Saikolojia na Wanyamapori ambao wanashauriwa kujitokeza kwa wingi kupitia Mikoa yao.

F4X-v7oXEAAMsxL.jpeg
F4X-waEWAAAscPy.jpeg


F4X-w1FWkAI6E5M.jpeg

F4X-xVFXkAAMtIW.jpeg
 
Kama huna mtu wa kushika mkono ukiwa jkt usijisumbue kwenda. Utahenyeka Bure na kurejea mtaani ukiwa mkakamavu unaanza kuendesha boda.


Jeshi Kuna undugu sana, wanakijji wa mabeyo hawakwenda hata jkt waliibukia rts
 
Back
Top Bottom