Je, ulipata kujua mwaka ambao Ulimwengu ulimjua rasmi Yesu kuwa ndiye Masihi aliyetabiriwa?

joex

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
787
640
Ukisoma Luka 3:1 inatambulisha kuwa katika mwaka wa 15 wa Roman Emperor Tiberius Caesar (Kaisari Tiberius).

Halafu ukienda chini kwenye hiyo Sura ya 3 unakuta masimulizi ya Yesu Kubatizwa katika Mto Yordan na Yohana. Na kwakweli, kwakuwa Wayahudi walikuwa wakiujua unabii mwingine wa Daniel kuhusiana na kuja kwa Mesiha, katika Luka 3:15 walikuwa wakitarsjia tukio hilo la kufunuliwa kwa Masiha litokee siku hiyo.

Unabii wa Daniel ninaouzungumzia ni ule wa Majuma 70, ambapo katika Dan 9:25 inasema " Tangu kutolewa kwa lile neno la kujenga upya Jerusalem mpaka ATAKAPOTOKEA MESIHA.

Sasa ukirudi kwenye historia tuliyosoma shule, na ukitafuta kwenye google, unapata kuona kuwa Kaisari Tiberius alianza kutawala mwaka wa 14 AD. Hivyo, mwaka wake wa 15 wa utawala wake unaangukia mwaka wa 29 AD. Huo ndio mwaka Yesu alibatizwa na rasmi kuwa masihi.

NB: Baada ya kupanda kutokea majini watu wote walisikia sauti ya Mungu na Roho Mtakatifu ikishuka juu yake. Sauti ilisema "Wewe ni mwanangu mpendwa nimekukubali. Aidha, rejea pia Dan 9:25 ilivyosema.
Kumbe, mwaka huu unaokaribia wa 2029 ni mwaka muhimu sana Kwetu wanadamu Kwakuwa italuwa inatimia miaka 2,000 tangu Yesu alipotambulishwa rasmi kuwa Masihi.

Unakumbuka Dunia yote ilivyoingia chaka wakati ulipokaribia na kufika mwaka wa 2,000? Mwenye akili na atambue

Screenshot_20230428-093953.png
 
Bado,
Mbona Wengine wanamwita Mungu,?
Ulimwengu bado hauja mjua Yesu ni Masihi wala Hauja jua Mungu
 
Unamaanisha nini? Kwamba Yesu anarudi tena mwaka 2029?. Yawezekana! Lakini kuna ishara mbona bado hazijatimia ingawa zinaelekea kutimia?, Ishara ya Ezekiel war(Russia, Iran, Turkey, Kush V. Israel), pia EU na NATO kuwa Wapinga Kristo(666)?.
 
Bado,
Mbona Wengine wanamwita Mungu,?
Ulimwengu bado hauja mjua Yesu ni Masihi wala Hauja jua Mungu
Yesu ni Mungu

Aliwahi watandika swali WAYAHUDI kuhusu Uungu wake ,watapoteana

Alikuwa anawapiga kwa Maandiko TU

Luka 20:41-47 BHN

Yesu akawauliza, “Yasemekanaje kwamba Kristo ni mwana wa Daudi? Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi: ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia mpaka niwaweke maadui zako kuwa kiti cha kuwekea miguu yako.’ Ikiwa Daudi anamwita yeye, ‘Bwana,’ basi, atakuwaje mwanawe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo anayesema Yesu akawauliza ni nani?
 
KAKA NI MWANA WA MUNGU.
 
Back
Top Bottom