Jerry Silaa, mbona hututembelei Manzese na Tandale, au kwa Mpalange unapita pita maeneo ya matajiri tu, hatukuoni vijijini!

Huyu dogo kazi itamshinda. Nchi ya watu milioni 60, uanze kutembelea kiwanja kimoja kimoja. Utamaliza lini mogogoro ya viwanja ya nchi nzima. Mliokaribu nae mshutueni.
 
Najua kwamba katika moja ya mambo ambayo SSH alitilia mkazo, ni ile migogoro yenye sura ya kitaifa, vijiji na hifadhi za taifa, vijiji na mapori, maeneo ya serikali na wananchi, na mengine kama hayo, akaunda kamati ya kitaifa ya mawaziri.

Mbona ndugu Silaa hajihusishi na hayo ambayo SSH aliyatilia nguvu, tena yana sura ya kitaifa na yanahitaji utatuzi wa wizara zaidi ya moja, na wizara yake ndio mwenyekiti wa kamati hiyo?

Kwa nini anatembea katika maeneo ambayo kizungu yanaitwa posh areas, za wenye nazo,akina Diamond Platnumz, kuna nini huko? Mbona hatumuoni Tandale? Kwa Mpalange? Au kwa kuwa hawana chochote?

Kule wilaya ya Bunda,Nyatwali, kuna mgogoro wa wananchi na hifadhi,Tarime wanataka kuuana na watu wa hifadhi, kule Mbeya, sijui ihefu, kuna jambo kubwa kati ya wananchi na hifadhi, kila mahala, tena migogoro yenye sura ya kitaifa, yanahitaji uamuzi wa kitaifa, kwanini anakesha kwenye vichochoro vya matajiri, kiwanja skwea mita 500, na ambao ukiwatisha wanakupiga tena(kikbaki)?

Migogoro yenye sura ta kitaifa inahusisha maelfu ya wapiga kura wa SSH. Hata Kigoma, Kagera kwa Mwijage, kila mahala. Morogoro Rais alitoa agizo mashamba aliyoyatwaa wagawiwe wananchi, mbona hakuna hata mkakati wa matumizi bora ya ardhi? Kule Rukwa, askofu kachukua kijiji kizima, mbona huendi huko?

Dotto Biteko anataka vyanzo vya maji yanayoenda Bwawa la Mwalimu Nyerere vilindwe, mkakati wake ukoje kwa upande wa wizara yake? Ataweka beacons na kupima ili wananchi wajue maeneo ambayo hawaruhusiwi? Au ndio siasa za bei chee na kukodi waandishi na kuwapa.......

Kwa nini hatembei na mawaziri wenzake atatue kero za kitaifa? Ile kamati ya Rais ilitoa mapendekezo na utekelezaji, Mama Anje na Lukuvi walikuwa wanakaa kutwa vijijini wakiwa na wakuu wa wilaya na mikoa wanapima maeneo yenye shida na kutoa suluhu, Silaa yeye ni Mikocheni na Mbweni, hayaoni hayo anabaki kutembea Mikocheni na Mbweni?, posh areas wanakoishi bilioneaz?
🤔💭 🔭📝
 
Hata mikocheni kuna skwea mita 500, acha Bunju huko kwa wachoma mikaa, na unainunua kwa bei mzito
Sasa billionaire ugombanie sqm 500 kwa wachoma mikaa? Wewe ni billionaire au millionaire au mnyonge?
 
Ni waziri mshamba asiyejua majukumu mtu wa kujikweza hana lolote
Tanzania ina viongozi wengi wasiojua majukumu yao na wengi hatuoni hilo au tunaona ni sawa
Hii mada ni mfano mzuri namna anavyodeal na migogoro ni sawa na mtu asiye na level yoyote ya elimu ndiyo anaweza kufanya mambo kama yeye hajui afanye nini
Serikali yetu haina mipango kabisa na imewashinda hawa watu

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom