Waandishi wa Habari wa Michezo Tanzania acheni Unafiki na Upuuzi

Cognizant

JF-Expert Member
Aug 13, 2022
491
1,056
kabla ya Taifa Stars kucheza na morocco leo katika michuano ya AFCON huko nchini ivory coast waandishi wa habari za michezo wa Tanzania walituaminisha kuwa morocco atafungwa tu huku wakiwapa sifa kem kem za uwongo na kweli wachezaji wa Taifa Stars na kuna wapuuzi na majuha waliwaamini

Cha kushangaza kama siyo kusikitisha baada ya mechi ya taifa stars na morocco kumalizika hivi punde tu waandishi wa habari wale wale wamegeuka na sasa kwa umoja wao uliojaa unafiki na upuuzi mwingi wanasema taifa stars imekutana na timu ngumu na kubwa hivyo kufungwa ilikuwa ni suala la muda tu na la lazima

Mmeshaona kabisa cognizant mimi mapema tu nimezitakia kila la kheri Morocco, Zambia na congo dr nyie mmepata wapi jeuri ya kupinga nilichokisema kuwa taifa stars itafungwa mechi zote katika kundi lake na kama utapata alama basi labda ni moja tu kwa kubahatisha sare au suluhu hasa hasa kutoka kwa zambia ila kwa congo dr yenye majembe ya uhakika tusipokuwa makini tunaweza hata kufungwa nao goli 5

Mnaacha kuandaa timu ya taifa kisayansi nyie kutwa mnaendekeza siasa, kutafuta sifa za kijinga, kuunda kamati za wapigaji na kuamini miujiza kama waumini wa mwamposa

leo nina furaha isiyo ya kifani
 
Waandishibwa habari wa michezo wana changamoto ya kuwaza namna ya kuuza habari kuliko uhalisia wa habari yenyewe. Mchezaji atapewa sifa nyingi ila kiuhalisia ni wa kawaida tu.....tuna safari ndefu
 
Wachambuzi wa mpira na waandishi wa habari hasa za kimichezo hatuna, alikuwepo mwalimu kashasha na doctor liki basi
 
Back
Top Bottom