Jacqueline si mtoto wa Prof Ndalichako, asihukumiwe bila hatia

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
201
1,534
Baada ya kusambaa kwa taarifa inayoonesha wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/17 kumejitokeza mjadala mkubwa juu ya jina la binti aliyejulikana kama Jacqueline Ndalichako, akidaiwa kuwa mtoto wa Waziri wa Elimu Prof.Joyce Ndalichako.

Mimi ni miongoni mwa watu waliohamaki baada ya kupata taarifa hiyo, na nikasema IKIWA NI KWELI JACQUELINE NI MTOTO WA PROF.NDALICHAKO basi inabidi Waziri huyo ajiuzulu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mtoto wa waziri hawezi kupata mkopo hata kama anakidhi vigezo vya kitaaluma. Mwongozo wa HESLB unamtaka mwanafunzi awe anatoka familia isiyojiweza kiuchumi, lakini mtoto wa Waziri hawezi kuwa kundi la wasiojiweza kiuchumi. Wapo watanzania wengi wenye uhitaji wa mikopo ya elimu ya juu kuliko watoto wa mawaziri.

#UKWELI_KUHUSU_TAARIFA_HIYO.

Baada ya kufuatilia nimegundua mambo yafuatayo:

1. Jacqueline si mtoto, ndugu wala hana unasaba wowote na Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi. Ni ufanano tu wa majina, baina ya watu hawa wawili lakini ni watu wasiofahamiana kabisa.

2. Profesa Ndalichako hana mtoto mwenye jina Jacqueline, wala hana ndugu mwenye mtoto mwenye jina hilo.

3. Watoto wa Profesa Ndalichako walishahitimu elimu ya juu na hakuna yeyote anayejiunga na elimu ya juu kwa sasa.

4. Jacqueline amehusishwa na Prof.Ndalichako kwa sababu ya ufanano wa majina, lakini si watu wenye kufanana nasaba.

5. Jacqueline hakusoma HGL kama ilivyoelezwa. Amesoma EGM na amechaguliwa kusoma Shahada ya Uchumi na Takwimu (B.A in Economics and Statistics).

6. Jacqueline anatoka familia yenye uchumi wa kawaida hivyo anakidhi vigezo vya kupewa mkopo. Amesoma St.Mary Gorreti katika mazingira ambayo si vzr kuyaeleza hapa. (Nimefuatilia taarifa za familia ya Jacqueline inayoishi Yombo Dovya lakini nisingependa kuziweka hapa).

SWALI: Je waliosema Ndalichako awajibike wamekosea?

JIBU: Hapana. Hoja ilikuwa "Kama kweli Jacqueline ni mtoto wake basi awajibike". Hii ina maana kuwa hakukuwa na sababu ya kuwajibika kama si mwanae.

SWALI: Walioibua hoja ya Jacqueline kuwa mtoto wa Ndalichako wamekosea?

JIBU: Ndio. Walioanzisha hoja hii wamekosea kwa kuwa kuna viashiria kwamba walikusudia kupotosha. Hoja hii imepata nguvu mitandaoni na kusababisha usumbufu ambao ungeweza kuepukika.

[HASHTAG]#MyTAKE[/HASHTAG]:
Kwanza niwape pole Jacqueline pamoja na Prof.Ndalichako kwa usumbufu ambao kila mmoja ameupata.

Pili niwatake wote wanaoendelea kusambaza taarifa kuwa Jacqueline na Prof.Ndalichako ni ndugu waache kufanya hivyo maana wanaweza kupotosha wengine.

Ufanano wa majina si kigezo cha kuhukumu wasio na hatia pasipo uchunguzi. Bahati mbaya Jacqueline ameingia kwenye mijadala ya mitandao bila hatia. Amekuwa victim wa social media kwa sababu za kisiasa, ambazo yeye hahusiki nazo kabisa. Pia nimpe pole Prof.Ndalichako kwa usumbufu alioupata.

Ukweli ni kwamba kufanana majina ni jambo la kawaida katika tasnia yoyote. Wapo wanafunzi wengi waliopo vyuoni au waliochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu wenye majina yanayofanana na viongozi wakubwa kisiasa lakini hawajahusishwa na viongozi hao.

Kuna mwanafunzi amechaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu Dodoma mwenye jina Gideon Wassira, lakini sijasikia akihusishwa na Mzee Stephen Wassira. Kijana Nobert Mbowe amehitimu Chuo kikuu Mlimani akisomea shahada ya Uhandisi wa madini (Mining Engineering) lakini hajawahi kuhusishwa na Mhe.Freeman Mbowe. Kuna mwanafunzi anaitwa Kennedy Yusuf Ndugai amechaguliwa shahada ya elimu maalum UDOM lakini hajahusishwa unasaba wake na Spika Job Ndugai.

Kwa hiyo nitoe wito watu waache kutumia habari inayomhusu Jacqueline kwa kumhusisha na Waziri Ndalichako maana ni watu wasio na uhusiano wowote kinasaba.

Najua wengi wamehamaki kusikia Jacqueline ni mtoto wa Waziri halafu kapewa mkopo huku watoto wa maskini wakikosa mikopo. Kumbe Jacqueline naye ni mtoto wa maskini pia, ila ameponzwa na ufanano wa majina na Waziri Ndalichako.

Nihitimishe mjadala huu kwa kutoa rai kwa "bloggers &social media emperors" kutokuendelea kujadili suala la Jacqueline na Waziri Ndalichako maana ni watu wasiofahamiana kabisa, achilia mbali kuhusiana kinasaba. Tumpe nafasi Jacqueline aweze kucocentrate ktk masomo yake, asiwe frustruted na mitandao. Let us end this discussion to save this innocent poor soul.!

Malisa GJ
 
Thanks kwa taarifa nzuri ya ufafanuzi.

Ila subiri tu reaction ya ufafanuzi wako maana humu JF kuna wadadisi we acha tu.

Kuna mwanafunzi anaitwa Agatha Ndalichako amemaliza St Marian 2012 A Level na amepata Div 2, O Level alipata Div 1 naye tutasema ni mtoto wa Prof Ndalichako!!?

Jamani majina tu haya,mbona wakina Mwinyi wapo wengi tu kwa hiyo watoto wote wenye majina hayo ni ndugu au watoto Rais Mwinyi

Aaaha jamani watanzania naona kuna mambo tumeanza kuyatafuta wenyewe hata sijui tunaelekea wapi

Just wait and see!!
 
Mwongozo wa HESLB unamtaka mwanafunzi awe anatoka familia isiyojiweza kiuchumi, ...
#UKWELI_KUHUSU_TAARIFA_HIYO.

Baada ya kufuatilia nimegundua mambo yafuatayo:

6. Jacqueline anatoka familia duni kiuchumi hivyo anakidhi vigezo vya kupewa mkopo.

Jackline amesoma St. Mary Goreti Secondary School, Moshi. (exam number: S 1187)

Tuthibitishie kuwa ametoka familia duni tafadhali.
 
Shida yote hii ni mikopo mikopo hivi mtu unazaa wa nini kama huwezi kumsomeshaa?

Watu wanaleta viumbe kwa starehe zao afu wanaishia kuvipatia shida tu, Serikali duniani zina kazi kwa kweli, haingii akilini mtu aanze la kwanza, form one hadi six mzazi hujajipanga na kujiandaa kumuwezesha mwanao kusoma.

Mungu wape maisha marefu wazazi wangu japo si katika hali ya kujikweza au elimu za ghari sana ila kwenye suala la Elimu walijipanga mapema.

Binafsi sioni hasara kuishi duniani bila ya mtoto ambaye ni wangu ili hali sijaandaa mazingira yatakayomharahishia maisha yake, Japo hatuwezi kuzuia mambo mengine yanayoweza kutokea kinyume na matarajio yetu,ni muhimu dhamira,jitihada na bidii za makusudi ziwepo ili kiumbe chako kisije kuwa tegemezi either kwa serikali au kwa mtu.

Nawaonea huruma sana wanafunzi waliofaulu na wanaoshindwa kumudu gharama za masomo hii haikuwa mipango wala si mapenzi yao ni failure ya wazazi wao, Serikali imekuwa kichaka cha kujifichia tu.
 
Mkuu wangu hongera kwa wazazi wako kujipanga kukupa elimu..

Ila kwa kifupi tu WE NI MBUNDA NA NAWASIKITIKIA SANA WAZAZI WAKO KUPOTEZA PESA ZAO KUMPA ELIMU MBUNDA KAMA WEWE..

shida yote hii ni mikopo mikopo hivi mtu unazaa wa nini kama huwezi kumsomeshaa??? Watu wanaleta viumbe kwa starehe zao afu wanaishia kuvipatia shida tu, Serikali duniani zina kazi kwa kweli, haingii akilini mtu aanze la kwanza, form one hadi six mzazi hujajipanga na kujiandaa kumuwezesha mwanao kusoma. Mungu wape maisha marefu wazazi wangu japo si katika hali ya kujikweza au elimu za ghari sana ila kwenye suala la Elimu walijipanga mapema. Binafsi sioni hasara kuishi duniani bila ya mtoto ambaye ni wangu ili hali sijaandaa mazingira yatakayomharahishia maisha yake, Japo hatuwezi kuzuia mambo mengine yanayoweza kutokea kinyume na matarajio yetu,ni muhimu dhamira,jitihada na bidii za makusudi ziwepo ili kiumbe chako kisije kuwa tegemezi either kwa serikali au kwa mtu. Nawaonea huruma sana wanafunzi waliofaulu na wanaoshindwa kumudu gharama za masomo hii haikuwa mipango wala si mapenzi yao ni failure ya wazazi wao, Serikali imekuwa kichaka cha kujifichia tu.
 
Ndo maana naipenda JF...ukija na talalila zako watu wanakugonga swali ambalo hata hukuhisi kuulizwa

Jiridhishe zaidi kwa kutembelea
St Mary Goreti Secondary School - Kilimanjaro, Tanzania

Cc GM
I never argue with weak minded people like you. Soma andiko vzr, nimesema nimefuatilia familia ya Jacqueline pale Yombo Dovya na nimegundua mengi ambayo wewe na "wapayukaji" wenzio hamuwezi kuyajua. Kuna story ndefu sana nyuma ya pazia kuhusu Jacqueline kusoma St.Mary Goreti. Fuatilia kwanza kabla hujatoa mapovu.
 
Mkuu mbona naona wewe ndo povu limeanza kukutoka..

If you think am weak minded...why bother argue with me then..

I never argue with weak minded people like you. Soma andiko vzr, nimesema nimefuatilia familia ya Joyce pale Yombo Dovya na nimegundua mengi ambayo wewe na "wapayukaji" wenzio hamuwezi kuyajua. Kuna story ndefu sana nyuma ya pazia kuhusu Jacqueline kusoma St.Mary Goreti. Fuatilia kwanza kabla hujatoa mapovu.

Sent from my HTC One E9PLUS dual sim using JamiiForums mobile app
 
Baada ya kusambaa kwa taarifa inayoonesha wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/17 kumejitokeza mjadala mkubwa juu ya jina la binti aliyejulikana kama Jacqueline Ndalichako, akidaiwa kuwa mtoto wa Waziri wa Elimu Prof.Joyce Ndalichako.

Mimi ni miongoni mwa watu waliohamaki baada ya kupata taarifa hiyo, na nikasema IKIWA NI KWELI JACQUELINE NI MTOTO WA PROF.NDALICHAKO basi inabidi Waziri huyo ajiuzulu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mtoto wa waziri hawezi kupata mkopo hata kama anakidhi vigezo vya kitaaluma. Mwongozo wa HESLB unamtaka mwanafunzi awe anatoka familia isiyojiweza kiuchumi, lakini mtoto wa Waziri hawezi kuwa kundi la wasiojiweza kiuchumi. Wapo watanzania wengi wenye uhitaji wa mikopo ya elimu ya juu kuliko watoto wa mawaziri.

#UKWELI_KUHUSU_TAARIFA_HIYO.

Baada ya kufuatilia nimegundua mambo yafuatayo:

1. Jacqueline si mtoto, ndugu wala hana unasaba wowote na Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi. Ni ufanano tu wa majina, baina ya watu hawa wawili lakini ni watu wasiofahamiana kabisa.

2. Profesa Ndalichako hana mtoto mwenye jina Jacqueline, wala hana ndugu mwenye mtoto mwenye jina hilo.

3. Watoto wa Profesa Ndalichako walishahitimu elimu ya juu na hakuna yeyote anayejiunga na elimu ya juu kwa sasa.

4. Jacqueline amehusishwa na Prof.Ndalichako kwa sababu ya ufanano wa majina, lakini si watu wenye kufanana nasaba.

5. Jacqueline hakusoma HGL kama ilivyoelezwa. Amesoma EGM na amechaguliwa kusoma Shahada ya Uchumi na Takwimu (B.A in Economics and Statistics).

6. Jacqueline anatoka familia yenye uchumi wa kawaida hivyo anakidhi vigezo vya kupewa mkopo. Amesoma St.Mary Gorreti katika mazingira ambayo si vzr kuyaeleza hapa. (Nimefuatilia taarifa za familia ya Jacqueline inayoishi Yombo Dovya lakini nisingependa kuziweka hapa).

SWALI: Je waliosema Ndalichako awajibike wamekosea?

JIBU: Hapana. Hoja ilikuwa "Kama kweli Jacqueline ni mtoto wake basi awajibike". Hii ina maana kuwa hakukuwa na sababu ya kuwajibika kama si mwanae.

SWALI: Walioibua hoja ya Jacqueline kuwa mtoto wa Ndalichako wamekosea?

JIBU: Ndio. Walioanzisha hoja hii wamekosea kwa kuwa kuna viashiria kwamba walikusudia kupotosha. Hoja hii imepata nguvu mitandaoni na kusababisha usumbufu ambao ungeweza kuepukika.

[HASHTAG]#MyTAKE[/HASHTAG]:
Kwanza niwape pole Jacqueline pamoja na Prof.Ndalichako kwa usumbufu ambao kila mmoja ameupata.

Pili niwatake wote wanaoendelea kusambaza taarifa kuwa Jacqueline na Prof.Ndalichako ni ndugu waache kufanya hivyo maana wanaweza kupotosha wengine.

Ufanano wa majina si kigezo cha kuhukumu wasio na hatia pasipo uchunguzi. Bahati mbaya Jacqueline ameingia kwenye mijadala ya mitandao bila hatia. Amekuwa victim wa social media kwa sababu za kisiasa, ambazo yeye hahusiki nazo kabisa. Pia nimpe pole Prof.Ndalichako kwa usumbufu alioupata.

Ukweli ni kwamba kufanana majina ni jambo la kawaida katika tasnia yoyote. Wapo wanafunzi wengi waliopo vyuoni au waliochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu wenye majina yanayofanana na viongozi wakubwa kisiasa lakini hawajahusishwa na viongozi hao.

Kuna mwanafunzi amechaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu Dodoma mwenye jina Gideon Wassira, lakini sijasikia akihusishwa na Mzee Stephen Wassira. Kijana Nobert Mbowe amehitimu Chuo kikuu Mlimani akisomea shahada ya Uhandisi wa madini (Mining Engineering) lakini hajawahi kuhusishwa na Mhe.Freeman Mbowe. Kuna mwanafunzi anaitwa Kennedy Yusuf Ndugai amechaguliwa shahada ya elimu maalum UDOM lakini hajahusishwa unasaba wake na Spika Job Ndugai.

Kwa hiyo nitoe wito watu waache kutumia habari inayomhusu Jacqueline kwa kumhusisha na Waziri Ndalichako maana ni watu wasio na uhusiano wowote kinasaba.

Najua wengi wamehamaki kusikia Jacqueline ni mtoto wa Waziri halafu kapewa mkopo huku watoto wa maskini wakikosa mikopo. Kumbe Jacqueline naye ni mtoto wa maskini pia, ila ameponzwa na ufanano wa majina na Waziri Ndalichako.

Nihitimishe mjadala huu kwa kutoa rai kwa "bloggers &social media emperors" kutokuendelea kujadili suala la Jacqueline na Waziri Ndalichako maana ni watu wasiofahamiana kabisa, achilia mbali kuhusiana kinasaba. Tumpe nafasi Jacqueline aweze kucocentrate ktk masomo yake, asiwe frustruted na mitandao. Let us end this discussion to save this innocent poor soul.!

Malisa GJ
Angalau Leo umeandika mambo ya maana! Endelea hivyo ila achana na kutukuza mambo ovyo kama kushabikia UKAWA!
 
Mimi ni mmoja wa wahanga wa mtoto kunyimwa mkopo kisa tu kasoma private school.

Tulipeleka vielelezo vyote kuwa mtoto ni yatima mpaka death certificates za wazazi...majibu tuliyopewa ni kwamba..kama alipata ufadhili wa kusoma private school, Basi mtafutieni mfadhili wa
kumlipia chuo..

Naomba tuishie hapa Mkuu...

Wewe ni nani mkuu? Nikijua itanisaidia kujipongeza vizuri.
 
Mimi ni mmoja wa wahanga wa mtoto kunyimwa mkopo kisa tu kasoma private school.

Tulipeleka vielelezo vyote kuwa mtoto ni yatima mpaka death certificates za wazazi...majibu tuliyopewa ni kwamba..kama alipata ufadhili wa kusoma private school, Basi mtafutieni mfadhili wa
kumlipia chuo..

Naomba tuishie hapa Mkuu...
Sawa. Kama mzazi nimekuelewa.
 
Katika sakata hili nimegundua kuwa sisi Watanzania tunachuki kali sana kwa watu wanaofanikiwa katika jambo fulani....

Mihemko ya roho ya kwanini na chuki kali vinamfanya mtu apoteze uwezo wake wa kutafakari jambo sawa sawa.....

Sisi Watanzania tunapenda sote tuwe level moja ya maisha....nyoyo zetu zinakuwa ngumu sana kukubali mafanikio ya wenzetu hasa watu wetu wa karibu......na panapotokea tu uchochoro wa kumsilibia hata kama iwe ni kwa uzushi....hapo ndipo utakapoona wanavyohamaki kuonesha kuwa walikuwa wanalingojea jambo hilo kwa muda mrefu.........

Hatuna utaratibu wa kutiana moyo kupiga hatua bali kukatishana tamaa ili mwenzio asifike ulipofika yeye.....anapenda yeye awe kileleni ili awe anawadithia anayoyaona ya juu...lakini sio kukuleta juu ili na wewe ujionee.....
Ni aina ya watu ambao kujiweka nao karibu kunaweza kupelekea anguko lako baada ya kukuinua......

Ndio nimepata kuelewa kuwa kwanini hata huko nje ya mipaka sisi tunakwepana......kwa maana tunafahamiana hila zetu......

Mwisho....naomba Mungu mkuu aziondoe jinamizi hilo kwenye nyoyo za Watanzania.......

Tusiwe wepesi wa kuhukumu kabla hata ya kujua upande wa pili......

Tufikirie kauli zetu kabla ya kuzitoa kwani kauli zetu zinaawaumiza wengine kihisia kuliko hata mijeledi ya moto.....

NB;
Kuna watoto wengine wanasomeshwa na familia zinazojiweza kwa misaada tu...lakini sio ndugu wa damu wa familia husika.....
 
Watanzania tuna sifa ya kukurupuka na huwa hatufuatilii jambo na kufahamu undani wake kabla ya kulijadili.Tujitahidi kusema kweli maana ndio utakao tuweka huru wakati wote,kuzua mambo hakuna msaada na hii imesababisha wataalamu wenzetu kuuwawa kwa kuchomwa moto kule dodoma kwa sababu ya kukurupuka kwetu wabongo.
 
Back
Top Bottom