Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 56
Swali ni je, hali mbaya ya wananchi wa nchi za "kibepari" afrika ni dalili ya kushindwa kwa ubepari Afrika?
Kuna documentari moja inatayarishwa na waandishi wa habari wa kiafrika wanaofanya kazi kwenye mashirika makubwa ya habari ya uropa na amerika. Documentari hii ilisimama kwa muda baada ya mmoja wa wataarifu habari (reporter) maarufu kutoka nchi moja ya afrika mashariki kuacha/chishwa kazi katika mazingira yasiyo na kueleweka kabisa.
Katika documentary hii, kumeonyeshwa maisha ya wananchi wa nchi zilizoamua kuwa za kibepari afrika baada ya uhuru ikilinganishwa na zile zilizoamua kuwa za kijamaa (au kutofungamana na upande wowote). Niliguswa sana na clips toka kwa majirani zetu wa Kenya, Uganda, na Congo.
Ilionyeshwa kuwa, Kenya kulikuwa na watoto ombaomba (chokoraa) karibu milioni moja wanaoishi maisha ya kubahatisha. Ilionyeshwa pia kuwa Kuna watu zaidi ya milioni nne wanaoishi katika slums na hali mbaya ya kiafya na kimazingira. Uganda kulionyeshwa maelfu ya watoto wanaotembea kilomita nyingi kila siku kwenda kulala kwenye miji mikubwa kwa sababu hawana pa kulala. Kuna watoto zaidi ya milioni moja Congo wasiokuwa na hakika ya kula mlo mmoja wa siku. Habari imekuwa mbaya kwa Malawi ambayo baa la njaa la miaka michache iliyopita limeacha watu wengi taabuni.
Nchi za kijamaa nazo wameonyesha Ghana, Tanzania, Zambia (sijui ni vigezo gani wametumia) zimepitia matatizo haya haya na hakuna mwenye nafuu kidogo ingawa waandishi hawa wote wanakiri kuwa Slums za Kibera nk za kenya ndizo kubwa kabisa katika nchi yoyote Afrika (sijui bado vigezo). Hii documentary imeonyeshwa kwa wanachama wa chama cha waafrika hapa chuoni kwangu ili kupata mawazo yao kabla haijaanza kusambazwa.
Kilichonishangaza ni kuwa, wengi walioiona hawakupinga kuwa iko biased ila walianza kulaumu ubepari na ujamaa. Wote tunajua kuwa ujamaa wa russia uliporomoka na kushindwa wakati wanaojiita mabepari - marekani wakionekana kufanikiwa. Swali ni je, hali mbaya ya wananchi wa nchi za "kibepari" afrika ni dalili ya kushindwa kwa ubepari Afrika?
Uuuhuu, hii haijakaa sawa!
Mkuu MWK,
Heshima mbele, sina uhakika kama mifano ya nchi zilizotajwa kama mifano ya ubepari katika Afrika, zinatimiza matakwa rasmi ya kupewa jina hilo la ubepari. Kwa sababu binafsi ninaaamini kuwa kuna cnhi ambazo zinatimiza matakwa hayo kama Afrika Kusini, Botswana, na Namibia, ambako ubaperi unafanyika in fulll gear na hakuna matatzio kama yaliyopo kwenye nchi ulizozitaja au zilizotajwa kwenye hiyo documentary, ubepari bado kushindwa kuanzia Afrika wala Europe, isipokuwa pale tu ulipojaribishwa bila ya kufuata masharti yake in full.
Argentina, ulikuwa ni mfano mkubwa wa kujaribisha bila kufuata masharti yake in full, mpaka walipokubali kufuata masharti yake yote sasa wameanza kuwa na nafuu na kuona matunda yake. Ubepari siku zote unafuatana na demokrasia, na sidhani kuna any ya hizo nchi zilizotumika kama mfano wa kushindwa kwa demokrasia Afrika, zimashawahi ku-practice angalau hata 1/4 ya true demokrasia.
Ubepari bado haujshindwa, lakini sio siri kuwa American empire iko njiani kuelekea kwenye ku-decline, kwa sababu ya ubepari kukosa mpinzani kwa muda mrefu!
Mwanamke wa Kike:
Hapa itabidi nitafute glove tuanze ngumi. Kwanza inabidi tutofautishe vitu viwili. Ubepari muundo wa kiuchumi na serikali ina-support huo muundo.
Ubepari kama muundo wa uchumi una kanuni zake na moja kubwa kuruhusu ushindani wa uchumi ulio huru na kazi ya serikali ni kuakikisha kuwa hizo za ushindani zinafuatwa.
Uganda, Kenya na Zaire hazikuwa nchi za kibepari. Serikali hazikulinda kanuni za ushindani na walichofanya viongozi ni kujipendelea kama vile unavyoona mafisadi wetu wa sasa.
Bin Mariam,
Mojawapo ya mazingaombwe ya ubepari ni ile dhana kwamba unaruhusu ushindani wa uchumi ulio huru. Ubepari misingi yake ni samaki mkubwa kummeza mdogo. Hata Marekani kwenyewe kumekuwepo na mabavu ya big corporates ku"squeeze out" competitions.
Wewe binti wa Maryam,
Bado nasubiri kuona tofauti ya ubepari muundo wa kiuchumi na serikali ina-support huo muundo. Huna sababu ya kuvaa gloves maana hii mada sio confrotational. It rather should be educational, what say you!
Kuna tofauti kubwa kati Bin na Binti. Na kwa sisi wenye asili ya kihabeshi Maryam ni jina la Kiume, remember !!!.
Ingawa sijui sana unamaanisha nini hapa lakini ngoja niachane nayo maana si sehemu ya mada labda ueleze kidogo kuhusu tofauti ya maneno uliyotaka kuhusiana na ubepari!
Kila mara nimekuwa nasema kilichotuangusha waafrika kiuchumi na kijamii kwa asilimia 100 ni viongozi wetu. Hakuna cha siasa ya ujamaa wala ubepari. Ni RUSHWA tu, PERIOD. Hebu angalia mwaka mmoja tu tumegundua uwizi wa $130m (minimum) benki kuu. Je miaka 46 ya uhuru ni kiasi gani wameiba hawa viongozi wetu? Je fedha zote hizo zingeingia kwenye uchumi leo hii tungekuwa wapi?
Mbona nchi kama Korea, Malaysia, Singapore, nk. pamoja na ubepari wao miaka ya 60 tulikuwa tumezipita mbali sana kiuchumi? Ni nini kilitokea hadi tukakwama kama sio uwizi na kukosa kuwajibika kwa viongozi wetu?
Kwa kweli kama hawa jamaa (viongozi) wana aibu basi wangepaswa hata kujinyonga na sio kusimama mbele za watu na kutamba kwamba wametuletea maendeleo, umoja na mshikamano.
Sometimes nakubaliana na Freeman kwamba heri wakati wa mkoloni kuliko wakati wowote baada ya uhuru watanzania.
This is a good analysis. Thank you!
FMES:
Matatizo ya dunia ya nne kwa sasa tunahitaji kukaa na kureflect tunatoka wapi na tunakwenda wapi. Kama nilivyosema awali, tunaishi kwenye very hostile world ambayo its everybody for himself and GOD for us all. Ujamaa na ubepari mifumo yote naona haijatusaidia (au masharti yake yametushinda) especially waafrica, nadhani its high time tuwe INNOVATIVE kutafuta mfumo mwingine! Mimi na wewe hatujui lakini hakika tunaweza kutafuta mfumo ambao unaangalia tulikotoka na tunakotaka kwenda. Kwa sasa HATUJITAMBUI ndo maana JK akienda China ataongea ujmaa na ukomunist na Premier wa China akienda Capitol Hill kwa Bush atacheza mdundiko wa ubepari! Bila kuangalia consequences kwa wananchi wake. Kifupi we dont know what we want and worse even our Moses (JK) doesnt know! Yes he admitted that!!!
Hatuwezi kuulaumu Ubepari wala ujamaa wa kujiangalia na kujisuta ni sisi: mfano kama mmoja alivyosema, katika mwaka mmoja tumegundua 130$$M zilizoibwa na akina Balali, je kabla ya hapo waliiba ngapi? Idrisa alichukua ngapi, Mramba, Msuya, Mkapa, Sumaye and on and on....is it the fault of ubepari? I say no its our culture of corruption. na kama ulivyoandika, Ubepari masharti yake ni magumu hatuyawezi kwa hiyo tunalazimisha unworkable ideals.
In Africa from my personal views hakuna economic system ambayo imefanikiwa iwe South Africa, Nigeria or else where, because we were just coopted by our colleagues in the west (and east!) to implement things which we were/are not honest about and yet we are not prepared to say no to such policies. Whose fault is that??
Nakubaliana na; Sio kushindwa, bali upo kwenye mpito!Swali ni je, hali mbaya ya wananchi wa nchi za "kibepari" afrika ni dalili ya kushindwa kwa ubepari Afrika?