Jenerali Ulimwengu; Jk anakwenda nje ya nchi kufanya 'shopping za kipuuzi' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jenerali Ulimwengu; Jk anakwenda nje ya nchi kufanya 'shopping za kipuuzi'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbaga Michael, Jun 20, 2012.

 1. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,911
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  KATIKA toleo Na. 215 la Raia Mwema, Jenerali Ulimwengu alitaja moja ya mapungufu ya watawala wetu Tanzania kwamba ni ile hulka yao ya kutotaka kujifunza na kuiga kutoka kwa wenzetu wa nje (Ughaibuni) wanaofanya vizuri.
  Aliandika hivi:

  "Watawala wetu ni watu wanaosafiri mno, hadi wamesababisha malalamiko kwamba hawatulii nyumbani jinsi walivyo ‘kiguru na njia'.
  Inashangaza kwamba wanakwenda Ughaibuni kila uchao lakini hawana wanachojifunza huko kuhusu jinsi wenzao walivyopiga hatua
  za haraka kujiletea maendeleo na kuzikwamua nchi zao kutoka kwenye mateso ya umasikini.

  "Wanakwenda Ughaibuni kushangaa maendeleo ya wenzetu na kufanya ‘shopping' za upuuzi wakati nchi yao inadidimia. Hawana uwezo hata wa kutazama, kuona, kuelewa na kutaka kuiga kilicho kizuri." Hivyo ndivyo alivyoandika Jenerali katika toleo hilo.

  Napenda kuuendeleza kidogo mjadala huo, na nianze kwa kuongeza kwamba; hata kile ambacho kipo chini ya uwezo wa nchi yetu kukitekeleza wenyewe wanachokiona huko Ughaibuni, hawawezi kukiiga. Kwa mfano, watawala wetu kadhaa wametembelea miji ya wenzetu kama New Delji (Green Delhi) wa India na Durban wa Afrika Kusini na wamejionea wenyewe jinsi ilivyo misafi na ya kijani lakini wameshindwa kuiga. Wameshindwa kuligeuza jiji letula Dar es Salaam lifanane angalu kidogo na miji hiyo kwa usafi na u-kijani.

  Je; hivi kweli hata usafi wa jiji letu la Dar es Salaam na kuligeuza kuwa la kijani, ni kitu kinachopaswa kusubiri ufadhili wa Wazungu? Kama hivyo ndivyo, ni nini basi tunachoweza kumudu kukifanya sisi wenyewe kwa pesa zetu wenyewe na kwa mikono yetu wenyewe?

  Lakini kinachokatisha tamaa zaidi kutoka kwa watawala wetu hawa wa zama hizi, ni kwamba wanashindwa kuiga hata kile chema kinachofanywa na majirani zetu. Mfano mzuri ni hiki kinachofanywa kila mwaka na wenzetu wa Rwanda kinachoitwa Umushyikirano.
  Kwa miaka tisa mfululizo, Rais Paul Kagame amekuwa akiitisha, kila mwaka, mkutano wa kitaifa wa kujadili Muafaka wa Taifa (National Dialogue) – mkutano ambao umepachikwa jina la Umushyikirano.

  Kila mwishoni mwa mwaka (Desemba 14 na 15) viongozi wa serikali kuu, viongozi wa serikali za mitaa, wawakilishi wa vikundi vya jumuiya za kiraia (NGOs), viongozi wa dini, wabunge, wanadiplomasia,wafanyabiashara, Wanyarwanda wanaoishi Ughaibuni nawananchi wa kawaida, hukutana kwa siku mbili kwenye ukumbi wa bunge kujadiliana utendaji kazi wa serikali ulivyokuwa kwa
  mwaka huo na kupeana mikakati kwa mwaka mpya unaofuata.

  Ni katika mikutano hiyo ya Umushyikirano ambako miafaka ya kitaifa hufikiwa katika masuala mbalimbali nyeti yanayoigusa nchi. Kwa ufupi, Umushyikirano ni mikutano ya kila mwaka inayojadili mustakabali wa taifa la Rwanda. Nimekuwa nikiifuatilia mikutano hii kwa miaka mitatu iliyopita ukiwemo wa wiki iliyopita, na lazima nikiri kwamba imenisisimua. Kwangu mimi, ni moja ya vitu vyema vilivyobuniwa na Rais Paul Kagame ambavyo kama vitaendelezwa, vitaiwezesha nchi hiyo kupiga kasi ya maendeleo kuliko
  tunayoishuhudia sasa.

  Kinachonisisimua zaidi kuhusu Umushyikirano ni namna mikutano hiyo inavyoendeshwa. Inaendeshwa kwa uwazi mkubwa. Mbali ya mikutano hiyo kuwa live kwenye televisheni na redio, mijadala yake pia huwekwa kwenye tovuti. Isitoshe, hata walen Wanyarwanda ambao hawakubahatika kuhudhuria wenyewe mikutano hiyo mjini Kigali, hupewa fursa ya kuchangia maoni yao au hata kuuliza maswali kupitia njia za simu za moja kwa moja na hata kwa njia za sms na twitter.

  Kwa uelewa wangu (naomba kusahihishwa kama nakosea), hakuna nchi yoyote ya Kiafrika yenye mkutano wa kila mwaka wa National Dialogue wenye ushiriki mpana na unaoendeshwa kwa uwazi kama huo wa Rwanda. Na bado wako watu wanaomwita Rais Kagame "dikteta mkubwa" (mimi nasema kama ni dikteta, basi, ni ‘dikteta poa' – benevolent dictator). Japo wanakiri kwamba Kagame
  ameiletea Rwanda maendeleo ya kasi, haraka haraka wanaongeza:"lakini anabana uhuru wa kujieleza na ni mvunjaji mkubwa wa haki za binadamu."

  Mimi sidhani kama kuna dikteta mkubwa popote pale duniani anayeitisha mikutano ya mijadala ya kitaifa mithili ya huu wa kila
  mwishoni mwa mwaka wa Rais Kagame unaoitwa Umushyikirano ambao kila mwananchi ana haki ya kutema cheche zake, kuuliza lolote au kuchangia lolote! Kama yupo dikteta wa namna hiyo, niambieni ni nani na ni wa nchi gani.

  Kwa sababu ya uwazi huo wa mikutano hiyo ya Kagame yaUmushyikirano, hata mimi niliye Dar es Salaam (na ambaye si Mnyarwanda) nimeweza kuifuatilia kwa miaka mitatu iliyopita, na naweza kuwam shuhuda wa baadhi ya matunda ya mikutano hiyo. Kwa mfano, katika mkutano wa Desemba mwaka jana, washiriki wengi ukumbini na hata waliopiga simu, waliishutumu Serikali ya Rais Kagame kwa kushindwa kuifanikisha haraka kampeni ya ujenzi wa nyumba bora za kuishi kote nchini.

  Kwa hakika, mjadala wa mwaka jana ulitawaliwa na utekelezaji wa programu hiyo ya serikali ya kujenga nyumba bora kwa wananchi na kutokomeza nyumba za udongo (nyakatsi) kote nchini Rwanda.

  Viongozi wa ngazi za chini walilaumiwa sana kwa kuvurunda programu hiyo. Baada ya majadiliano makubwa, mkutano huo wa Umushyikirano ulikubaliana kwamba watakaozembea kwenye programu hiyo kwa mwaka 2011 watawajibishwa. Matokeo yake ni kwamba katika mkutano wa mwaka huu, uliofanyika wiki iliyopita, shutuma zilikuwa chache.

  Washiriki wengi walieleza kuridhishwa na programu hiyo ya kuteketeza nyumba za udongo nchini humo kwa kujenga za kisasa. Wenyewe wanakiri kwamba programu hiyo sasa imefanikiwa kwa asilimia 98! Hiyo maana yake ni nini? Hiyo maana yake ni kwamba muda si mrefu nyumba za udongo katika Rwanda zitakuwa ni historia. Hebu tulitafakari jambo hili kwa undani kidogo. Ni hivi; wenzetu Rwanda, kwa kupitia mkutano huo wa Umushyikirano, walifikia mwafaka wa kitaifa kwamba nyumba za udongo (nyakatsi) katika Rwanda ziwe historia ndani ya miaka mitano.

  Baada ya mwafaka huo wa kitaifa, wote wakaanza kuchapakazi kwa pamoja kuitimiza ndoto hiyo, na kila mwaka wamekuwa wakikutana (kupitia Umushyikirano) kufanya tathmini. Wamesutana na kunyoosheana vidole kwa wale waliovurunda lakini pia
  wamepongezana na kutiana moyo kwa wale waliofanya vizuri. Matokeo yake ni kwamba mafanikio kwa mwaka huu wa 2011 unaoelekea ukingoni, yamekuwa asilimia 98! Hiyo maana yake ni kwamba, muda si mrefu nyumba za udongo za nyakatsi zitakuwa historia katika Rwanda.

  Je; ni lini nasi nyumba za udongo katika Tanzania zitakuwa historia? Si tu kwamba hatuna programu ya kuzitokomeza hapa nchini, lakini hata wazo tu la kuwanayo programu ya namna hiyo halipo! Najua wapo watakaodai kwamba Rwanda ni ka-nchi kadogo kenye watu wachache, na hivyo ni rahisi kutekeleza programu ya namna hiyo. Hiyo ni kweli – Rwanda ni ka-nchi kadogo kenye watu wachache ikilinganishwa na Tanzania, lakini pia ni kweli kwamba ka-nchi hako kadogo hakana utajiri mkubwa wa maliasili ambao Tanzania imejaliwa nao.

  Kwa maneno mengine; kama tungekuwa na viongozi wa aina ya Kagame, hakika tungeweza kuutumia utajiri huo mkubwa wa maliasili tulionao kutokomeza zile tembe za Wagogo kule Dodoma au za Wasukuma kule Shinyanga au hata zile nyumba za msonge kule Upareni! Ndugu zangu, nimetoa mfano mmoja tu wa kutokomezwa nyumba za nyakatsi kama moja ya matunda ya mikutano hiyo ya Umushyikirano ya mijadala ya kitaifa yenye lengo la kufikia miafaka ya kitaifa katika masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa Taifa la Rwanda, lakini naamini ipo mifano mingi tu mingine ya mafanikio. Tukirejea hapa nyumbani kwetu, je; hatuwezi nasi kuiga jambo hilo jema la Rwanda?

  Kama Umishyikirano imeisaidia Rwanda kuharakisha maendeleo yao, kwanini isitusaidie pia sisi? Kwanini tusiianzishe mikutano ya namna hiyo na kuitafutia jina letu ili nasi ituwezeshe kufikia miafaka ya kitaifa kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo yetu?

  Nauliza hivyo; maana, kwa hali ilivyo sasa hapa nchini mwetu, hatuna National Dialogue. Siku zote tunasikiliza tu kutoka kwa
  watawala wetu na si kujadiliana nao. Ni lini nasi watatusikiliza na kujadiliana nasi kuhusu mustakabali wa Taifa letu? Afadhali zama za Nyerere; kwani mara moja moja alikuwa akienda pale UDSM, ukumbi wa Nkrumah, kukutana na wasomi wetu na kujadiliana nao kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. Siku hizi si tu kwamba watawala wetu wanakwepa majadiliano ya moja kwa moja na wasomi, lakini hata mikutano tu na waandishi wa habari wanaikwepa?

  Siku hizi wakubwa wetu wakiwa na jambo zito la kitaifa, hawataki mjadala au ushauri wa mtu yeyote nje ya dola. Watawaita wazee (wa CCM) pale Diamond Jubilee au ukumbi wa PTA na
  kuwahutubia au kuwaeleza msimamo wao (wa serikali yao) kuhusu jambo hilo. Wazee hao wa CCM ‘wakishahutubiwa', watapiga
  makofi na kushangilia; hata kama hawakukielewa vyema hicho alichozungumza bwana mkubwa kinachohusu mustakabali wa taifa letu sote.

  Staili hii hovyo ya uongozi ni ile wanayoiita kwa kimombo "top down"; yaani kila kitu kinatoka juu kwa wakubwa kwenda chinikwa wananchi. Kwa maneno mengine, wa chini ni wapokeaji tu wa amri na maelekezo! Nihitimishe safu yangu hivi: Watawala wetu wanajigamba kwamba katika miaka 50 ya Uhuru, wamethubutu. Kama kweli wanathubutu, nawasihi basi wathubutu pia kujifunza
  somo la Umushyikirano kutoka kwa jirani yetu, Rais Paul Kagame wa Rwanda.

  Binafsi, naamini ni somo maridadi linaloweza kutusaidia.Kwangu mimi; mikutano ya kila mwaka kama hiyo ya Rwanda yenye ushiriki mpana, na yenye kujadili na kufikia miafaka yakitaifa kuhusu masuala mbalimbali, ni matumizi mazuri ya fedha za walipakodi kuliko mikutano ile ya Rais Kikwete kama ule wa Sullivan.

  Tafakari.
   
 2. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kweli bwana mi nakuunga mkono mleta thread na hoja hizo hapo juu.. Na NINAMUUNGA JENERALI ULIMWENGU YUKO SAHIHI KABISA..
   
 3. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  We have said time and again!! The President had difficulty with Father Figure in his early life! Something somewhere compromised it ... Don't have to count this ..it will express itself at national level in several times!! The National is in void of real bold character, Father Quality!! ... and without that TOUGH LOVE QUALITY ... what do we have!!!?
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Yaani hawana tofauti na mwanakijiji wa kule Kimbiji ambaye ata City Centre hajawai fika!
   
 5. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  maziwa ya kunywa yanapatikana mitaani kwenye mashine za kisasa nchini rwanda....sisi bar kila hatua
   
 6. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #6
  Jun 20, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Hii imenikumbusha maneno ya Madame Speaker Makinda leo mapema alikuwa anawahusia Wabunge kuepukana na kuonyeshana nani ni Mwanasiasa bora na kutoleana lugha chafu na badala yake waangalie Budget iliyoko mezani na kubwa ni hitaji la kuwa na dialogue, since then hili neno la dialogue limestick kichwani kwangu. Uliyoyasema yana mantiki kubwa.........mimi nashangaa tunashindwa kuwa na dialogue hata katika ngazi za mitaa ije kuwa kitaifa, mfano recently kuna habari nilisikia Wananchi wa mtaa {sikumbuki jina} Mabibo walivuruga ujenzi wa ofisi ya Serikali ya mtaa kwasababu ulifanyika bila ya kuwashirikisha na pia Ujenzi huo ulipelekea kukatwa kwa mabomba ya maji na hivyo kuwafanya kufata maji mbali. Sasa hapa ni kwa kujiuliza kama hali imefikia hivi kusema kweli ni mbaya sana pale Mwenyekiti anapojiona Mungu mtu je huyo Rais wetu ndio yukoje.............seriously we lack leadership
   
 7. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,731
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  They can learn....but only can learn bad things.

  CCM ni janga kubwa kuliko maradhi yote kwa pamoja. Kwao (ccm) umaskini, maradhi na ujinga ni mitaji hivyo wanaviongeza kila kona kila iitwapo leo.

  I had some Rwandese neighbors and they were keenly participating to their last national conevention/dialogue. They feels and owns it dearly. Good point Mh. Ulimwengu, thank you mleta mada.
   
 8. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,688
  Likes Received: 12,725
  Trophy Points: 280
  Jk kwa kusafiri utamtaka,picha na beckham yan ndio mambo anayo jua tu.
   
 9. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #9
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,911
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  Ahsante ni taifa letu vwema kuweka mipango mizuri yenye manufaa.
   
 10. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #10
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,911
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  na muda wote ziko wazi, yani inamanisha watu wapo hawafanyi kazi.
   
 11. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,492
  Likes Received: 2,738
  Trophy Points: 280
  Labda huwa anakwenda kushangaa pia!!!! Ndiyo maana huwa tunaambiwa kuwa Mwanza itajengwa kama Calfornia na Kigoma kama Dubai ndani ya miaka 5!! Ndoto za Arinacha!! Tatizo inawezekana kabisa wenzetu huwa wanafikiria kuwa hayo maendeleo waliyonayo wenzetu wameshushiwa na Mungu!!
   
 12. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,795
  Likes Received: 2,564
  Trophy Points: 280
  Nadhani mzee yupo Brazil attending rio+20 conference. Tulie tu.
   
 13. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,377
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Naunga mkono hoja 100%!
  Mkuu umemaliza kila kitu tatizo
  ccm hawashauriki na wala si wasikivu!
  Humu kuna viongozi kibao lakini wanajifanya hawaoni kabisaa!
  Sasa huu sio udhaifu???
   
 14. ERIC JOSEPH

  ERIC JOSEPH JF-Expert Member

  #14
  Jun 20, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nakupongeza kwa mawazo yako mazuri ya kunuru nchi na janga la umasikini na kupunguza matabaka kati ya wenye nacho na wasionacho mana tunakoelekea sio kuzuri.asante na mpango wako wa kupunguza matatizo ktk nchi yetu.tatizo viongoz wetu Picha hawaioni ina mana hata kusoma alama za nyakati thawasomi
   
Loading...