Je wewe ni mpinzani, mkosoajiau, waibua kero kwa Serikali?

Pantosha

JF-Expert Member
Sep 22, 2022
374
506
Naomba niweke mambo sawa ili tusiendelee kuumizana.

Kutokana na kwamba baadhi ya watu wana uelewa finyu kuhusu misamiati ya mpinzani, mkosoaji, mwanaharakati na sisi waibua kero; kuna watu wameumizwa kwa kuonekana kana kwamba ni wapinzani.

Mfano: Bwana mmoja aliona mabweni ya wanafunzi yana nyufa huku ujenzi ukiwa unaendelea. Alipotoa hizo taarifa kwa umma wa wana fungi, alisakamwa mno.

Huku kitaa ukiwa mtu wa kuripoti kero unaonekana mpinzani au mkosoaji wa Serikali.

Hii tabia ya kuwaona wanaoibua kero ni wapinzani au wakosoaji imetoka wapi?

Ni vyema watu wakawa huru kuibua kero ili Serikali izifanyie kazi.
 
Mbele ya wenye mamlaka wote mnahesabika wahalifu.

Ndio maana huko mitaan mfano likitokea tatizo ukajitia kiherehere kuwa shahidi au mtoa taarifa, ukifika kwenye vyombo vya dola hakuna rangi utaacha kuiona.
 
haya yote ni sabau za nidhamu za uoga tunazokuwa nazo na jamii inatumezesha ivo ivo haya mambo uwezi sikia nchi kam Uingerza
 
Back
Top Bottom