Kuimarika kwa CCM ni mwiba kwa Upinzani

Mdudu halisi

JF-Expert Member
May 7, 2014
2,737
2,000
Ndg zangu wana JF,

Natumaini nyote ni wazima wa afya njema.

Naomba nitumie nafasi hii kuwafahamisha watanzania wenzangu kwamba kwa mwenendo huu wanaouonesha Chama Cha Mapinduzi katika kipindi hiki cha cha Awamu ya Nne, ni dhahiri ya kwamba Wapinzani wana safari ndefu ya kuhakikisha wanaingia Ikulu. Katika uhalisia wake CCM imeendelea kukubalika vijijini na mijini hasa kutokana na utekelezaji usio wa kubabaisha wa ilani yake ya uchaguzi.

Mifano halisi ya hivi karibuni inayoonesha ni jinsi gani wananchi wamejenga moyo wa matumaini kwa chama hiki ni vile kilivyoweza kujizolea kura lukuki katika chaguzi za Madiwani katika kata 27 pamoja na chaguzi ndogo za wabunge zilizofanyika katika jimbo la Kalenga na Chalinze.

Lakini kama hiyo haitoshi, wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi katika mikutano mbalimbali ya CCM inayoendelea kote nchini, mfano mzuri ni mikutano ambayo Katibu Mkuu, Comrade Abdulrahiman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Mh. Nape Nnauye wameifanya katika mikoa ya Tabora na Singida ilivyohudhuriwa na wananchi wengi wapenda maendeleo

. Mahudhurio haya ni yamethibitisha kwamba watanzania wengi wana imani na Chama Cha Mapinduzi na kwamba ndicho kitakachowakomboa toka kwenye lindi la umaskini.

Comrade Kinana na Nape walikuwa katika ziara ya kukagua uhai wa chama pamoja na kukagua utekekelezaji wa ilani ya uchaguzi ambapo wamekagua utekelekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya za mikoa Tabora na Singida.

Si vibaya pia tukajikumbusha mafanikio haya yaliyopatikana chini ya utawala huu makini wa Chama Cha Mapinduzi;

Kwanza ni ujenzi wa misingi imara ya kiuchumi. Hapa, watanzania wamejionea ubora na uimara wa miundo mbinu, kwa mfano barabara zimeboreshwa kiasi ambacho wafanyabiashara wanauwezo wa kusafirisha bidhaa zao kutoka na kwenda kokote hapa Tanzania bila usumbufu wowote unaosababishwa na ubovu wa barabara hivyo unaweza kujipatia bidhaa yoyote ukiwa popote Tanzania hata kama ni kule kijijini Mbaha, kando kando ya ziwa Nyasa.

Reli nayo imeimarishwa kwa kufanyiwa ukarabati na sasa unaweza kusafiri kwa treni toka Dar kwenda Kigoma kwa muda wa siku mbili tu tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ilichukua muda wa siku tatu kutoka Dar kwenda Kigoma. Viwanja vya ndege vya Kigoma na Mtwara vimefanyiwa ukarabati mkubwa ikiwa ni katika kuhakikisha usafiri wa anga unaimarika.

Mafanikio mengine ya CCM ni pamoja na kuondoa kero ya ukosefu wa maji safi na salama kwa wananchi wa maeneo mbalimbali nchini, na hapa tumeshuhudia uanzishwaji wa mradi mkubwa wa maji wa ziwa Victoria ili kuondoa kero ya maji kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa. Katika sekta ya Elimu, serikali ya Chama Cha Mapinduzi imefanikiwa sana kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na ule uliohusisha Elimu ya Sekondari (MMES).

Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2002 watoto wengi waliohitimu elimu ya msingi wameweza kujiunga na elimu ya sekondari na hivyo kuhakikisha kwamba suala la kupata elimu ni haki ya kila mtoto. Pia kumekuwa na ongezeko la vijana wanaojiunga na Elimu ya Juu, huku Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ikibeba jukumu kubwa la kutoa mikopo kwa ajili ya kugharimia mafunzo na kuhakikisha kwamba vijana wote wanaojiunga na kiwango hicho cha elimu wanahitimu masomo yao.

Pia CCM imefanikiwa kuimarisha utawala bora kwa kuweka na kujenga misingi imara ya kiuongozi na kiutawala kwa kuhakikisha viongozi wanawajibika ipasavyo kwa wananchi. Kiongozi anapokosea huchukuliwa hatua za kinidhamu ama zile za kisheria na pale anapofanya vizuri hupongezwa. Katika kulitekeleza hili, tumeshuhudia viongozi mbalimbali wakipongezwa na huku wengine wakiwajibishwa kutokana na makosa mbalimbali waliyofanya.

Mfano, kuna kesi zinaendelea mahakamani kuhusiana na matumizi mabaya ya madaraka na ambapo wahusika wake ni vigogo kadhaa waliopata kuhudumu kwenye serikali ya Chama Cha Mapinduzi.

Lakini kuimarika kwa miundo mbinu kama vile majengo mbalimbali kwa ajili ya makazi ya watu na ofisi mbalimbali za idara za serikali na mashirika ya umma ni mafanikio mengine ambayo CCM wamejipatia katika kipindi chote cha utawala wao.
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,292
2,000
Yaani kwa sasa kusema ukweli mimi nawaonea huruma upinzani, hususan watani zangu "magwanda".

Kinana tafadhali, punguza spidi, regeza na kamba hawa jamaa zetu wapumue kidogo, unakaba mpaka kivuli!

Mheshimiwa Kinana nakuomba kwa heshima na taadhima, unawamaliza hawa na siasa inakuwa haina raha tena, hebu punguza ghadhab upumzike kidogo na hawa jamaa zangu wapumue japo "kiduchu".

Sasa wewe Mnyika si ndiyo ulisema Rais "dhaifu", kamuombe radhi Mwenyekiti wa CCM, mmemuudhi mpaka kamtoa Kinana kwenye ustaafu sasa anawaumiza.

Rais Kikwete najuwa Kinana hawezi kupunguza spidi bila wewe kumwambia, tafadhali rudisha roho unatutoa raha ya kupiga porojo za unazi na hawa jamaa zetu, maana sasa hata humu JF wanaonyesha wazi wazi hasira zao na wamebaki matusi tu.

Nakuomba Rais Kikwete, Mwenyekiti wangu, wahurumie.
 

Mdudu halisi

JF-Expert Member
May 7, 2014
2,737
2,000
Yaani kwa sasa kusema ukweli mimi nawaonea huruma upinzani, hususan watani zangu "magwanda".

Kinana tafadhali, punguza spidi, regeza na kamba hawa jamaa zetu wapumue kidogo, unakaba mpaka kivuli!

Mheshimiwa Kinana nakuomba kwa heshima na taadhima, unawamaliza hawa na siasa inakuwa haina raha tena, hebu punguza ghadhab upumzike kidogo na hawa jamaa zangu wapumue japo "kiduchu".

Sasa wewe Mnyika si ndiyo ulisema Rais "dhaifu", kamuombe radhi Mwenyekiti wa CCM, mmemuudhi kamtoa Kinanan kwenye ustaafu sasa anawaumiza.

Rais Kikwete najuwa Kinana hawezi kupunguza spidi bila wewe kumwambia, tafadhali rudisha roho unatutoa raha ya kupiga porojo za unazi na hawa jamaa zetu, maana sasa hata humu JF wanaonyesha wazi wazi hasira zao na wamebaki matusi tu.

Nakuomba Rais Kikwete, wahurumie.
Ni speed 120 kwenye barabara ya vumbi. Hatari sana.
 

Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Katika kushauriana na wataalamu, nilipata kipande cha uchunguzi ambacho nitakiambatanisha hapo chini. I was shocked. Lakini nashauri hoja na majibu yetu yapimwe hapo. (Naogopa tusijekuwa tunafit criteria za sample ya uchunguzi huo)


Countries With The Highest Average IQ
RankCountryAverage IQ
1Hong Kong107
2South Korea106
3Japan105
4Taiwan104
5Singapore103
6Austria102
6Germany102
6Italy102
6Netherlands102
10Sweden101
10Switzerland101
12Belgium100
12China100
12New Zealand100
12United Kingdom100
16Hungary99
16Poland99
16Spain99
19Australia98
19Denmark98
19France98
19Mongolia98
19Norway98
19United States98
25Canada97
25Czech Republic97
25Finland97
Countries With The Lowest Average IQ
1Equatorial Guinea59
2Ethiopia63
3Sierra Leone64
4Democratic Republic of the Congo65
5Zimbabwe66
5Guinea66
7Nigeria67
8Ghana71
9Tanzania72
9Sudan72
 

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Ukweli uko wazi juu ya hili wataiona ccm inasonga mbele kwa kuwatumikia watanzania.
 

Mdudu halisi

JF-Expert Member
May 7, 2014
2,737
2,000
Katika kushauriana na wataalamu, nilipata kipande cha uchunguzi ambacho nitakiambatanisha hapo chini. I was shocked. Lakini nashauri hoja na majibu yetu yapimwe hapo. (Naogopa tusijekuwa tunafit criteria za sample ya uchunguzi huo)


Countries With The Highest Average IQ
RankCountryAverage IQ
1Hong Kong107
2South Korea106
3Japan105
4Taiwan104
5Singapore103
6Austria102
6Germany102
6Italy102
6Netherlands102
10Sweden101
10Switzerland101
12Belgium100
12China100
12New Zealand100
12United Kingdom100
16Hungary99
16Poland99
16Spain99
19Australia98
19Denmark98
19France98
19Mongolia98
19Norway98
19United States98
25Canada97
25Czech Republic97
25Finland97
Countries With The Lowest Average IQ
1Equatorial Guinea59
2Ethiopia63
3Sierra Leone64
4Democratic Republic of the Congo65
5Zimbabwe66
5Guinea66
7Nigeria67
8Ghana71
9Tanzania72
9Sudan72
Kwa maana nawe ni miongoni mwa wenye IQ kiduchu mkuu!
 

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,614
2,000
Waambie waandae hiyo mikutano bila kusomba watu na Malori,kuweka Pombe za gongo na Ulanzi,na kugawa buku mbili mbili na ubwabwa then Utuletee tathmini.

Ccm is no more.
 

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,394
2,000
Ndg zangu wana JF,
Natumaini nyote ni wazima wa afya njema.
Naomba nitumie nafasi hii kuwafahamisha watanzania wenzangu kwamba kwa mwenendo huu wanaouonesha Chama Cha Mapinduzi katika kipindi hiki cha cha Awamu ya Nne, ni dhahiri ya kwamba Wapinzani wana safari ndefu ya kuhakikisha wanaingia Ikulu. Katika uhalisia wake CCM imeendelea kukubalika vijijini na mijini hasa kutokana na utekelezaji usio wa kubabaisha wa ilani yake ya uchaguzi. Mifano halisi ya hivi karibuni inayoonesha ni jinsi gani wananchi wamejenga moyo wa matumaini kwa chama hiki ni vile kilivyoweza kujizolea kura lukuki katika chaguzi za Madiwani katika kata 27 pamoja na chaguzi ndogo za wabunge zilizofanyika katika jimbo la Kalenga na Chalinze. Lakini kama hiyo haitoshi, wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi katika mikutano mbalimbali ya CCM inayoendelea kote nchini, mfano mzuri ni mikutano ambayo Katibu Mkuu, Comrade Abdulrahiman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Mh. Nape Nnauye wameifanya katika mikoa ya Tabora na Singida ilivyohudhuriwa na wananchi wengi wapenda maendeleo. Mahudhurio haya ni yamethibitisha kwamba watanzania wengi wana imani na Chama Cha Mapinduzi na kwamba ndicho kitakachowakomboa toka kwenye lindi la umaskini.
Comrade Kinana na Nape walikuwa katika ziara ya kukagua uhai wa chama pamoja na kukagua utekekelezaji wa ilani ya uchaguzi ambapo wamekagua utekelekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya za mikoa Tabora na Singida.

Si vibaya pia tukajikumbusha mafanikio haya yaliyopatikana chini ya utawala huu makini wa Chama Cha Mapinduzi;

Kwanza ni ujenzi wa misingi imara ya kiuchumi. Hapa, watanzania wamejionea ubora na uimara wa miundo mbinu, kwa mfano barabara zimeboreshwa kiasi ambacho wafanyabiashara wanauwezo wa kusafirisha bidhaa zao kutoka na kwenda kokote hapa Tanzania bila usumbufu wowote unaosababishwa na ubovu wa barabara hivyo unaweza kujipatia bidhaa yoyote ukiwa popote Tanzania hata kama ni kule kijijini Mbaha, kando kando ya ziwa Nyasa. Reli nayo imeimarishwa kwa kufanyiwa ukarabati na sasa unaweza kusafiri kwa treni toka Dar kwenda Kigoma kwa muda wa siku mbili tu tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ilichukua muda wa siku tatu kutoka Dar kwenda Kigoma. Viwanja vya ndege vya Kigoma na Mtwara vimefanyiwa ukarabati mkubwa ikiwa ni katika kuhakikisha usafiri wa anga unaimarika.

Mafanikio mengine ya CCM ni pamoja na kuondoa kero ya ukosefu wa maji safi na salama kwa wananchi wa maeneo mbalimbali nchini, na hapa tumeshuhudia uanzishwaji wa mradi mkubwa wa maji wa ziwa Victoria ili kuondoa kero ya maji kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa. Katika sekta ya Elimu, serikali ya Chama Cha Mapinduzi imefanikiwa sana kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na ule uliohusisha Elimu ya Sekondari (MMES). Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2002 watoto wengi waliohitimu elimu ya msingi wameweza kujiunga na elimu ya sekondari na hivyo kuhakikisha kwamba suala la kupata elimu ni haki ya kila mtoto. Pia kumekuwa na ongezeko la vijana wanaojiunga na Elimu ya Juu, huku Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ikibeba jukumu kubwa la kutoa mikopo kwa ajili ya kugharimia mafunzo na kuhakikisha kwamba vijana wote wanaojiunga na kiwango hicho cha elimu wanahitimu masomo yao.

Pia CCM imefanikiwa kuimarisha utawala bora kwa kuweka na kujenga misingi imara ya kiuongozi na kiutawala kwa kuhakikisha viongozi wanawajibika ipasavyo kwa wananchi. Kiongozi anapokosea huchukuliwa hatua za kinidhamu ama zile za kisheria na pale anapofanya vizuri hupongezwa. Katika kulitekeleza hili, tumeshuhudia viongozi mbalimbali wakipongezwa na huku wengine wakiwajibishwa kutokana na makosa mbalimbali waliyofanya. Mfano, kuna kesi zinaendelea mahakamani kuhusiana na matumizi mabaya ya madaraka na ambapo wahusika wake ni vigogo kadhaa waliopata kuhudumu kwenye serikali ya Chama Cha Mapinduzi.

Lakini kuimarika kwa miundo mbinu kama vile majengo mbalimbali kwa ajili ya makazi ya watu na ofisi mbalimbali za idara za serikali na mashirika ya umma ni mafanikio mengine ambayo CCM wamejipatia katika kipindi chote cha utawala wao.

Ok siku hizi hamubebi tena watu kwa malori? km wanankuja wenyewe vema. Kina masanja na wasanii wengine hawatumiki tena? Nyie wenyewe ndio mnaojua nguvu kubwa mnayotumia kuleta watu kwenye mikutano. Mbona jana watu walikuwa wanaondoka wakati mkutano unaendelea?....
 

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Poleni sana, Kinana na Kikwete wanakaba mpaka kivuli. Tumewaomba humu wapunguze spidi kidogo inakuwa hamna raha ya kuwa na upinzani.
Jk na kinana ni kiboko yao wapinzani watajuta kuwepo kwa jk na kinana kwenye siasa.
 

Arnold Ringo

Verified Member
Jan 23, 2014
2,319
1,170
Nafikiri Mleta Mada huna uwakika na unachosema Maana ungekua na uwakika ugetazama Ukawa wanachofanya na ccm mlipo poleni sana tena sana serekali Tatu ndio suluhu la matatizo ya Tanganyika tuitakayo
 

Mdudu halisi

JF-Expert Member
May 7, 2014
2,737
2,000
Ok siku hizi hamubebi tena watu kwa malori? km wanankuja wenyewe vema. Kina masanja na wasanii wengine hawatumiki tena? Nyie wenyewe ndio mnaojua nguvu kubwa mnayotumia kuleta watu kwenye mikutano. Mbona jana watu walikuwa wanaondoka wakati mkutano unaendelea?....
Mkuu, kitendo cha watu kuondoka wakati mkutano unaendelea ni cha kawaida sana kwani hata kwenye mikutano ya UKAWA hayo yanatokea.
 

Mdudu halisi

JF-Expert Member
May 7, 2014
2,737
2,000
Nafikiri Mleta Mada huna uwakika na unachosema Maana ungekua na uwakika ugetazama Ukawa wanachofanya na ccm mlipo poleni sana tena sana serekali Tatu ndio suluhu la matatizo ya Tanganyika tuitakayo
Kwani UKAWA wamefanya nini cha ajabu, mbona kule Mafinga wananchi walibeba mabango kuwapinga?
 

Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,783
2,000
Kinana ametengeneza CCM ndani ya CCM ndiyo kuimalika huko?Ulishawahi ona wapi chama tawala kinaiponda serekali yake?Hapo hakuna chochote cha maana alichokifanya Kinana.Alichokifanya Kinana ni kuangalia ni kitu gani ambacho kinatumiwa na wapinzani kuwavutia wananchi akagundua kuwa ili uweze kuwapata wananchi ni kuishambulia serekali kwa maovu inayoyafanya wakati maovu hayo ni ya CCM yenyewe na kuendeleza kutoa ahadi nyingi ambazo nyingi zimeshindwa kutekelezwa na hazitekelezeki.Alicho kifanya Kinana ni kufanya yale ambayo wapinzani wanayafanya baada ya kugunduwa kuwa wapinzani wanayatumia hayo kuibomoa CCM.Kwa hiyo Kinana aliona kuwa hakuna jipya ambalo anaweza kulifanya ili wananchi waendelee kuihurumia CCM isipokuwa ni kuunda upinzani ndani ya CCM ili ifanane na wapinzani halisi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom