Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,468
- 113,583
Wanabodi,
Kwanza angalieni hii picha
More than 60% of Rwanda’s parliamentarians are women. Photo: Sam Ngendahimana
Nimesoma kwenye Ripoti ya WB, Bunge la Rwanda ndilo Bunge linaloongoza Dunia kwa gender equality baada ya kuwa na asilimia kubwa ya wabunge wanawake kuliko wanaume, wakati Bara la Africa likiongoza duniani kwa kuwa na maspika wengi wanawake kuliko mabara yote.
Hii maana yake ni gender equality is possible ila pia nafasi za upendeleo kwa wanawake vikiwemo viti maalum, dhumuni lake sio kuongeza tuu idadi ya wanawake bungeni, bali ni kuwajengea uwezo wabunge wanawake walioteuliwa, yaani empowerment, kuwa empower.
Hilo kwa Rwanda limewezekana kwasababu ubunge wa viti maalum kule ni kwa awamu moja tuu, awamu ya pili wanakwenda majimboni na kupisha wengine.
Mnaonaje na sisi Tanzania tukafuata mfumo huo?.
Japo sio neno zuri kulitumia lakini ndio ukweli wenyewe, Ubunge wa Viti Maalum ni ubunge wa kubebwa. Sasa kama wewe Mbunge mwanamke umebahatika kubebwa, ukaukwaa ubunge wa Viti Maalum, na ukakaa Bungeni miaka 5, maana yake umeisha kuwa empowered, huhitaji kubebwa tena kumendea ubunge kupitia Viti Maalum, sasa unakuwa umeiva kustahili kwenda kugombea jimboni.
Kama umekuwa Mbunge Viti Maalum miaka mitano na bado huwezi kwenda jimboni, then wewe utakuwa hufai, hata ukirudi Bungeni utakuwa huna jipya!, hivyo ni bora upumzishwe, wapewe nafasi wengine wenye uwezo wa kujiongeza kwasababu kiukweli kabisa kuna baadhi ya hawa wabunge wa viti maalum huwasikii wakichangia mjadala wowote zaidi ya kuupara na kutokelezea, hadi watu humu kuwabatiza jina la Wabunge wa "Vitu Maalum".
Ukibebwa, bebeka, haiwezekani mtu ubebwe mara ya kwanza, uvushwe mto mpaka ng'ambo ya pili, halafu baada ya kufika upande wa pili, badala ya kushuka na kutembea mwenyewe, wewe bado unang'ang'ania mgongoni uendelee kubebwa!. Kitakacho fuata hapo ni wewe kubwaga tuu chini puu!, unless huyo anayekubeba, naye anapata uroda fulani kukubeba,maana kiukweli ukibeba chochote nimzigo kwako,ila kama mzigo huo unafaida kwako, japo ni mateso kuendelea kuubeba, utaendelea kuubeba tuu.
Mnaonaje wanabodi, hawa wabunge wa kubebwa kupitia Viti Maalum, wawekewe ukomo wa miaka 5 tuu au kwa sababu kubebwa ni raha, na kula uroda hivyo wabebaji wanapenda kuendelea tuu kubeba na wabebwaji wanaona uroda kubebwa?.
Ukibebwa bebeka, na next time jibebe, usibwete, na kupenda kuendelea kubebwa tuu, oneni aibu!. Tuweni kama Rwanda!.
Vipi wajameni, wa kubebwa waendelee kubebwa tuu au wajibebe, na wasipojibeba wabwagwe?
Paskali

Africa takes historic lead in female parliamentary speakers
The archetype of the strong African woman standing as an unmoving pillar of her community is one that transcends national borders on the African continent. While in the past, this image often faded the instant a woman crossed the threshold of business or politics, 2019 saw...
blogs.worldbank.org