Je Zanzibar imewahi kuwa Koloni la Waarabu au la Watanganyika?

Wacha kutawalika kimawazo eti
mwafrika ,sisi wafrika, Hivi ni nyinyi WaTanzania tu au tuseme
Watanganyika tu mnaoumwa nahuu mnaoiita uafrika ,mbona sisikii Kenya
wala Uganda wakijilabu kwa hilo ,wandugu mliolala kimawazo ondokaneni na
donda hilo la kutumia sisi waafrika,hilo limeshapitwa na wakati.

Nchi nyingi siku hizi zinajilabu kwa uinchi na sio ubara au
ucontinental .Ukisikia mtu au watu wanahusisha kwa kusema sisi waafrika
akiwa ndani ya nchi yake basi mjue huyo mtu hana maana hata chembe, Na
wengine masikini za Munngu wanajua waafrika ni watu weusi peke yao ,hawa
ni malimbukeni.

Juzi nikitazama ITV,kipindi cha watoto wa shule jeshini mbagala ,kuna
wadada wakigawa zawadi(American Garden) mmoja alikuwa mweusi na mwengine
mweupe ,mtangazaji akisema kwa kuwauliza watoto waliobahatika kuchukua
zawadi
Nani anataka kwenda kuchukua zawadi kwa dada mweupe na nani anaetaka
kwenda kuchukua zawadi kwa dada mweusi ,nilichokiona hapo ni
udhalilishaji kwani hakuna hata mwanafunzi mmjoa aliekwenda kwa dada
mweusi wanafunzi wote waliekea kwa dada mweupe ilhali si muarabu wala
muhindi au mzungu ,basi amejaaliwa kuwa mweupe kama wale kabila la
wairaqi wa arusha. Mwisho mtangazaji alishtuka na kuacha kutumia mweusi
na mweupe.

@ Mzizi wa Mbuyunapenda uelewe kuwa hakuna tamaduni za kiafrika ,maana
kama zipo na zinafuatwa basi tembea uchi kwani hizo nazo ni tamaduni za
kiafrika ,ila hata Austaralia wapo waendao uchi ,burma ,red indians
,nionavyo dunia hapo mwanzo haikuwa na mipaka hivyo tamaduni zilienea na
kuzagaa kila kona ,si vibaya WaZanzibar wakafuata tamaduni za Kiarabu.

Maana kuna mchaga wa mwanzo kuimba Taarabu (Captain Temba) kuna mkuria
wa Mwanzo kuimba taarabu (Asha Mashausi) Je hii nayo ni aibu ??? Maana
Taarabu kwao ni Zanzibar au tuseme uarabuni. Je Masri (Kiini cha
Taarab) na nchi nyingi za Afrika kaskazini zinazungumza kiarabu au
tuseme ni waarabu ,Je wao si waafrika ?

Linapokuja suala la watu kujifanya waarabu lazima tukumbushane uafrika wetu.

Hao weusi wa amerika huwa wanajinasibu kwa uamerika wao si kwa uafrika wao! Sasa vije wewe mzanzibari mwafrika tena mmakonde ujinasibu kwa uarabu? Aibu!
 
Usiwe mtumwa wa hisia na chuki, tulia na chambua mambo "with sober mind". Raha ya taalam ni pale mtaalam anapotoka nje ya hisia na kuliangalia jambo "objectively".

kitu gani nimeandika kimo katika hisia na chuki au ni uongo nilivyoandika???

naona kinyume chake sisi watanganyika tumejazwa hizo propaganda za chuki na uongo na wengi tunakuwa wavivu kuusikiliza ukweli
 
Linapokuja suala la watu kujifanya waarabu lazima tukumbushane uafrika wetu.

Hao weusi wa amerika huwa wanajinasibu kwa uamerika wao si kwa uafrika wao! Sasa vije wewe mzanzibari mwafrika tena mmakonde ujinasibu kwa uarabu? Aibu!

si aibu ni hiari ya mtu , pilipili usioila yakuwashia nini???

MIND YOUR BUSINESS ,

sisi watanganyika tuamke tumind business zetu nchi inamalizwa na mafisadi kwa visingizio hivi uarabu , uafrika , umoja , muungano

lugha nzuri kumbe ni machozi ya mamba hayo
 
kitu gani nimeandika kimo katika hisia na chuki au ni uongo nilivyoandika???

naona kinyume chake sisi watanganyika tumejazwa hizo propaganda za chuki na uongo na wengi tunakuwa wavivu kuusikiliza ukweli
Sasa hizo ndio hisia na chuki na sio uchambuzi wa kisomi! Ama wewe huzioni?
 
Sasa hizo ndio hisia na chuki na sio uchambuzi wa kisomi! Ama wewe huzioni?

Na ndio nikaandika maana kila wakati utasikia historia za watumwa , waarabu , waafrika na utazikia hizi nyimbo kutoka kwa wanaoongoza system ,na baadhi ya viongozi wa makanisa, kumbe ndio turufu zao za kuendeleza ufisadi nchini
 
mr. dominick, let me tell you one important thing, you will never never learn history unless you abide to objectivity. Take and analyse facts and don't dwell on opinions.
 
WAnasema Zanzibar ni koloni la TAnganyika; wanatuita watu wa bara kuwa ni "wakoloni"; wanasema bila hata kufikiria kuwa ati Muungano hauna uhalali kwa vile hakukuwa na kura ya maoni; kwamba ati "watu waulizwe" kwanza ili wajue wanataka nini. Hawa hawa hawaelezikama Sultani alipigiwa kura na Wazanzibari kuwa SUltani wao? Hawa wanaamini Sultani alikuwa na uhalali wa kutawala Zanzibar hata kama Sultani huyo hakupigiwa kura, wala wananchi wake kuulizwa kama wanataka aendelee kuwatawala.

Hivi, kabla ya uhuru wa 1963 Wazanzibar walipiga kura ya maoni kuhusu kuendelea kwa Sultani kama "constitutional monarchy" au nani aliamua hili?
Mzee Mwanakijiji

Ukoloni maana yake nini?
Kwa mtazamo wa haraka haraka mtu hawezi kusema kuwa Tanganyika ni mkoloni lakini akiondoa ushabiki na jazba ataona kuwa Muundo wa Muungano umejenga utaratibu wa kuwa na nguvu za mkoloni.

Muungano ambao kwa kadiri siku zilivyokwenda mbele tokea kuanzishwa kwake ni kunaongeza mambo ya muungano. Hii ina maana kuwa madaraka ya serikali ya Zanzibar yanapungua/yanapunguzwa na mwisho wake Serikali ya Zanzibar itabakia kama serikali ya mkoa au serikali ya mtaa.

Pale vilipounganishwa TANU na ASP na baadae Chama kushika hatamu ndio kiini cha ukoloni wenyewe. Ikawa maamuzi yote hata yale yanayoihusu Zanzibar yanaamuliwa Chimwaga(Dodoma) au Dar.

Taasisi za kifedha za muungano zimekuwa hazizingatii athari za kiuchumi kwa Zanzibar zinapopanga ,sera za kifedha,mikakati na mipango yake ya kuboresha uchumi wa Tanzania(hapa isomeke Tanganyika) hili limelalamikiwa sana na Wenzetu Wazanzibari. Hapa niseme kuwa ndio sababu sasa Naibu Gavana wa BOT anakuwa Mzanzibari ili asaidie katika kuweka sawa mizania.

Hata sheria za uanzilishi wa vyama ni aina ya ukoloni, Zinalazimisha kufanya siasa kuwa ni jambo la Muungano. Kwa tafsiri yangu, hii ilikuwa janja ya CCM, iliamini hakitatokea chama chengine chenye nguvu katika pande mbili za Muungano na hivyo ndivyo ilivyo.CCM ambao ndio wamekuwa watawala tokea 1977 wamewaburuza sana wazanzibari, naamini hisia za" mkoloni mweusi" zina asili yake katika hili.

Tokea siasa za vyama vingi ziliporudia Tanzania, CCM chama dola na serikali zake zimetumia vyombo vya dola, usalama wa taifa, polisi, jeshi kuhakikisha kinabaki madarakani. Kwa upande wa Zanzibar ni kuwa kila unapofanyika uchaguzi, Taasisi hizo hutumika "kuyalinda mapinduzi", kuwapiga na kuwanajisi, kuwabambikizia kesi watu, kuwapiga risasi, kuwatia vilema na kuwaua. Wanajeshi wa ziada hupelekwa Zanzibar kusaidia uchakachuaji wa matokeo na kuwadhibiti wanaodai haki itendeke. Vyombo hivi vya dola viko chini ya nani?

Kuna sehemu umetoa wito, Mwanakijiji, polisi na jeshi la Tanganyika(Tanzania) lisitumike kulinda Mapinduzi ya zanzibar.
It is for this reason, sisi watu wa bara tumechoka kulinda mapinduzi ambayo Wazanzibari wenyewe hawataki kuyalinda; hatutaki Muungano na vyombo vya Muungano viendelee kulinda mapinduzi wakati serikali ya "Mapinduzi" ya Zanzibar ikifikiria na kutoa hata baraka za kubadili jina lake! Hatutaki polisi na JWTZ la Muungano lilinde mapinduzi ambayo halikuyafanya! Wazanzibar walinde mapinduzi yao nje ya Muungano!!!

Let Zanzibar Go!!!
Mkoloni ndiye anayelinda koloni lake !, au kwa nini kama Wazanzibari wanataka kuleta mabadiliko kwao tuwazuie kufanya hivyo?

Pia kuna kauli zitolewazo kuwa Zanzibar nje ya kivuli cha Tanganyika itakuwa nini?
Kauli hizi haziashirii ukoloni?

Kama tutasema kuwa Tanganyika sio mkoloni wa Zanzibar, basi inapasa kukubali kuwa kuna mambo yametendeka na yanayotendeka hadi sasa ambayo yanaashiria kuwa tunajifanya "wakoloni" mbele ya macho ya Wazanzibari. Tunawaburuza!

Link tudaitanganyikayetu
 
mr. dominick, let me tell you one important thing, you will never never learn history unless you abide to objectivity. Take and analyse facts and don't dwell on opinions.

Facts ndio unaziona maana huyo anayekuambia historia ndiye mamba wenyewe , utaamini historia na nyimbo zake???

Ondoa uchafu kwanza weka mazingira mazuri ndio uanze kutafuta historia ya kweli

KAMA UNAZIKUBALI HADISI ZA MATAPELI NA MAFISADI HIYO NI HIARI YAKO
 
Facts ndio unaziona maana huyo anayekuambia historia ndiye mamba wenyewe , utaiamni historia na nyimbo zake???

Ondoa uchafu kwanza weka mazingira mazuri ndio uanze kutafuta historia ya kweli
Kwani huyo mamba akikwambia maumbile yake haya ruhusu kuishi kwenye maji ya chumvi ndio maana haishi baharini bali kwenye mito na maziwa atakuwa anadanganya?
 
Mkuu Mwanakijiji heshima mbele.

Sasa wote sisi tunafahamu kwamba Zanzibar kilikuwa ni kisiwa chenye wakazi ambao ni waafrika na walikuwepo hapo kwa miaka mingi tu.

Kwenye kisiwa hiki wamepita Wareno ambao baadae walishindwa na waarabu wa kutoka Oman ambao ndio walianzisha mifumo ya biashara ya utumwa na mazao kama karafuu.

Kama kawaida ya watu hawa wana pesa kwahio walijikita kwenye kisiwa hiki na kushamiri kwa biashara ya waafrika watumwa kutoka bara ndiko kulikopelekea Uingereza kutamka bayana kwamba biashara hiyo basi na waarabu hawa waache shughuli hiyo na wafanye shughuli zingine tu za biashara ambapo wakahodhi biashara ya karafuu.

Katika hali ya kupigania himaya kati ya waarabu, Ujerumani na Uingereza na hata kupelekea kuwepo kwa vita iitwayo Anglo Zanzibar War.

Uingereza kama kawaida ya kushikilia watu wenye faida au "interest" nao wakasahau kabisa kwamba sehemu hiyo ilikuwa na waafrika hapo mwanzo na wakaimarisha uhusiano wao na Sultani na kuifanya Zanzibar kama neo lililo chini ya uangalizi "protectorate" na sio koloni.

Lakini uamuzi wa Uingereza kumuachia Sultani Jamshid bin Abdullah awe ndie mtawala wa kisiwa cha Zanzibar na Pemba ni uamuzi ambao ulikuwa ni wa hatari kwa maana kwamba ni wao waingereza ndio walompa hifadhi ya kisiasa nchini humo hadi leo hii.

Ni uamuzi hatari kwa sababu ulikuwa ni uamuzi wa dharau kwa waafrika ambao eneo lao liliitwa Zangibar au Pwani ya Weusi.

Kwahio Zanzibar haijawahi kuwa koloni iwe kwa Wareno, Waarabu, Wajerumani wala Uingereza ila ni sehemu ambayo waafrika wachache walikuwa wakiishi wakiwa wenyeji ila wasio na shughuli zozote ambazo zingeonekana ni shughuli rasmi za biashara.

Hizi ndio zile historia wanazotoa mafisadi na matapeli , unaweza kuita HIS STORY , bila hizi hadisi, ufisadi inakuwa ni vigumu kuufichuwa na mamba ataendelea maisha kututafuna
 
Kwani huyo mamba akikwambia maumbile yake haya ruhusu kuishi kwenye maji ya chumvi ndio maana haishi baharini bali kwenye mito na maziwa atakuwa anadanganya?

Mamba huyu katika mbinu zake za kukutafuna anaweza hata kukwambia maumbile yake yanamruhusu kuishi maji ya chumvi
 
Linapokuja suala la watu kujifanya waarabu lazima tukumbushane uafrika wetu.

Hao weusi wa amerika huwa wanajinasibu kwa uamerika wao si kwa uafrika wao! Sasa vije wewe mzanzibari mwafrika tena mmakonde ujinasibu kwa uarabu? Aibu!

Kwa Uamerica wao ,natumai nasi tungethamini Utanzania wetu ,au Utanganyika wetu au Uzanzibari wetu na sio Uafrika ,sijui unanielewa ?

Hivi nikuhulize suali ,Wamisri ni Waafrika au waarabu ? Halafu nimekuuliza huo Uafrika wa kujinasibu ni kitu gani au ni upi ?
 
Mamba huyu katika mbinu zake za kukutafuna anaweza hata kukwambia maumbile yake yanamruhusu kuishi maji ya chumvi
Sasa naona tunaenda pamoja, umeweza kutofautisha kati ya "FACTS" na "OPINION". kwa hiyo wewe kama msomi utajua kuwa mamba anadanganya na kwa nini anadaganganya! Basi tumia busara hiyo kuchambua taarifa unazopewa toka pande mbalimbali!
Usiku mwema!
 
Hiztoria inasema Zanzibar haijawahi kutawaliwa na ndio maana Tanganyika inajifanya ndio mtawala ,na ndio ukaona WaZanzibari wapo mstari wa mbele kudai uhulu wao ,wawachwe wapumue kabla hawajawapumulia !
 
Hizi ndio zile historia wanazotoa mafisadi na matapeli , unaweza kuita HIS STORY , bila hizi hadisi, ufisadi inakuwa ni vigumu kuufichuwa na mamba ataendelea maisha kututafuna

Historia ipi wewe unaifahamu?

Tanzania haina historia inayoeleweka ukizingatia tumo kwenye ukoloni mamboleo wala haijawekwa vizuri ili wananchi wenye upeo finyu kama wewe uweze kuelewa.

Nenda kasome historia vizuri na ukiishaisoma uwaze na uchambue pumba na mchele halafu ujiulize ni kwanini Waingereza waliamua kumwachia Zanzibar Sultan Jamshid.

Tatizo la mwafrika ni kutoweza kufikiri na kutafuta suluhisho kwa faida ya wengi na hili sasa naliona kwa wewe mwafrika mwenzangu ambae siku zote unangoja HIS STORY.

Nashukuru Mungu nimetembea na kuona tofauti kati ya mabwanyenye, watwana, ukoloni mamboleo na ubepari..

Tusiende nje ya topic tujadili je Zanzibar imewahi kuwa koloni la waarabu au watanganyika?
 
unaleta mambo ya historia aliyokuandikia nyerere ?? sikulaumu kwani ndiye baba yenu

wewe umetembea na kupita njia , mimi nimeishi na hao watu

kwani mwarabu ni nani ??? Mtanganyika ni nani??
 
unaleta mambo ya historia aliyokuandikia nyerere ?? sikulaumu kwani ndiye baba yenu

wewe umetembea na kupita njia , mimi nimeishi na hao watu

kwani mwarabu ni nani ??? Mtanganyika ni nani??

Mkuu mimi wala sijasoma historia ambayo imeandikwa na Nyerere wala maswahiba wake.

Nyerere alikuwa na wakti wake na sasa ni wakti mwingine, hivyo huna budi kuchambua historia yake ili upate pumba zipi na mchele upi.

Ntaamini vipi historia yake kwamba ulichanganywa udongo Zanzibar na Tanganyika na ikatoka Jamhuri ya Muungano?

Anyway, tuachane na ubishani uso na maana, sasa wewe mawazo yako ni yapi Zanzibar iliwahi kuwa koloni la Waarabu au Watanganyika?
 
kwa hio Wenzetu wa Zanzibar wanahitaji nini zaidi, wanakosa nini hasa? kama mapunduzi waliyafanya, kama ardhi wanayo, rais yupo, katiba, bendera, etc, nitaje kwa uchache
Hata yanga wanayo bendera katiba rais ! Wanahitaji kupumua wajiamulie mambo Yao bila ya kuingilwa na mtu
Suali: kwani south Sudan walikosa nini kutoka Sudan kudu
 
Mkuu mimi wala sijasoma historia ambayo imeandikwa na Nyerere wala maswahiba wake.

Nyerere alikuwa na wakti wake na sasa ni wakti mwingine, hivyo huna budi kuchambua historia yake ili upate pumba zipi na mchele upi.

Ntaamini vipi historia yake kwamba ulichanganywa udongo Zanzibar na Tanganyika na ikatoka Jamhuri ya Muungano?

Anyway, tuachane na ubishani uso na maana, sasa wewe mawazo yako ni yapi Zanzibar iliwahi kuwa koloni la Waarabu au Watanganyika?

ndio kule nikakuwekea masuali mawili ambayo lazima tuyatofautishe

nakuwekea tena

kwani mwarabu ni nani ??? Mtanganyika ni nani??

kukuweka sawa nauliza

JEE Kuna nchi inaitwa mwarabu??
 
Back
Top Bottom