econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 15,766
- 21,761
Ningependa kukishauri chama Cha CHADEMA kiweke mfumo mzuri wa viti maalum ulio wazi Ili kuepuka Yale ya Covid 19 yasijirudie. Tujifunze kutokana na makosa, la sivyo huko mbeleni litajirudia Tena. Hili la kusema wanawake waliogombea majimboni na kushindwa watapewa nafasi ya mbele kwenye Viti Maalim sio mzuri kabisa.
Akina Halima Mdee walitumia huo mwanya kujiingiza bungeni bila kufuata kanuni na sheria. Inakuaje mnaruhusu mgombea ubunge jimboni akishindwa kwenye Jimbo anapewa nafasi ya viti maalum?
Halima Mdee kagombea Kawe kashindwa na Ask. Gwajima halafu Cha kushangaza anawaacha wote walioshinda viti maalum huko mikoani Dares salaam kwenye chama na kujipeleka bungeni.
Nadhani Ni muda Sasa turuhusu wale waliogombea viti maalum kwenye majimbo au Mkoa ndio wapewe nafasi za viti maalum,baadala ya kuwapa walioshindwa majimboni. Inaondoa maana ya viti maalum
Kwa mfano, Esther matiko aligombea tarime, bulaya aligombea bunda, kaboyoka same, Mdee aligombea kawe, makamba aligombea shinyanga, mwaifunga aligombea Tabora mjini, etc. Lakini wote Hawa na wengine wamechukua nafasi za wale walioshinda viti maalum.
Tuamue moja anayekubali kugombea viti maalum agombee na apewe nafasi na anayegombea jimboni agombee akishindwa ajiandae kwa uchaguzi mwingine.
Pia chama kijitahidi kabla ya uchaguzi kiwe tayari na list yake ya wabunge wa viti maalum, ili wakichakachua kuwepo na rejea ya kupitia majina halali. Sio mpaka uchguzi uishe ndio Tume isubirie majina Hapo ndipo wenye Nia ovu wanatumia kuvuruga chama.