Je Zanzibar imewahi kuwa Koloni la Waarabu au la Watanganyika?

Hapa tatizo si utumwa wa kiarabu bali ule wa watu kujitakia kuwa watumwa kama sasa ambapo waswahili wengi wenye ngozi maji ya kunde hujiona waarabu zaidi ya waswahili. Mie sioni kosa kwa wazanzibari kutaka kuishia mradi wasirudi mambo yatakapowashinda kama wenzao wa Comoro. Kila la heri nendeni salama ila mwendako siko wanangu. Laiti mgejua kuwa si kila ving'aravyo ni dhahabu!

what shall they do??? Jee waendelee kudhalilishwa na hii sytem iliojaa mafisadi, wezi kwa kisingizio cha muungano na uafrika ??
 
WAnasema Zanzibar ni koloni la TAnganyika; wanatuita watu wa bara kuwa ni "wakoloni"; wanasema bila hata kufikiria kuwa ati Muungano hauna uhalali kwa vile hakukuwa na kura ya maoni; kwamba ati "watu waulizwe" kwanza ili wajue wanataka nini. Hawa hawa hawaelezikama Sultani alipigiwa kura na Wazanzibari kuwa SUltani wao? Hawa wanaamini Sultani alikuwa na uhalali wa kutawala Zanzibar hata kama Sultani huyo hakupigiwa kura, wala wananchi wake kuulizwa kama wanataka aendelee kuwatawala.

Hivi, kabla ya uhuru wa 1963 Wazanzibar walipiga kura ya maoni kuhusu kuendelea kwa Sultani kama "constitutional monarchy" au nani aliamua hili?

Naona umeishupalia sana Zanzibar, haipiti siku mbili tatu lazima uanzishe ufataani kuhusu Zanzibar. Hivi wewe Zanzibar inakuhusu nini? Au ni rafiki wa Fred Mercury?
 
Mzee Mwanakijiji, unajaribu kupotosha malengo na dhamira ya Wazanzibar katika kujikwamuwa kutoka kwenye makucha ya muungano kwa makusudi. Nna kila sababu ya kuamini kwamba unaouelewa wakutosha wakile wanachokidai Wazanzibar, ila kupitia makala zako hizi ulizo zifululiza ukiongozwa na chuki, choyo na husda dhidi ya Wazanzibar (kwa sababu ya udini uliokujaa), unaamuwa kuyageuza malengo ya madai yao na hata kujipumbaza na kujifanya huna akili zakung'amuwa wakidaicho wazanzibar!

Kuna uhusiano gani wa madai ya sasa ya wazanzibar ya kutaka dola yao huru na usultan? Mbona unajidhalilisha Mze Mwanakijiji, sababu hizi makala zako ni chini ya uwezo wako wakufiri niujuwao! Hata ikiwa sultan hakutawala kwa kura ya maoni, does it justify uwepo wa muungano usio ridhiwa na upande mmoja? Hivi alokwambia wazanzibar wanataka kuvunja muungano iliwatawaliwe na sultan ni nani? Mbona upeo wako wakufikiri ni mkubwa kuliko hayo uandikayo Mzee? Hivi propaganda hii uenezayo unafikri itaathiri kwa namna yoyote mapambano yakudai Zanzibar huru yanayoendelea zanzibar? Au unadhani CCM wa zanzibar (wa hafidhina) watatishika na hivyo basi watazidi kuwakumbatia watanganyika? Unapoteza muda Mzee hizi nyimbo zako si ngeni masikioni mwa Wazanzibar, "zilipendwa hizi"! Zimeimbwa wakati wasiasa za chuki na uhasama na bado hazikuathiri kitu, hivi sasa CUF na CCM wameunda serikal ya Umoja wa kitaifa! Nyimbo hizi zimebaki kuwa hekaya kama vile Adil na Nduguze, Ali Babaa n.k! Wazanzibar wakizisikia huona mtoaji wa hadithi hizi ) kama mtu alofufuka kutoka kuzimu, amepitwa na wakati! Sasa tupo zama za kizazi kipya, chenye maono na dira mpya...ZANZIBAR HURU!

Hivyo Mzee Mwanakijiji nakushauri badala yakuendelea kujidhalilisha kwa kuandika makala zisizo na viwango (kulingana na upeo wa akili yako) kwa lengo la kuwafitinisha Wazanzibar, ni bora ukaendelea kuandika "vitabu vya mapenzi" kama hicho ulichokitoa hivi karibuni! Kinyumeche utapoteza wateja wa hata hivyo vitabu vya mapenzi, kama wataendelea kusoma utumbo unaoandika hapa JF kuhusu zanzibar! Wata "doubt" hata hayo uandikayo kwenye mapenzi!
 
si kwanza uijue hii uliyozaliwa nayo ndio ushughulikie iliyopita ambayo kila mmoja ana his story yake.

Vijana wameshaona wanadanganywa na kuibiwa rasilmali zao,huku wao wakiwa na hali duni za maisha. Yule wanayemchagua ni sisi watanganyika ndio tunawaamulia nani awe kiongozi wao.

Huo kama si ukoloni waite nini???

Hata mimi ingalikuwa wazanzibari wanatufanyia hivyo nisingalikubali,
This is too low! ukifanya hivyo unaweza usimtambue adui wako wa kweli! utakuwa kama mjinga anaeenda kwa mganga wa jadi kupiga ramli iliajue chanzo cha maradhi yake, mpiga ramli ataishia kumgombanisha na mama yake mzazi kuwa ndie anae mroga! Vijana wanashauriwa kuifuatilia historia yao na sio kuhamaki kwa kusikiliza hadithi za masangoma a.k.a wajomba toka............
 
Hivi, katiba iliyompa Sultani nafasi ya kuwa mkuu wa nchi baada ya Waingereza kuondoka ilipigiwa kura ya maoni na Wazanzibari? au iliandaliwa na nani?
 
Kabla ya mapinduzi ya 1964, wananchi wa Zanzibar waliishi kimatabaka ya waliokuwa nacho na wale watwana na wakwezi, Watwana na wakwezi walikuwa wengi zaidi kuliko watawala na mamwinyi ambao ndio walikuwa na nguvu. Historia inaonesha wazi kwamba nguvu ya umma daima hushinda ili mradi tu kuwepo na "effective organisation and mobilization".

Nguvu ya UMMA ipi hiyo inayoshinda? ni nguvu ya demokrasia ya kura iliyompa ushindi Shamte na kuwamwaga ASP au ni nguvu ya mapinduzi ya 1964 chini ya Okello (karume alijificha)? Ninauliza ili niweze kujua hiyo nguvu ilikuwa kwa ajili ya maslahi ya Sultan ambaye Wazenji wa sasa wanamhitaji na kuiona Tanzania bara kama ni watawala wao, au ni nguvu hiyo hiyo iliyokataa dhuluma ya Sultani na kufanya mapinduzi ya kumung'oa sultani na baadaye kufanya muungano na Tanganyika?
 
This is too low! ukifanya hivyo unaweza usimtambue adui wako wa kweli! utakuwa kama mjinga anaeenda kwa mganga wa jadi kupiga ramli iliajue chanzo cha maradhi yake, mpiga ramli ataishia kumgombanisha na mama yake mzazi kuwa ndie anae mroga! Vijana wanashauriwa kuifuatilia historia yao na sio kuhamaki kwa kusikiliza hadithi za masangoma a.k.a wajomba toka............

kwani wewe ukiibiwa nyumbani kwako utaanza kutafuta historia yako au utaanza kushughulikia hicho ulichoibiwa ???
 
Muungano una matatizo kibao la kwanza likiwa mkataba wa muungano wenyewe
.
Mkuu Madela

Matatizo haya ya Muungano yatatuliwa lini?
Kwani matatizo yenyewe ni yepi?
Ni ujinga kudhani Zanzibar ni koloni la Tanganyika wakati Tanganyika yenyewe hata katika ramani ya dunia au ya kisiasa haipo. Kinacho wapa tatizo wazanzibari leo hii ndicho hicho hicho kilicho iua Tanganyika.

Kitu gani kiliua Tanganyika?
JokaKuu anasema hivi:
..Tanganyika ipo, na wa-Tanganyika wapo. Kilichotokea, na kinachowanganya watu akili, ni kwamba shughuli za utawala ktk Tanganyika zilikasimiwa kwa serikali ya muungano mwaka 1964.

..Inawezekana kabisa kujadili haki za wa-Tanganyika ndani ya muungano huu. Wahusika wanajitia vichwa maji tu lakini sina shaka kabisa kwamba hilo linawezekana.
Sasa Tanganyika ipo? Au imekufa/imeuliwa? Au imebadilishwa jina?
Sijui waungwana wanaodai Uhalai wa Sultani wanaweza kutuambia ni Sultani gani duniani anayepigiwa kura??

Hilo ndilo swali alilouliza Mzee Mwanakijiji, mimi sijapata kusikia Mfalme , Malkia, Sultani kupigiwa kura sehemu yeyote duniani.
Lakini zaidi hata sultani wa Tanzania(CCM) hapigiwi kura,kura hazina uzito, ni kauli tu ya Mkuu wa NEC kutangaza nani atakuwa mtawala.
 
kwani wewe ukiibiwa nyumbani kwako utaanza kutafuta historia yako au utaanza kushughulikia hicho ulichoibiwa ???
Busara inasema unatakiwa kufanya uchunguzi wa kina ili umfahamu mwizi wako na sio kujari tu hisia zako ambazo zinaweza zikawa zimechochewa na huyohuyo aliyekuibia ili kukuondoa katika mstari sahihi wa wewe kumtambua yeye kuwa ndiye aliyekuibia.
 
Hivi, katiba iliyompa Sultani nafasi ya kuwa mkuu wa nchi baada ya Waingereza kuondoka ilipigiwa kura ya maoni na Wazanzibari? au iliandaliwa na nani?

Bwana Yesu anasema, Mathew 7

1. Do not judge, or you too will be judged. [SUP]2 [/SUP]For in the same way you judge others, you will be judged, and with the measure you use, it will be measured to you

mwanakijiji unajifanya hujui historia au ndio njia yako ya kufitinisha hiyo??? Sultani hakuwa mkuu wa nchi , Mkuu wa nchi ni PM .

Katiba hiyo ilikubaliwa na wabunge wote wakiwemo hao unaowaona wewe waafrika. Na Hao unaowaona wewe waafrika walikuwa na uwezo wa kupeleka pendekezo lao bungeni kuomba Ufalme uondoshwe bila kumwaga damu lakini sisi watanganyika tukawachafulia kila kitu kwa roho zetu mbaya na udini
 
Busara inasema unatakiwa kufanya uchunguzi wa kina ili umfahamu mwizi wako na sio kujari tu hisia zako ambazo zinaweza zikawa zimechochewa na huyohuyo aliyekuibia ili kukuondoa katika mstari sahihi wa wewe kumtambua yeye kuwa ndiye aliyekuibia.

na ndio maana hukuanza kuangalia historia ya babu yako ulikishughulikia kile kinachokupa taabu
 
Bwana Yesu anasema, Mathew 7

1. Do not judge, or you too will be judged. [SUP]2 [/SUP]For in the same way you judge others, you will be judged, and with the measure you use, it will be measured to you

mwanakijiji unajifanya hujui historia au ndio njia yako ya kufitinisha hiyo??? Sultani hakuwa mkuu wa nchi , Mkuu wa nchi ni PM .

Katiba hiyo ilikubaliwa na wabunge wote wakiwemo hao unaowaona wewe waafrika. Na Hao unaowaona wewe waafrika walikuwa na uwezo wa kupeleka pendekezo lao bungeni kuomba Ufalme uondoshwe bila kumwaga damu lakini sisi watanganyika tukawachafulia kila kitu kwa roho zetu mbaya na udini

Katika mafataani wanaotumia mitandao hii kijamii Tanzania huyo ni Sultani wao.
 
na ndio maana hukuanza kuangalia historia ya babu yako ulikishughulikia kile kinachokupa taabu
Soma tena bandiko langu! bila historia utajuaje leo imetokea wapi?

Busara inasema unatakiwa kufanya uchunguzi wa kina ili umfahamu mwizi wako na sio kujari tu hisia zako ambazo zinaweza zikawa zimechochewa na huyohuyo aliyekuibia ili kukuondoa katika mstari sahihi wa wewe kumtambua yeye kuwa ndiye aliyekuibia.[/QUOTE
 
Soma tena bandiko langu! bila historia utajuaje leo imetokea wapi?

historia gani wakati kwenye macho yako unaona huyo anayejifanya ni muafrika na mpinga utumwa wa kiarabu huku anahubiri muungano na umoja na kukutaka uijue historia yako amekuwa ni mamba anakula huku machozi yakimtoka

Tuwe wakweli watanganyika wenzangu nchi hii haiwezi kwenda si bara wala si zanzibar kwa kuendelea na muungano

Tunahitaji kuuvunja huu muungano tulionao kwanza, ili tuisafishe mafia ya mafisadi waliojificha chini ya mgongo wa muungano feki

HIZO HISTORIA KILA SIKU TUNASOMESHWA KILA MMOJA NA YAKE HATA ILE YA KINJEKETILE KUNA AINA TOFAUTI , ZOTE NI MBINU ZA WAJANJA TU HIZO
 
historia gani wakati kwenye macho yako unaona huyo anayejifanya ni muafrika na mpinga utumwa wa kiarabu huku anahubiri muungano na umoja na kukutaka uijue historia yako amekuwa ni mamba anakula huku machozi yakimtoka

Tuwe wakweli watanganyika wenzangu nchi hii haiwezi kwenda si bara wala si zanzibar kwa kuendelea na muungano

Tunahitaji kuuvunja huu muungano tuliona kwanza ili tuisafishe mafia ya mafisadi waliojificha chini ya mgongo wa muungano feki

HIZO HISTORIA KILA SIKU TUNASOMESHWA KILA MMOJA NA YAKE HATA ILE YA KINJEKETILE KUNA AINA TOFAUTI , ZOTE NI MBINU ZA WAJANJA TU HIZO
Usiwe mtumwa wa hisia na chuki, tulia na chambua mambo "with sober mind". Raha ya taaluma ni pale mtaalam anapotoka nje ya hisia na kuliangalia jambo "objectively".
 
Mkuu Mwanakijiji heshima mbele.

Sasa wote sisi tunafahamu kwamba Zanzibar kilikuwa ni kisiwa chenye wakazi ambao ni waafrika na walikuwepo hapo kwa miaka mingi tu.

Kwenye kisiwa hiki wamepita Wareno ambao baadae walishindwa na waarabu wa kutoka Oman ambao ndio walianzisha mifumo ya biashara ya utumwa na mazao kama karafuu.

Kama kawaida ya watu hawa wana pesa kwahio walijikita kwenye kisiwa hiki na kushamiri kwa biashara ya waafrika watumwa kutoka bara ndiko kulikopelekea Uingereza kutamka bayana kwamba biashara hiyo basi na waarabu hawa waache shughuli hiyo na wafanye shughuli zingine tu za biashara ambapo wakahodhi biashara ya karafuu.

Katika hali ya kupigania himaya kati ya waarabu, Ujerumani na Uingereza na hata kupelekea kuwepo kwa vita iitwayo Anglo Zanzibar War.

Uingereza kama kawaida ya kushikilia watu wenye faida au "interest" nao wakasahau kabisa kwamba sehemu hiyo ilikuwa na waafrika hapo mwanzo na wakaimarisha uhusiano wao na Sultani na kuifanya Zanzibar kama neo lililo chini ya uangalizi "protectorate" na sio koloni.

Lakini uamuzi wa Uingereza kumuachia Sultani Jamshid bin Abdullah awe ndie mtawala wa kisiwa cha Zanzibar na Pemba ni uamuzi ambao ulikuwa ni wa hatari kwa maana kwamba ni wao waingereza ndio walompa hifadhi ya kisiasa nchini humo hadi leo hii.

Ni uamuzi hatari kwa sababu ulikuwa ni uamuzi wa dharau kwa waafrika ambao eneo lao liliitwa Zangibar au Pwani ya Weusi.

Kwahio Zanzibar haijawahi kuwa koloni iwe kwa Wareno, Waarabu, Wajerumani wala Uingereza ila ni sehemu ambayo waafrika wachache walikuwa wakiishi wakiwa wenyeji ila wasio na shughuli zozote ambazo zingeonekana ni shughuli rasmi za biashara.
 
Back
Top Bottom