CCM Zanzibar kujadili kauli tata za Balozi Karume

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1685602454317.png

Vuguvugu la mpasuko limeendelea kufukuta visiwani Zanzibar baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuahidi kufanya uchambuzi wa kauli mwanasiasa na mwanadiplomasia, Balozi Ali Abeid Karume kuhusu viongozi wa chama hicho kukosa uhalali wa wananchi kuongoza Zanzibar.

Ali Karume aliyegombea mara kadhaa nafasi ya kuongoza Ikulu ya Zanzibar bila mafanikio ndani ya chama, ametumikia nafasi mbalimbali ndani ya chama na serikalini tangu akiwa na miaka 28 hadi Serikali iliyomaliza muda wake mwaka 2020 akiwa kwenye baraza la mawaziri.

Leo Jumatano, Mei 31, 2023, Katibu Kamati Maalumu NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Khamis Mbeto akizungumza na Mwananchi Digital amesema chama kimesikia kauli hizo hivyo suala lake litashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu za chama.

“CCM ina taratibu zake, zipo kamati za maadili wenyewe ndio wanashughulikia masula hayo kama wataona ipo haja kumuita watamuita kuzungumza naye kisha baada ya hapo tutatoa taarifa kitakachofuata,” amesema Mbeto.

Mbeto amemtaka Balozi Ali ambaye ni mtoto wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Karume kutumia taratibu za chama kwa ajili ya kuwasilisha jambo lolote kama mwanachama mzoefu na mwenye heshima.

“Yeye amekuwa waziri katika serikali ya awamu ya saba, kama ipo hivyo anavyosema mbona hakujiondoa au kukataa akisema haridhishwi na upatikanaji wake? Ifike mahala asijivunjie heshima zake mana ni mtu anayeheshimika kwa nafasi zake alizopitia,” amesema Mbeto.

Siku mbili zilizopita, Balozi Karume aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano, Uchukuzi na Usafirishaji katika awamu ya saba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) alinukuliwa kauli hizo zilizosambaa mitandaoni wakati akijibu swali katika mahojiano yaliyofanyika kwa njia ya mtandao huko Zanzibar.

Katika maoni yake Balozi Karume alitakiwa kufafanua sababu za kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUKI) visiwani huko uliotokana na makubaliano ya mgawanyo wa madaraka baada ya uchaguzi.

“GNU ipo kwa sababu viongozi wa CCM walikuja kuona kwamba kila chaguzi za Zanzibar CCM inashindwa uchaguzi, sasa inashindwa kwa sababu gani, hilo tutazungumza siku nyingine. Lakini naamini walikuwa wanashindwa kwa kuweka wagombea wasio na mvuto,” alisema Balozi Karume akifafanua:

“Wakienda kwenye uchaguzi wa kweli na haki wanashindwa kura hawa wadogo zangu na matokeo tumeyaona mfano mwaka 2015 hebu tuambizane ukweli kama kweli tulikubaliana uchaguzi uwe haki ilikuwaje tutumie mabavu, nguvu?“

Kutokana na kauli hiyo, juzi rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein Mwinyi, alijibu hoja hiyo kwakupuuza: “Kama nilivyosema, upuuzi haujibiwi, unapuuzwa. Hili siwezi kulijibu,”alisema Dk Mwinyi alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo. “Nani asiyejua mfumo wa uchaguzi wa nchi yetu?.

“Maana watu wengine wanahoji kuanzia huko kwenye kura za maoni, ahaa kapewa tu na mwenyekiti. Jamani, kuna mwaka uliowahi kuwa wazi katika uchaguzi kama ilivyokuwa mwaka 2020? Kura zimepigwa hadharani, zimehesabiwa hadharani imewahi kutokea? Katika hili naomba nimpuuze tu.”

MWANANCHI
 
Kwa maoni yangu apuuzwe kama alivyosema rais Hussein Mwinyi

Kwasababu kumjadili ni kukuza tatizo na kumpa credit,mengi yataibuka ,

Kama vipi washughulike nae kimya kimyakimya,Ndio busara
 
Bila CCM kusimama kidete kuulezea mchakato wa upigaji kura na uwazi wake hawa wapotoshaji wataunda umoja wao siku moja kupotosha ukweli na uongo wao ukaonekana ndio ukweli
 
Kwa maoni yangu apuuzwe kama alivyosema rais Hussein Mwinyi

Kwasababu kumjadili ni kukuza tatizo na kumpa credit,mengi yataibuka ,

Kama vipi washughulike nae kimya kimyakimya,Ndio busara
Baada ya SMZ kupora kipande cha ardhi kutoka Tanganyika, Ally Karume asipuuzwe
 
Kwa maoni yangu apuuzwe kama alivyosema rais Hussein Mwinyi

Kwasababu kumjadili ni kukuza tatizo na kumpa credit,mengi yataibuka ,

Kama vipi washughulike nae kimya kimyakimya,Ndio busara
Hiyo 2020 ndo Kura zilipigwa siku moja kabla na Watumishi waliopiga Kura wakawa zaidi ya Laki 6?
 
Acha apasue , ukweli ndio huo aliousema Ali Karume,
Lakini CCM imezowea kuficha ukweli.
2015 Maalim Seif Alishinda na Chama chake CUF na ndio Jecha akafuta Matokeo ya Uchaguzi pasi na kuwepo sababu za kufanya hivyo.
Uchaguzi ule ulikuwa wa Huru zaidi na Haki , hakukuwa na Misuguano popote.
Vyama vyote vilisaini matokeo na kukubali yantangazwe.

Ali Karume yuko sawa.

Husein kachukua nchi Kwa mauwaji na Mabavu, Kura siku 2
Jeshi nchi nzima Kafew wiki nzima.
Wacha awape ukweli.
Najua Wanaweza kumfukuza au kumpiga kama Mzee Baraka Shamte
 
View attachment 2642164
Vuguvugu la mpasuko limeendelea kufukuta visiwani Zanzibar baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuahidi kufanya uchambuzi wa kauli mwanasiasa na mwanadiplomasia, Balozi Ali Abeid Karume kuhusu viongozi wa chama hicho kukosa uhalali wa wananchi kuongoza Zanzibar.

Ali Karume aliyegombea mara kadhaa nafasi ya kuongoza Ikulu ya Zanzibar bila mafanikio ndani ya chama, ametumikia nafasi mbalimbali ndani ya chama na serikalini tangu akiwa na miaka 28 hadi Serikali iliyomaliza muda wake mwaka 2020 akiwa kwenye baraza la mawaziri.

Leo Jumatano, Mei 31, 2023, Katibu Kamati Maalumu NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Khamis Mbeto akizungumza na Mwananchi Digital amesema chama kimesikia kauli hizo hivyo suala lake litashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu za chama.

“CCM ina taratibu zake, zipo kamati za maadili wenyewe ndio wanashughulikia masula hayo kama wataona ipo haja kumuita watamuita kuzungumza naye kisha baada ya hapo tutatoa taarifa kitakachofuata,” amesema Mbeto.

Mbeto amemtaka Balozi Ali ambaye ni mtoto wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Karume kutumia taratibu za chama kwa ajili ya kuwasilisha jambo lolote kama mwanachama mzoefu na mwenye heshima.

“Yeye amekuwa waziri katika serikali ya awamu ya saba, kama ipo hivyo anavyosema mbona hakujiondoa au kukataa akisema haridhishwi na upatikanaji wake? Ifike mahala asijivunjie heshima zake mana ni mtu anayeheshimika kwa nafasi zake alizopitia,” amesema Mbeto.

Siku mbili zilizopita, Balozi Karume aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano, Uchukuzi na Usafirishaji katika awamu ya saba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) alinukuliwa kauli hizo zilizosambaa mitandaoni wakati akijibu swali katika mahojiano yaliyofanyika kwa njia ya mtandao huko Zanzibar.

Katika maoni yake Balozi Karume alitakiwa kufafanua sababu za kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUKI) visiwani huko uliotokana na makubaliano ya mgawanyo wa madaraka baada ya uchaguzi.

“GNU ipo kwa sababu viongozi wa CCM walikuja kuona kwamba kila chaguzi za Zanzibar CCM inashindwa uchaguzi, sasa inashindwa kwa sababu gani, hilo tutazungumza siku nyingine. Lakini naamini walikuwa wanashindwa kwa kuweka wagombea wasio na mvuto,” alisema Balozi Karume akifafanua:

“Wakienda kwenye uchaguzi wa kweli na haki wanashindwa kura hawa wadogo zangu na matokeo tumeyaona mfano mwaka 2015 hebu tuambizane ukweli kama kweli tulikubaliana uchaguzi uwe haki ilikuwaje tutumie mabavu, nguvu?“

Kutokana na kauli hiyo, juzi rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein Mwinyi, alijibu hoja hiyo kwakupuuza: “Kama nilivyosema, upuuzi haujibiwi, unapuuzwa. Hili siwezi kulijibu,”alisema Dk Mwinyi alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo. “Nani asiyejua mfumo wa uchaguzi wa nchi yetu?.

“Maana watu wengine wanahoji kuanzia huko kwenye kura za maoni, ahaa kapewa tu na mwenyekiti. Jamani, kuna mwaka uliowahi kuwa wazi katika uchaguzi kama ilivyokuwa mwaka 2020? Kura zimepigwa hadharani, zimehesabiwa hadharani imewahi kutokea? Katika hili naomba nimpuuze tu.”

MWANANCHI
Kama anao wadhifa kwenye ccm itakuwa sahihi kumuita kwenye kikao na kumhoji hukusu kauli zake. Lakini kama ni mwanachama tu siyo sawa kumuita; anayo haki ya kuwa na maoni binafsi. Isitoshe, sababu ya nguvu nyingi za vyombo vya ulinzi kutumika Zanzibar miaka yote zinazopelekea raia kuumizwa na wengine kuuawa ni ushahidi kuwa ushindi wa ccm ni wa kulazimisha.
 
Kwa maoni yangu apuuzwe kama alivyosema rais Hussein Mwinyi

Kwasababu kumjadili ni kukuza tatizo na kumpa credit,mengi yataibuka ,

Kama vipi washughulike nae kimya kimyakimya,Ndio busara
Ameongea ukweli na kwenu ccm ukweli hautakiwi ndio maana mnakimbilia kusema ashughulikiwe badala ya kufanyia kazi anachosema.
 
Back
Top Bottom