Je, una ndoto za kusoma nje ya nchi hususan Sweden? Niulize swali nitakujibu ninachokifahamu

Vipi kuhusu PhD positions, nahitaji kuomba this year nipe mwongozo.
PhD mara nyingi nimeona huwa wanatangaza kupitia Chuo husika. Unaomba kama kazi kabisa. Kwahiyo unatakiwa ujue chuo gani kinaendana na unachohitaji kusoma kisha unakuwa unatupia jicho kwenye website yao mara kwa mara. Ningeweka hapa link ya list za vyuo sema toka jana nashindwa kuweka link kwa simu sijui shida ni nini.
 
Mkuu huko kuna konyagi na nyama choma ya mbuzi
Vilevi vipo ila sina uhakika kuhusu Konyagi. Nyama za kuchoma pia zipo ila mara nyingi mnakutana mnachoma wenyewe. Wenye nchi yao wanaita "Barbecue ".
 
Ndio Mkuu inawezekana. Naomba univumilie nikitumia computer nitaweka list ya vyuo na programs zote. Tena ukiwa kwenye NGO ndio safi kabisa.
 
Ha ha haa. Swali gumu kidogo Mkuu.
 
Hivi hizi scholarship zina age limit kama bado uko working age?

Mfano ukiwa na 35 to 40 unaweza pata hizi full funded scholarship?
 
Hivi hizi scholarship zina age limit kama bado uko working age?

Mfano ukiwa na 35 to 40 unaweza pata hizi full funded scholarship?
Scholarship ya Sweden haina age limit.

Inaitwa "Swedish Institute Scholarship for Global Professionals".

Sifa kubwa uwe na experience ya kazi angalau kuanzia 3 years.
 
Vip kuhusiana na GPA wanataka GPA kuanzia ngapi.
Hakuna GPA requirement kwenye criteria za kupata Scholarship. Vyeti unaambatanisha tu wakati wa kuomba admission. Kwenye upande wa Scholarship wanachozingatia zaidi ni jinsi unavyojibu maswali yaliyoulizwa, work and leadership experiences.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…