Jengo la PSPF mita 134 ndo Refu Tanzania, Wenzetu wanajenga Jengo lenye Urefu wa Mita 1,700 huko Tokyo

Japan na China ni kama Tanzania na Kenya. Kila mmoja anaetaka aonekane yuko mbele ya mwenzake. Lakini ki ukweli ardhi ya Japan ni ya mashaka sana, wakiendelea kutaka kushindana na China kwa kila kitu. Basi kuna siku watakuja kuwaangamiza raia wao kwa kujenga vitu ambavyo havitaweza kuvumilia tetemeko lolote litakalotokea.
Hakika baada ya mapinduzi ya fedha yao nilifikiri japan atatambua kuwa kumzidi uchina tena ni jambo lisilowezekana kutokana na ukubwa wa uchina
 
Tanzania wapangaji wa magorofani wachache sana.
Lile la mawasiliano tupu.
Yale ya Moroco sijui wataanza kupangisha lini maana toka 2016 huko yapo tu na yamekamilika.
Kuna chuo kilipanga KKKT Kinondoni toka kilivyohama hapajapangishwa tena.
 
Hii Japan si ndo juzi tu kumetokea tetemeko kwenye mji wa Kumamoto na kuua watu?! Anyways Tanzania magorofa marefu ya nini wakati nje kidogo tu ya miji mikubwa kuna mapori kibao. Kibongo bongo maeneo yaliyokaliwa na watu ni madogo kuliko yaliyo wazi. Kingine majanga ya moto, nyumba tu za chini kukitokea majanga ya moto hua tunashindwa kuzima, leo hii mtu anaongelea jengo la mita 1700, Mzee si itakua unajenga tu makaburi ya kuzikia watu na mali zao?!
 
Ni ulimbukeni fulani.

Tunajifananisha na Tokyo, wenzetu hawana ardhi na hivyo wanalazimika kujenga kwenda juu.

Wana uchumi unaohitaji ofisi zaidi. Wana umeme mpaka wa nuclear. Wana zimamoto za kueleweka mpaka kufanya kazi kwenye matetemeko ya ardhi.

Sisi tunataka kumuiga tembo kunya tu, tutapasuka msamba.
Hapo tu Victoria maghorofa kibao yapo empty,,, mengine wamejaribu kupangisha watu waishi wananchi hawa afford gharama
 
Back
Top Bottom