Ablessed
JF-Expert Member
- Mar 19, 2013
- 4,616
- 3,502
Habari zenu wana MMU ninaamini kabisa wote mko salama . Nina jambo nataka kushare nanyi najua halitakua geni sana kwenu wengi mmekumbana nalo kama si wote . Mmmmh ktk familia zetu nyingi huwa kuna mchanganyiko wa watotot na watu wazima . Je nyie mmewahi kumsikia huyu mtoto ambae huwa anatajwa na watoto karibu wote hasa wanapokua wamekosea ??? Ukikuta uharibifu wowote ndani ya nyumba ukiwauliza watoto basi watakutajia jina la huyo mtoto na ukijaribu kumtafuta kamwe hautampata na nimesema siku nikimpata huyo mtoto atanitambua kwa kweli . Kiukweli mtoto huyu anasumbua sana. Unajua Mtoto huyo anaitwa nani , anaitwa "SIJUI".
Nawatakia maandalizi mema ya kuianza week mpya na nawaombea wote Mungu awabariki na kuwatia nguvu ktk kulisukuma gurudumu la maendeleo. Muuone wepesi kila muendapo kutimiza majukumu yenu.
Be blessed.
Nawatakia maandalizi mema ya kuianza week mpya na nawaombea wote Mungu awabariki na kuwatia nguvu ktk kulisukuma gurudumu la maendeleo. Muuone wepesi kila muendapo kutimiza majukumu yenu.
Be blessed.
Likes Received (0)