Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
WAnasema Zanzibar ni koloni la TAnganyika; wanatuita watu wa bara kuwa ni "wakoloni"; wanasema bila hata kufikiria kuwa ati Muungano hauna uhalali kwa vile hakukuwa na kura ya maoni; kwamba ati "watu waulizwe" kwanza ili wajue wanataka nini. Hawa hawa hawaelezikama Sultani alipigiwa kura na Wazanzibari kuwa SUltani wao? Hawa wanaamini Sultani alikuwa na uhalali wa kutawala Zanzibar hata kama Sultani huyo hakupigiwa kura, wala wananchi wake kuulizwa kama wanataka aendelee kuwatawala.
Hivi, kabla ya uhuru wa 1963 Wazanzibar walipiga kura ya maoni kuhusu kuendelea kwa Sultani kama "constitutional monarchy" au nani aliamua hili?
Hivi, kabla ya uhuru wa 1963 Wazanzibar walipiga kura ya maoni kuhusu kuendelea kwa Sultani kama "constitutional monarchy" au nani aliamua hili?