Heaven Seeker
JF-Expert Member
- May 12, 2017
- 478
- 1,046
Amani iwe nanyi Wakuu,
Maisha ya sasa imekuwa adimu binadamu kumtendea wema binadamu mwingine. Imekuwa ni nadra sana kumsaidia mtu mwingine hata tu kwa mawazo. Yaani wivu, utapeli, chuki na mambo mengine mabaya yanayofanana na hayo imekuwa ndio sehemu ya walio wengi. Imekuwa ngumu zaidi kupeana "michongo" ya hapa na pale.
Namshukuru Mungu, hata kabla sijafika Ulaya nikiwa home kwetu huko kijijini ndanindani ñilitamani siku moja Dunia iwe sehemu ya kukaliwa na watu wenye Tabia njema, wenye kuaminiana na kupendana. Hasahasa kupeana michongo ama kuhabarishana kuhusu mambo kadha wa kadha. Msukumo wa mambo haya upo ndani yangu, na ninafurahia kuwatendea mema binadamu wengine siku zote. Wakifanikiwa ndio furaha yangu.
Huko nyuma nimewahi kuleta uzi wa kutoa taarifa kwa wahitaji kuhusu fursa ya kimasomo Sweden hasahasa Scholarship ktk level ya Masters. Ni matuamaini yangu kuwa nilijitahidi kujibu maswali kadri yalivyoulizwa.
Ila si mbaya siku ya leo tena nikakumbushia jambo lilelile; ama huenda unahitaji kujua wenzetu Ulaya wanaishije. Nimeishi Sweden kwa miaka miwili sasa. Nilibahatika kufika kutokana na Scholarship niliyoipata mwaka 2019.
Kwa sasa nimehitimu salama masomo yangu. Na sasa nina muda mzuri wa kujibu maswali ya wadau hapa jukwaaani. Nitatumia uzoefu na uelewa wangu wa machache niliyonayo kujibu maswali endapo yatajitokeza.
Kama ilivyo ada; sihitaji kulipwa wala kujipatia faida binafsi kwa kuanzisha uzi huu. Naomba maswali yaulizwe hapahapa na nitajitahidi kuyajibu. Niwe muwazi kuwa maswali "personal" ni ridhaa yangu kuyajibu ama kuyaacha. Hivyo ukiuliza swali lenye nature hiyo na usipate majibu naomba unielewe.
Zaidi ya yote, sihitaji kuulizwa au kufuatwa inbox(PM). Naomba niulizwe hapahapa. Wala sihitaji kubadilishana contacts na mtu yeyote. Ikitokea hivyo basi ni nadra sana! Karibuni Wakuu!