Je, wewe ni mwanamke unayetaka kuolewa ila haufanikiwi? Ijue saikolojia iliyojificha kwa wanaume wanaotaka kuoa

EMMANUEL JASIRI

Senior Member
Feb 2, 2015
113
59
Kinacho changia wanawake wengi kuwa katika mahusiano bila ndoa ni tofauti iliyopo katika fikra ya mwanaume na mwanamke wanapo ingia katika mahusiano. Mfano mwanamke aingiapo katika mahusiano na mwanaume,mwanamke hufikiri kuwa hiyo ni hatua ya kwanza kuelekea ndoa,kitu ambacho kwa mwanaume sivyo. Mwanaume anapoingia katika mahusiano na mwanamke,huingia kwa sababu nyingi tofauti tofauti,

Mfano

Mwanaume anaweza kuingia katika mahusiano na mwanamke kwa lengo la kumchunguza/kumpeleleza mwanamke kama atafaa kuolewa naye au la. Na mwanaume asiporidhishwa na mwenendo wa tabia za huyo mwanamke,humwacha na kutafuta mwingine ataye hisi kuwa tabia zake ataelewana nazo.

Pia mwanaume anaweza kuingia katika mahusiano na mwanamke ,kwa lengo la kupata faraja,burudani na furaha ya maisha kupitia huyo mwanamke,na si kuoa. Hapo mwanamke asiposhtukia mapema aweza kudumu katika mahusiano hayo kwa miaka mingi huku akitarajia ndoa na asiolewe kama alivyo tarajia.

Hii ndio sababu utafiti unaonyesha,kati ya wanawake arobaini , wanaoingia katika mahusiano na wanaume,wanaofanikiwa kupata ndoa(kuolewa)ni wanawake kumi tu,wengine thelathini huachwa bila ndoa. Nini hupelekea wanawake wengine kuolewa na wengine kuto olewa?

Kuna vitu ambavyo wanaume huviangalia kwa mwanamke,kama kigezo cha kumfanya kuwa mke au la. Unapotaka kuolewa,ni muhimu ukafanya utafiti wa kutosha kuwa,matakwa,matarajio,malengo,mtazamio ya mwanaume mwoaji yakoje? Jiulize swali hili,wewe, kama mwanamke unaye taka ndoa,je! ,umekidhi vigezo vya wanaotaka kukuoa? Je unazo sifa au ubora wanao utaka wanaume wenye lengo na nia ya kuoa?

Lakini pia kama tulivyoona hapo juu kuwa,kuna wanaume ambao huingia katika mahusiano na mwanamke bila kuwa na lengo la kuoa,anaingia ili kupata burudani na furaha tu kupitia hayo mahusiano,

Sasa wewe mwanamke,mwenye nia ya kupata mume kwa ajili ya kukuoa,utatambuaje kuwa mwanaume uliye naye katika mahusiano kuwa ana nia, au hana nia ya kukuoa? Na ukitambua hivyo ufanyeje?

Nitakusaidia ushauri endapo utataka. Ushauri utapewa baada ya kulipia simu utakayo pigiwa moja kwa moja ili kupata ushauri katika dakika sitini. Utapewa fursa ya kuuliza maswali na kujibiwa ndani ya muda huo.

Karibu ili kupata ushauri.

Wako ni mimi ,Emmanuel

img_wallpaper_01.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

3 Reactions
Reply
Top Bottom