Jee waandishi wa habari wa Tanzania wana-abuse power waliokuwa nayo?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jee waandishi wa habari wa Tanzania wana-abuse power waliokuwa nayo??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by tHe NapSTer of Tz, Aug 7, 2008.

 1. tHe NapSTer of Tz

  tHe NapSTer of Tz Member

  #1
  Aug 7, 2008
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JF,

  Watanzania wengi wanapoamka asubuhi kwenda ofisini, kabla hawajaingia ofsini wanatupa macho yao kwenye vichwa vya habari vya magezeti!!!

  Tukiangalia kwa kina tutaona kwamba waandishi wa habari wa Tanzania wananguvu kubwa sana. Yaani mpaka hatari! Waandishi wa habari wamekuwa wakimanipulate habari nyingi na tukizipindua wanavyotaka wao!..

  Watanzania wanasoma sana magazeti. Na infact wanaamini sana magazeti!

  Waandishi wetu wakobiased ile mbaya!...... Hawa hawa waandishi wanaotuandikia habari za viongozi mafisadi wao wenyewe wengi wao ni mafisadi na wanafanya kazi na hao (hidden) expert fisadis!...

  Waandishi ama mass media ni chombo muhimu kwenye jamii!!! Jee tunakubali kutawaliwa na waandishi waongo,mafisadi na wanafki waliokosa uzelendo kazi kuchochea fitna na uhasama baina yetu?
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Aug 7, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Toa mifano kidogo (mingi siyo vibaya) ili kujenga kesi yako au kile unachobase swali lako. Na kwa vile wamo humu nina uhakika hawatasita kukujibu.
   
 3. tHe NapSTer of Tz

  tHe NapSTer of Tz Member

  #3
  Aug 7, 2008
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  1. Kuna magazeti yanajulikana kwa ku RE-WRITE habari za zamani na kulichochea swala ambalo limetatuliwa au limepita just kuamsha hisia za watu na kuharibu jina!....
   
 4. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  The real question is "Kuna waandishi wa habari Tanzania?"
   
 5. tHe NapSTer of Tz

  tHe NapSTer of Tz Member

  #5
  Aug 7, 2008
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good question,
  And where were u when i was writing this post? Ungenikumbusha to ask this question!....
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,804
  Likes Received: 83,182
  Trophy Points: 280
  Waandishi wa habari wa Tanzania wengi wanafanya kazi vizuri kabisa, ukiondoa wahuni wachache wanaotumiwa na mafisadi kuandika kile ambacho mafisadi wanataka kiandikwe au kisiandikwe katika magazeti yaTanzania.

  Magazeti ndiyo yamekuwa mstari wa mbele kufichua uozo mbali mbali wa hali ya juu uliokuwa ukifanywa na viongozi mafisadi wangazi za juu akiwemo fisadi Mkapa. Wamekuwa mstari wa mbele katika kuibua uozo wa mbali mbali ndani ya BoT kama vile EPA, fisadi mkono kulipwa bilioni 8 ambazo hakustahili, fisadi Mzindakaya kupatiwa mkopo na BoT pamoja na kwamba BoT hawatoi mikopo kama hiyo bali benk za biashara, gharama kubwa kupita kiasi za ujenzi wa Twin Towers, kuajiriwa kwa watoto wa 'viongozi ambao hawana quaifications zozote za kuajiriwa BoT na mengi mengineyo yakiwemo ya mkataba wa Buzwagi, Richmond n.k.

  Hata mabalozi mbali mbali wa nchi za wafadhili zikiwemo US, UK, Holland, Germany, Denmark n.k. wamewasifia waandishi wa habari wa Tanzania kwa kufichua maovu mengi ndani ya CCM na SIRI KALI. Hata wanahabari wa CNN na BBC mashirika makubwa ya habari duniani huwa wanafanya makosa mara nyingi na kuomba samahani.

  Hivyo tusiwakatishe tamaa waandishi wa habari wa Tanzania ambao wengi wao wanafanya kazi yao vizuri sana ukiondoa wahuni wachache.
   
 7. tHe NapSTer of Tz

  tHe NapSTer of Tz Member

  #7
  Aug 7, 2008
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi bado napata shaka katika hayo ya kufichuwa maovu!... Wanafanya wao wynyewe au wanalipwa na wakubwa, na kambiwa nani wamharibie jina!... na kuongeza uongo kidogo!.....

  Maana ukiamuliwa kuondesha sehemu! waandishi wa habari ndio weapon nzuri....

  Habari wanazoandika ni SADIKI ukipenda!!!
   
 8. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  kituko cha TANZANIA DAIMA wikiendi hii:
  Ok inawezekana ikawa mara moja ni bahati mbaya...lakini huyu mwandishi wa gazeti la Mbowe akakisha likaendelea kuonyesha ujinga na uvivu wa kufikiri na kufanya research kwa kudai hivi:
  UKWELI WA NANI MWENYEKITI WA BODI YA NSSF HUU HAPA:


  http://www.nssf.or.tz/board_of_trustees.php


  Jamani tuache ushabiki halafu tuangalie hili gazeti FREEMAN MBOWE LINAVYOOAJIRI makanjanja  hivi huyu kweli ndio Dr MUSSA HASSAN au kajibadilisha?
  [​IMG]
  Mrs. Blandina Nyoni
  Board Chairperson
  National Social Security Fund
  Dar es salaam


  hivi wanashindwa kuingia JAMII FORUMS kutafuta referencing kama KUBENEA na MWANAHALISI?

  What a shame!
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,804
  Likes Received: 83,182
  Trophy Points: 280
  Wewe kama bado unapata shaka hilo ni tatizo lako, lakini wengi wa Watanzania tunaamini kwamba waandishi wengi wa habari utendaji wao wa kazi ni mzuri. Naam wako wahuni wachache wanaotumiwa, lakini huwezi kuwachafulia majina watu kama RA, Lowassa, na Mkapa wakashindwa kuja na ushahidi wa kuonyesha kile kilichoandikwa na magazeti ni uzushi mtupu!!!! Na siku zinayoyoma bila kusikia chochote toka kwao

  Tulisikia RA kuwashtaki Mwanahalisi kwa kumchafulia reputation yake, lakini hadi hii leo hajafanya hivyo. Tukasikia tena Lowassa akitamka kuwashtaki hao hao mwanahalisi hadi hii leo hajafanya hivyo!!! Tukasikia tena kwamba fisadi Mkapa atayashtaki magazeti yote yanayomchafua kuhusiana na ufisadi alioufanya wakati akiwa Ikulu, hadi hii leo bado n bubu na hata anazikacha shughuli za chama na serikali ambazo alistahili kuhudhuria.

  Mabalozi toka nchi za wafadhili walikuwa wanasoma Newsweek, Times, The Guardian la UK na magazeti mbali mbali ya nje lakini hivi sasa wanasoma baadhi ya magazeti yetu yakiwemo THIS DAY, THE CITIZEN na mengineyo na kusifia yale wanayasoma ndani ya magazeti hayo
   
 10. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Lakini siku za nyuma kuna mwana JF alitoa analysis juu ya waandishi Tanzania na alimzungumzia mhariri wa TANZANIA DAIMA au tuseme gazeti la FREEMAN MBOWE kwa kusema hivi:
  source: https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=13378&highlight=Stan+Katabalo

  need i say more?
   
 11. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #11
  Aug 8, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  GT
  watakwambia wewe ni mnafiki na huwatakii mema ktk mafanikio ya kisiasa na kihabari,kwani wewe hujui kua Tanzania daima ndilo gazeti pekee ambalo halitumiwi na RA na siku zote linaandika ukweli mtupu.
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Aug 8, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,804
  Likes Received: 83,182
  Trophy Points: 280
  Kama nilivyosema kuna wahuni wachache katika fani ya uandishi kama ilivyo katika fani yoyote ile Tanzania na hata duniani zikiwemo uhandisi, uhasibu, udaktari n.k. Pamoja na kuwa na hao wahuni wachache waandishi wa habari wengi wanafuata miiko ya taaluma na wanafanya kazi nzuri sana ambayo imetufahamisha uozo mwingi na wa kutisha uliofanywa na mafisadi ndani ya chama na serikali hata kumwagiwa sifa kem kem na mabalozi wa nchi mbali mbali za wafadhili na hata baadhi ya wabunge wa bunge letu uchwara wamewamwagia sifa kem kem. Sikubaliani na msemo usemao kwamba "samaki mmoja akioza basi wote wameoza" Kuna wahuni wachache katika taaluma hiyo lakini kuwatuhumu waandishi wa habari wote kamwe si kuwatendea haki hata kidogo wale wengi ambao ni wazuri.
   
 13. tHe NapSTer of Tz

  tHe NapSTer of Tz Member

  #13
  Aug 8, 2008
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I wish wangekuwa wachache katika hao.
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Aug 8, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ngoja nishangae kwanza. Mwanzisha thread amezungumzia WAANDISHI wa habari. GT analishambulia Tanzania Daima. Naomba mwongozo, tujadili nini?
   
 15. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #15
  Aug 8, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  waandishi wao wenyewe hawana maadili, wanafanya mambo ya kifisadi na kihuni. wakifika kwenye makazi yao wanayaendeleza tu
   
 16. m

  mgirima Member

  #16
  Aug 8, 2008
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sawa. Hakuna waandishi wa habari TZ.

  Lakini tujiulize, ni fani ipi hapa TZ ambayo inaweza kusimama kidete kudai ina mchango mkubwa kwa wananchi wa TZ.

  Engineers ndio hao wanaoishia kujenga barabara/magorofa zisizo na viwango; Accountants ndio hao embezzlers na wanaosaidia wakwepaji kodi wakubwa; Doctors wanaopasua mguu kwa mgonjwa wa kichwa; Lecturers/Teachers wanaoendekeza maksi za chupi; Town Planners wanaogawa Plots moja kwa zaidi ya wamiliki wawili; Bankers wanaomtoza mfanyakazi riba ya 18% wakati ana guarantee ya mwajiri hivyo mkopo huo kuwa almost risk-free; Judges/Mahakimu wenye kutoa hukumu za utata. Kifupi ni kuwa fani zote hapa nchini zina watu wachache tu walio makini na fani zao. Big % ni wabangaizaji tu. Tusiishangae fani ya Journalism tu!
   
 17. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #17
  Aug 8, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  http://www.freemedia.co.tz/daima/2006/9/7/habari35.php

  Lakini hii si sehemu ya mjadala wa aliyeanzisha, turudi kwenye mada
   
 18. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #18
  Aug 8, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mkamap na mwenzio GT, munajikaanga kwa mafuta yenu. Hiyo mada ya huo waraka wa kina Mkapa na wenzake, ulijadiliwa kwa kina murudi na kuisoma vyema. Tukirudi kwenye mada husika kuhusu waandishi wa Tanzania, nadhani mukiwa munatenda haki, munaweza kurudi na kuangalia habari zote zilizoandikwa na Majira na Rai kwa wiki mbili zilizopita, mutaona ni aibu tupu. Angalia Majira habari walizoandika kuhusu Wangwe, utaona siku ya Press Conf ya Kina Lipumba waliandika stori na baada ya siku mbili wakarudia habari ile ile tena kwa uzito mkubwa, hapo sijui hao ndio wanaokusudiwa kuandika habari kwa kutumwa, au munazungumzia kina nani? Angalia Majira wanaandika wakimnukuu Paul Kyara, bila kuwaambia wasomaji Kyara ni nani na alitokea wapi kabla ya kuanzisha chama chake na kauli zote za Kyra zina mrengo gani!! Huo ndio mfano hai wa uchafu katika fani ya habari. Vinginevyo urudi nyuma na mifano hai ya jinsi, Sumaye, MWandosya, Malecela, Kitine, Kigoda, Dk. Salim na wengine wengi walivyoathiriwa vibaya na matumizi mabaya ya vyombo vya habari na walioshiriki kutunukiwa japo sasa wameonekana udhaifu wao na mifano ipo wazi. Vinginevyo musilete mjadala wa kujadili HEWA toeni mifano watu wajadili na kuona PUMBA na MCHELE ni upi
   
 19. tHe NapSTer of Tz

  tHe NapSTer of Tz Member

  #19
  Aug 8, 2008
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yeah u ryt,.......

  Hey i didnt start this thread beacause i hate waandishi ila ni kwamba tunapokwenda ni pabaya. Mwaandishi ikiwa atakubali kutumiwa kuharibu na kuchafua jina kwasababu binafsi maanake tunakaribisha civil war!!! Jamani tuangalie!

  Wana JF wengi ni wasomi (wanayajua kupambanua) kuna watu wanameza kila wanacho kiona kwenye gazeti! Tuandike habari inavyotakiwa, tusitie watu hamasa!...
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Aug 8, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mimi ni mpenzi sana wa vyombo vya habari. Siku yangu bila kusoma gazeti au kuangalia TV, inakuwa haijapita sawasawa.
  Lakini nachelea kukuunga mkono moja kwa moja kwa sababu umegeneralise.
  Ni wkeli wapo waandishi wa aina unayoisema lakini si waandishi wote. wapo ambao wamejichanganua na wanatambulika kwa kazi zao. tatizo ni kuwa hata kwa hao, wanahukumiwa na misimamo ya wanaowasoma. Mtu huijudge habari kutokana na msimamo wake yeye na si ukweli au uongo uliopo katika habari hiyo.
   
Loading...