Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,205
- 5,332
Biblia ina andiko la wakati Mungu akimpa Adam mamlaka ya dunia, Adam anashindwa kuitii amri ya Mungu na hatimaye anaishia kumkabidhi mamlaka hayo shetani.
Quran inasema "isipokuwa kwa wajakazi (wafuasi) wangu (shetani) hauna mamlaka yeyote juu yao, isipokuwa kwa wale wanaokufuata(wanaokutii)
Tunaona katika vitabu hivi viwili vya imani kuwa shetani amepewa mamlaka juu ya watu wa Mungu kwa sababu ya dhambi.
Je, maandiko yanasemaje kuhusiana na Mungu kuwa ndiye mmliki au mtawala wa ulimwengu huu.
Yesu anasema "mamlaka yote nimekabidhiwa mimi, mbinguni na duniani" mathayo 28:18
Katika sala ya Bwana ndani ya mathayo 6:13 inaishilia na mstari huu "...kwa kuwa ufalme ni wako na nguvu na utukufu, milele, amina! (Andiko hili limewekwa kwenye mabano katika toleo la biblia ya NASB na limeondolewa katika NIV, RSV na ESV)
Waefeso 1:20-22 inasema "Akamwinua kutoka katika mauti na akamweka mkono wa kulia.....na akaweka kila kitu chini ya miguu yake"
Daniel 4:17, 25, 26, mara tatu inatuambia "Aliye juu zaidi uongoza ufalme wa binadamu na umpa yeyote amtakaye"
2 wakolosai 20:6 inathibitisha "Ewe Mwenyezi Mungu wa baba zetu, je siye Mungu wa mbinguni? Na utawalaye falme zote hata za wapagani? Na katika mkono wako je hakuna nguvu na uwezo, kiasi hakuna hawezae kuhimili?"
Je, maandiko yanasemaje kuhusiana na Shetani kuwa mtawala au mmliki wa ulimwengu huu?
Luka 4:6, Shetani akamjaribu Bwana Yesu jangwani, shetani akamwambia Yesu kuwa ufalme wote wa duniani ni wangu na nampa yeyote yule nimtakaye. (Kumbuka kauli hii ni kinyume na Daniel 4:17,25,26)
Mathayo 4:4 shetani akaahidi kumpa kristo utawala wa dunia kama zawadi ya kumwinamia na kumwabudu.
Tuangalie katika matoleo kadhaa ya biblia tukianza na NIV "Dunia iko chini ya utawala wa mwovu"
Warumi 12:9, NKJV, NASB katika mathayo 5:37 na 6:13, Holman standard, ESV (vitabu vyote vinathibitisha kuwa shetani ndiye "Mtawala wa ulimwengu" Yohana 12:31,14:30 na 16:11)
Yohana 14:30 Sitosema tena mengi nanyi kwa sababu mtawala wa dunia hii anakuja. Yeye hana uwezo juu yangu.
Yohana 12:31-33 "Wakati wa Mungu kutamka hukumu juu ya ulimwengu imetimia, huu ni wakati ambao shetani, MTAWALA WA DUNIA hii, 'ATAPINDULIWA' nami nitakapoinuliwa kutoka ardhini nitawavuta watu wote waje kwangu.
Waefeso 2:1-3 Ninyi mlikuwa mmekufa kwa sababu ya dhambi zenu. Na hata sisi sote tulikuwa kama wao;tuliishi kufuatana na mtindo mbaya wa ulimwengu huu, MKAMTII MTAWALA WA PEPO WENYE NGUVU WA ANGA, pepo ambao hutawala sasa watu wasiomtii Mungu. Na hata sisi sote tulikuwa kama wao;tuliishi kufuatana na tamaa zetu za kidunia na kufanya mambo yale yaliyo ipendeza miili na akili zetu ila dunia, sisi kama vile pia wao, tulistahili ghadhabu ya Mungu.
Waefeso 6:12-13 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya WAKUU WA GIZA NA MAJESHI YA PEPO WABAYA katika ulimwengu wa kiroho.
Tunaona pia kuwa hata malaika mkuu Mikaeli mamlaka yake haizidi ile ya shetani, Yuda 1:9 kwamba hata ' Mikaeli malaika mkuu, katika ule ubishi na ibilisi juu ya mwili wa musa, Mikaeli akuthubutu kumshitaki kwa kumlahumu bali alisema, Bwana na akukemee.
Yesu mwenyewe alimwita shetani 'mtawala wa ulimwengu' Yohana 16:11
Ni wazi kuwa kulingana na maandiko haya, shetani ana mamlaka katika dunia. Na mifumo ya ulimwengu mzima inaendeshwa kulingana na design alizoamua. (Angalia tena, waefeso 2:2)
Ndiyo maana wenye kuiamini hekima toka kwa Mungu wanaonekana kama wajinga na waliopotoka kwa sababu mtizamo wao ni tofauti kabisa na hekima ya kiulimwengu. (1wakorintho 1:21-25)
Shetani utawala juu ya mifumo ya ulimwengu na Biblia inathibitisha hili kwa kukazia "Je hamtambui kuwa rafiki wa dunia ni adui wa Mungu? Yeyote atakaye kuwa rafiki wa dunia ujifanisha mwenyewe kuwa adui wa Mungu (James 4:4)(1 Yohana 2:15) inaamuru" usipende ulimwengu au vitu vyake, endapo mtu atapenda ulimwengu, upendo wa baba hautokuwa nae; kwa sababu adui wa Mungu ni MTAWALA WA ULIMWENGU.
Kama haitoshi katika Quran shetani kuonesha mamlaka na uwezo wake anamwakikishia Allah kuwa "Nitawaendea uso kwa uso, na kwa kutokea nyuma, na kutokea kulia na kwa kutokea kushoto" (I shall approach them head on and from behind and from the right and from the left)
Kulingana na ushahidi wa maandiko matakatifu hayo hapo juu yamhusuyo Mungu na Shetani toka katika pande zote mbili,
1. Wewe kama mwamuzi, toa jibu lako na sababu kuwa nani ni mtawala halisi wa ulimwengu huu?
2. Ikiwa unadhani shetani ndiye mtawala wa ulimwengu, Je ni haki kuishi kinyume nae kwa kutii amri za mamlaka nyingine?
3. Ikiwa unadhani Mungu ndiye mtawala wa ulimwengu, Je ni haki kuendelea kumshtumu shetani aliye ndani ya mamlaka yake?