ward41
JF-Expert Member
- Apr 3, 2022
- 397
- 1,394
Kuna propaganda kubwa sana wa Africa IPO miongoni. Tumeaminishwa kwamba utajiri wa marekani unatokana na wizi wa madini Africa bila kujua kwamba marekani kuna kila aina ya malighafi.
Wengi wetu ukitaja maziwa makuu, atakwambia ziwa Victoria, Tanganyika, Nyasa. Tumedanganywa sana. Maziwa makubwa duniani ya napatikana nchini Marekani.
Haya maziwa ni Michigan, Ontario, superior, Huron na Erie. Haya maziwa ni makubwa kuliko Victoria, Tanganyika na Nyassa.
Cha ajabu haya maziwa yameunganishwa na mfumo wa mifereji (plates) . Yaani meli inaweza kusafiri kutoka ziwa Victoria hadi Tanganyika hapa katikati wakachimba mifereji na kujaza maji na ikaendelea na safari hadi ziwa nyasa kwa njia hiyo hiyo. Wanachifanya ni kwamba pakiwa mlima, meli inaingia, kwenye kitu kama tenki, alafu maji Yanajazwa hadi wanafika kwenye sehemu tambalare ambako kunakuwa na Mfereji.
Kwa hiyo meli husafiri kwa njia hiyo kutoka sehemu moja Hadi sehemu Nyingine. Kwenye ubunifu kama huu, kwanini wasipate Maendeleo. Kuna mengi Sana ya kunifunza kuto USA kuliko kubisha tu. Hawa jamaa wanastahili hayo Maendeleo. Ni wabunifu Sana