Je, waandishi wa Biblia hawakuona aibu kufanya ‘Plagiarism’ ya wazi wazi kwenye ‘Vibao vya Sumeria’ na kufanya editing bila aibu kabisa?

Sasa badala ya kushusha nondo ushaanza kubishana na watu...watu nao hawajashushiwa nondo washaanza kukushushia furushi la mabishano.kama unachakusema we sema mabishano baadae.mi nangoja hayo maneno EB Fanya chap kushusha mavituz
 
Asili ya wanadamu kwa mujibu wa vibao vya kale vya Sumeria.

Sumeria, au ardhi ya ’wafalme waliostaarabika’ ilistawi huko Mesopotamia, kwa sasa panaitwa Iraq, kwenye miaka 4500BC. Wasumeria walifanikiwa kutengeneza himaya za kiutawala zenye mifumo yao wenyewe ya ujenzi , sanaa, unajimu wa nyota na hisabati. Mfumo wao wa kidini ulikuwa mtambuka sana na ulihusisha mamia ya miungu. Kwa mujibu wa maandiko ya kale, kila mji wa Sumeria ulilindwa na mungu wake; na japo binadamu waliishi sambamba na miungu, binadamu walikuwa ni watumishi wa miungu.
Hadithi ya uumbaji kutoka kwa waSumeria inapatikana katika kibao cha udongo kilichovumbuliwa huko Nippur, katika Mesopotamianya kale, mji ulioundwa takriban miaka 5000 kabla ya kuzaliwa kristu.
Uumbaji wa Dunia (Enuma Elish) kwa maelezo ya vibao vya Sumeria ulikuwa hivi:

“Wakati katika anga za juu mbingu haikuwa na jina,
Na ambapo dunia chini yake haikuwa na jina, Na ambapo Apsu wa kale, aliezifanya kuwa,
Na vurugu, Tiamut, mama wa wote wawili
Maji yao yalikorogwa pamoja,
Na hakuna ardhi iliyotengenezwa, hakuna kinamasi kilichoundwa; kipindi ambacho katika miungu, hakuna aliyeitwa kuwa, Na hakuna kati yao aliekuwa na jina, na hakuna hatma zilizokuwa zimekwisha kugawiwa; Basi hapo wakaumbwa ‘miungu’ katikati ya mbingu, Lahmu na Lahamu wakaitwa kuwa...”


Hadithi za waSumeria zinadai kwamba, hapo mwanzo, ‘Miungu’ wenye mfanano na binadamu walitawala Dunia. Walipokuja Duniani, kulikuwa na kazi nyingi sana za kufanya, na waliifanyia kazi ardhi, waliichimba kuifanya iwe sehemu inayoweza kubeba uhai huku wakichimba madini yake .
Maandiko hayo yanasema kwamba, baada ya muda ‘Miungu’ hao walifanya mgomo kutokana na kazi hiyo kuwa ngumu sana.
Miungu hao walipoifanya kazi hiyo ngumu
Waliona ni mateso makali sana, maumivu ya uvujaji jasho wao ulikuwa mkubwa sana
Kazi ilikuwa nzito, mateso yalikuwa makali.
ANU, mungu wa miungu, alikiri kwamba kweli kazi hiyo ilikuwa ni nzito sana. Mtoto wake wa kiume ENKI, akatoa wazo kwamba aumbwe binadamu ili abebe mzigo huo mzito wa kuvuja jasho na kufanya kazi hiyo nzito, na hivyo basi, kwa msaada wa dada yake nusu aitwae NINKI, wakafanya ikawa . mungu mmoja wapo akauwawa, na mwili wake na damu yake vikachanganywa na udongo wa mfinyanzi. Na kutokana na mchanganyiko huo binadamu wa kwanza akaumbwa, kwa mfano wa miungu hao.

“Mmemuua mmoja wa miungu pamoja na haiba yake
Hivyo basi nimewaondolea mateso ya kazi yenu nzito
Kazi hiyo nzito nimeihamishia Kwa binadamu.

...”

Katika udongo (mfinyanzi), mungu na bindamu wataunganishwa,
Kwa umoja utakaoletwa pamoja;
Ili katika siku za mwisho
Mwili na roho
Ambavyo katika mungu vimeiva –
Kiasi roho katika udugu wa damu viunganishwe.

Binadamu wa kwanza aliumbwa ‘Eden’, Eden ni neno la kiSumeria linalomaanisha ardhi isiyo na mabonde. Katika maandiko ya Gilgamesh, Eden ipo Mesopotamia kati ya mito ya Tigris na Euphrates.

Hapo chini, ni moja wapo ya vibao vya Sumeria, vikimuonyesha ENKI katika hadithi ya uumbaji

79E32A6A-6B85-451B-9DC4-53A8EE7630BB.jpeg


Hapo awali binadamu hawakuweza kuzaliana wenyewe, ila baadae walifanyiwa maboresho kwa msaada wa Enki na Ninki.
Hivyo, Adapa akaumbwa kama binadamu kamili anayejitegemea na aliyejitosheleza katika ukamilifu wake. Maboresho haya yalifanyika bila ruhusa ya kaka yake ENKI, aliyeitwa ENLIL, na ugomvi mkubwa baina ya miungu ukaanza. ENLIL akawa adui mkubwa wa binadamu, na kibao hicho cha Sumeria kinasema kwamba binadamu waliwatumikia miungu na walipitia nyakati ngumu na mateso makali sana katika utumishi wao kwa miungu.

Adapa, kwa msaada wa ENKI, alipalizwa hadi juu kwa Anu ambapo alishindwa kujibu swali kuhusu ‘mkate na maji ya uzima’.

Hadithi za waSumeria
Uumbaji wa wanadamu


Shairi hili linaanza kwa kuelezea jinsi ilivyowabidi miungu kufanya kazi kwa ajili ya mkate wao wa kila siku kwa kuchimba mifereji mikubwa ya umwagiliaji:
Miungu walikuwa wakichimba mito na kuweka mchanga pembeni
na miungu waliokuwa wanachimba mfinyanzi wakaanza kulalamika.
Nammu, ambae ni mungu wa bahari na mito, akaenda kwa mtoto wake aitwae ENKI, ambae alikuwa amelala na akamuamsha kutoka usingizini na kumuamrisha kwa kusema "waumbe watumishi wa miungu". Enki, ambae ndiye mungu wa hekima, akawaza kuhusu nguvu ya urutubishaji ya mfinyanzi na maji ya kinamasi, kisha akamwambia Nammu awaamrishe miungu wa ‘tumbo la uzazi’ waufinye huu mfinyanzi na kisha wafinyanzi waufanye uwe mzito ili aweze kuufinyanga na kuzaa.

“Changanya moyo wa mfinyanzi uliopo kwenye kinamasi,
Kisha wafinyanzi wataufanya uwe mzito,
Wewe, [Nammu] fanya mikono na miguu iwe;
Ninmah [mama wa dunia au mungu wa uzazi] atafanya kazi juu yako, mungu wa uzazi atakuwa pembeni yako wakati wa uumbaji wa kijusi; O mama yangu, toa hatma yake (kijusi tumboni),
Ninmah atahuisha sura ya uso wa miungu kwenye kijusi hicho,
ni mwanaume . . . .

Hivyo mwanadamu aliumbwa ili kuwapunguzia miungu mzigo wa kazi nzito na ngumu.

Miungu wakaamua kufanya karamu kubwa sana ili kusheherekea uumbaji huu mpya wa binadamu ambao wangebeba mzigo wa kazi zao, Kisha Enki na Ninmah wakaanza kunywa bia / pombe na kisha ‘wakaanza kujisikia vizuri ndani yao’
Ninmah akaanza kujisifia kwamba yeye, akiwa kama mungu wa uzazi na tumbo la uzazi, ndiye anaeamua kama uumbaji wa kijusi tumboni uende vizuri au uende mrama. Enki akajibu kwamba yeye, akiwa kama mungu wa hekima na mwerevu, anaweza akamtafutia nafasi ya utumishi katika jamii hata kwa wale watakaozaliwa na vilema vya aina mbalimbali. Ninmah akaumba kutoka katika udongo mwanaume mwenye mikono inayotetemeka, lakini Enki akampa kazi ya utumishi wa mfalme. Baada ya hapo Ninmah akaumba mwanaume kipofu, lakini ENKI akamfanya mwimbaji wa hadithi. NINMAH akaamuma kuumba mwanaume mwenye miguu iliyopinda, lakini ENKI akamfanya kuwa mtumishi wa wafua vyuma. NINMAH akaendelea kuumba binadamu wenye vilema: "akaumba mtu asiyeweza kuzuia mkoja wake, akaumba mwanamke tasa, akamumba binadamu asiyekua na jinsia ya kiume wa ya kike, na vilema vingine vya aina mbali mbali, lakini mara zote hizo ENKI aliweza kumtafutia kilema huyo nafasi katika jamii na kiweza kuendesha maisha yake". Mwanamke ambae hakuweza kuzaa kwa mfano, alipewa nafasi ya kuwasimamia wasusi katika nyumba ya malkia,
, na yule mtu aliyezaliwa bila jinsia alipewa nafasi ya kusimama pembeni ya mfalme.

NINMAH baada ya kuona amezidiwa ujanja na ENKI, akautupa chini ule
Mfinyanzi wa uumbaji kwa hasira. Sasa ENKI akaamua yeye kuumba binadamu mwenye kilema, na akamzodoa NINMAH ajaribu kama ataweza kuamua aina ya kilema atakachozaliwa nacho mtu huyo. Sasa ENKI, katika namna ambayo haijaelezwa vizuri sana kwenye kibao hiki, akafanya mtu azaliwe njiti (kabla ya siku zake)" . Kiumbe kilichozaliwa kilikuwa na ulemavu wa hali ya juu sana : Mikono yake ilitetemeka, / hakuweza kuweka chakula mdomoni, / uti wake wa mgongo ulikuwa umepinda vibaya, / njia yake ya haja kubwa ilikuwa imeziba/ mifupa ya mapaja ilikuwa laini, / miguu na ngozi yake ilikuwa inavunjika vunjika / hakuweza kutembea kwenye kinamasi. NINMAH akajaribu kumlisha kipande cha mkate kiumbe huyo, lakini alikuwa dhaifu sana na hakuweza kula mkate aliopewa. Hakuweza kusimama, wala kukaa wala kukunja magoti yake. NINMAH alipata mshangao wa uwoga pamoja na huzuni kwa kile alichokiumba ENKI na akamlaani kwa kitendo hicho, maana NINMAH aliona kwamba endapo watu wenye vilema vikali aina hii watazaliwa mara kwa mara basi watu wataacha kumuabudu. ENKI akaamua kupooza hasira za ninmah kwa kukiri kwamba kiumbe kile chenye ulemavu hakikuwa kazi ya mikono ya NINMAH bali kazi ya mikono yake.
Shairi linaisha kwa wimbo wa kutukuza nguvu na uwezo wa uumbaji wa kiume wa ENKI pamoja na werevu wake, lakini hadithi yenyewe pia inajaribu kuonyesha kwamba ENKI haweza kufanya uumbaji bila msaada wa mungu wa uzazi NINMAH.

Pia hadithi inavuta zaidi umakini kwa kuanza na miungu wanaofanya kazi ngumu kwa ajili ya mkate wao wa kila siku, halafu inaisha kwa kiumbe kisichoweza kupewa mkate na mungu wa uzazi.

Sehemu ya chini ya kibao hiki kimekatika na hakuna anaejua kilichoandikwa kwenye kipande hicho cha chini, hivyo hadithi imebidi iishie hapa. Kwa anaetaka kukiona anaweza kutembele kwenye jumba la makumbusho huko Uingereza, unalipia kiingilio kidogo tu.

Tujiandae kwa hadithi ya kibao kingine kinachofauta, vibao vipo maelfu kwa maelfu.
 
Kwa hiyo unashauri tuamini kuwa Quran ilishuka kutoka juu kama papai linavyodondoka? Maana bwana mtume hakujua kusoma wala kuandika.
Njemba Soro.: Mbona hapo hakuna sehemu hata moja fanani amehusisha Quran?, Ebu tujitahidi kujibu au kuchangia kutokana na mada husika tukiwa watu wa namna hii huwa tunaonekana hatuna hoja.
 
Kwa maandiko ayo usiseme biblia tu bali sema "Je, waandishi wa vitabu vya dini (Biblia na Quran) hawakuona aibu kufanya ‘Plagiarism’ ya wazi wazi kwenye ‘Vibao vya Sumeria’ na kufanya editing bila aibu kabisa?" Maana naona wote wameenda tofauti na ayo maandiko.
Hiyo ya Quran ielezee wewe labda yeye kayaona ya biblia tu vipi au ya Quran atayaleta baadae, cha msingi hapa nakushauri jikite kwenye hoja husika kwanza.
 
Tunapima umri wa vitu kwa kutumia mbinu za kisayansi, mfano vitu vilivyokuwa na asili ya uhai (organic) tunatumia Carbon dating, vitu kama mawe pia vina ‘method yake’ . hivyo vibao vimetambulika kwa mbinu hizo kuwa na miaka 3,000 zaidi ya kipindi cha kuandikwa kwa biblia. Maana hata sasa kuna mashahidi ya kaburini yanaandikwa kwenye mawe, ila haimaanishi mashahidi haya yana umri zaidi ya vibao vya sumeria
Is Carbon 14 accurate?

At least to the uninitiated, carbon dating is generally assumed to be a sure-fire way to predict the age of any organism that once lived on our planet. Without understanding the mechanics of it, we put our blind faith in the words of scientists, who assure us that carbon dating is a reliable method of determining the ages of almost everything around us. However, a little more knowledge about the exact ins and outs of carbon dating reveals that perhaps it is not quite as fool-proof a process as we may have been led to believe.

What is Carbon Dating?

At its most basic level, carbon dating is the method of determining the age of organic material by measuring the levels of carbon found in it. Specifically, there are two types of carbon found in organic materials: carbon 12 (C-12) and carbon 14 (C-14). It is imperative to remember that the material must have been alive at one point to absorb the carbon, meaning that carbon dating of rocks or other inorganic objects is nothing more than inaccurate guesswork.

All living things absorb both types of carbon; but once it dies, it will stop absorbing. The C-12 is a very stable element and will not change form after being absorbed; however, C-14 is highly unstable and in fact will immediately begin changing after absorption. Specifically, each nucleus will lose an electron, a process which is referred to as decay. This rate of decay, thankfully, is constant, and can be easily measured in terms of ‘half-life’.

Half-life refers to the amount of time it takes for an object to lose exactly half of the amount of carbon (or other element) stored in it. This half-life is very constant and will continue at the same rate forever. The half-life of carbon is 5,730 years, which means that it will take this amount of time for it to reduce from 100g of carbon to 50g – exactly half its original amount. Similarly, it will take another 5,730 years for the amount of carbon to drop to 25g, and so on and so forth. By testing the amount of carbon stored in an object, and comparing to the original amount of carbon believed to have been stored at the time of death, scientists can estimate its age.

So what’s the Problem?

Unfortunately, the believed amount of carbon present at the time of expiration is exactly that: a belief, an assumption, an estimate. It is very difficult for scientists to know how much carbon would have originally been present; one of the ways in which they have tried to overcome this difficulty was through using carbon equilibrium.

Equilibrium is the name given to the point when the rate of carbon production and carbon decay are equal. By measuring the rate of production and of decay (both eminently quantifiable), scientists were able to estimate that carbon in the atmosphere would go from zero to equilibrium in 30,000 – 50,000 years. Since the universe is estimated to be millions of years old, it was assumed that this equilibrium had already been reached.

However, in the 1960s, the growth rate was found to be significantly higher than the decay rate; almost a third in fact. This indicated that equilibrium had not in fact been reached, throwing off scientists’ assumptions about carbon dating. They attempted to account for this by setting 1950 as a standard year for the ratio of C-12 to C-14, and measuring subsequent findings against that.

Has it Worked?

In short, the answer is… sometimes. Sometimes carbon dating will agree with other evolutionary methods of age estimation, which is great. Other times, the findings will differ slightly, at which point scientists apply so-called ‘correction tables’ to amend the results and eliminate discrepancies.

Most concerning, though, is when the carbon dating directly opposes or contradicts other estimates. At this point, the carbon dating data is simply disregarded. It has been summed up most succinctly in the words of American neuroscience Professor Bruce Brew:

“If a C-14 date supports our theories, we put it in the main text. If it does not entirely contradict them, we put it in a footnote. And if it is completely out of date, we just drop it.”

What does this mean for Contemporary Carbon Dating?

Essentially, this means that carbon dating, though a useful tool, is not 100% reliable. For example, recently science teams at the British Antarctic Survey and Reading University unearthed the discovery that samples of moss could be brought back to life after being frozen in ice. The kicker? That carbon dating deemed the moss to have been frozen for over 1,500 years. Now, if this carbon dating agrees with other evolutionary methods of determining age, the team could have a real discovery on their hands. Taken alone, however, the carbon dating is unreliable at best, and at worst, downright inaccurate.
 
Ungejiuliza kwanza Wwe hiyo Akili yako

,Ukristo wa Leo umewagawanya Watu na Kuwafamya Wawe na Chuki Kati Yao ,Mkatoliki hawawezi kuoana na Msabato, Msabato hataki kuolewa na Anglicana.

Mmegawanyika Hamna Umoja Wowote ule maana Mnasimamia Kitu kisicho na Ukweli ndani yake.

Dini ipi ambayo haijagawanyika na haina chuki taja moja tu nami nitakuonyesha madhaifu with evidence. Ila usitaje uislam maana huo ndio uozo wa chuki miongoni mwao na hatari kuliko dini nyingjne maana wana madhehebu mengi na wana chuki wazi wazi kwa kuchapa hata dibaji kwenye kitabu chao kuonesha chuki ya kimadhehebu
 
Dini ipi ambayo haijagawanyika na haina chuki taja moja tu nami nitakuonyesha madhaifu with evidence. Ila usitaje uislam maana huo ndio uozo wa chuki miongoni mwao na hatari kuliko dini nyingjne maana wana madhehebu mengi na wana chuki wazi wazi kwa kuchapa hata dibaji kwenye kitabu chao kuonesha chuki ya kimadhehebu
Haipo Dini Maana Mungu Haitaji Kuabudiwa Katika Dini na Mgawanyike kwa Ajili yake.

Kwahiyo ukijiona Unaabudu katika Dini Yeyote jua unaabudu Viumbe siyo Mungu, Mungu mwenye vyote haabudiwi katika Dini Yeyote Unayoijua wewe

Dini ni mfumo wa Viumbe kuabudiana Wao kwa Wao ndio maana Unaona Kuna Makundi makundi kwa Sababu kila Mmoja anataka mamlaka yake mwenywe kwa mambo yake
 
Kuna elimu na uzushi huku dunia wa kiwango cha kutisha. Ndio maana naelewa kwanini Kanisa Katoliki limewekeza kwenye elimu kubwa kwa mtu kuwa Padre! Miaka kumi ya kumuimarisha na dunia hii ili aweze kutetea imani kikamilifu kwenye kila eneo!

Hii ya kuwa mchungaji within 3 month labda kukemea mapepo tu lakini kuna issues ukikutana na atheists, wana science au historia deep wanakutoa kwenye reli. Kadri werevu wa wana wa nyoka unavyopaa lazima muwe na watumishi walioiva kila eneo kujibu kila hoja inayochomekwa kwa werevu kuharibu Kanisa na mafundisho yake. Kwavile elimu ipo hapo dawa ni shule usitegemee Roho Mtakatifu atakufunulia vitu ambavyo alishafunua na mitaala ipo!
 
Ungejiuliza kwanza Wwe hiyo Akili yako

,Ukristo wa Leo umewagawanya Watu na Kuwafamya Wawe na Chuki Kati Yao ,Mkatoliki hawawezi kuoana na Msabato, Msabato hataki kuolewa na Anglicana.

Mmegawanyika Hamna Umoja Wowote ule maana Mnasimamia Kitu kisicho na Ukweli ndani yake.
Hilo siyo tatizo hata uislamu umegawanyika kiasi cha msuni kumuua mshia akiamini ni mpagani hana dini.
 
Kuna elimu na uzushi huku dunia wa kiwango cha kutisha. Ndio maana naelewa kwanini Kanisa Katoliki limewekeza kwenye elimu kubwa kwa mtu kuwa Padre! Miaka kumi ya kumuimarisha na dunia hii ili aweze kutetea imani kikamilifu kwenye kila eneo!

Hii ya kuwa mchungaji within 3 month labda kukemea mapepo tu lakini kuna issues ukikutana na atheists, wana science au historia deep wanakutoa kwenye reli. Kadri werevu wa wana wa nyoka unavyopaa lazima muwe na watumishi walioiva kujibu kila hoja inayochomekwa kwa werevu kuharibu Kanisa na mafundisho yake.
Hujaijua Mission yao tu. Angalia walivyowekeza ndio utajua. Si kwa ajili ya Mungu bali wao wenyewe
Hilo siyo tatizo hata uislamu umegawanyika kiasi cha msuni kumuua mshia akiamini ni mpagani hana dini.
Ndio mjue kwamba kuna Tatizo hapo, si kwamba Tatizo halipo. Mungu hawezi kuabudiwa katika Dini Yeyote ile na Nyie muuane kwa mapanga kwa Ajili yake Yeye. Mungu mwenye vyote hayupo katika Dini. Dini ni mifumo ya Viumbe kuabudiwa
 
Hujaijua Mission yao tu. Angalia walivyowekeza ndio utajua. Si kwa ajili ya Mungu bali wao wenyewe

Ndio mjue kwamba kuna Tatizo hapo, si kwamba Tatizo halipo. Mungu hawezi kuabudiwa katika Dini Yeyote ile na Nyie muuane kwa mapanga kwa Ajili yake Yeye. Mungu mwenye vyote hayupo katika Dini. Dini ni mifumo ya Viumbe kuabudiwa
Mungu hajawahi kuabudiwa nje ya dini. Labda hujui dini ni nini.
 
Sumeria walikuwa watu wa wapi, ni nchi gani Leo zenye asili hiyo, maandiko hayo yaliandikwa miaka mingapi KK (sio kabla ya biblia), ni lini watawala wa Rumi walipokea ukristo? Wakati huo biblia ilikuwa imeandikwa au bado?
 
Back
Top Bottom