Kwa vita hivi ulimwengu utamjua Yesu ni nani!

prince john john

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
2,080
3,106
Sasa ulimwengu utamjua Yesu ni nani. Lakini vita hivi ni fursa ya Ukristo kuzishinda dini zingine. Laiti tungelimakinika na fursa hii!
Waliokuwa wanamkataa Yesu watamjua Yesu sasa.

Nadhani tangu hivi karibuni, kila dakika kumi Mungu anapokea roho ya marehemu fulani, mhinga wa vita. Ikija roho ya mtoto, inakuja roho ya mtu mzima. Ikija roho ya kijana, inakuja roho ya mzee. Ikija roho ya mrefu, inakuja roho ya mfupi. Ikija roho ya mnene, inakuja roho ya mwembamba. Ikija roho ya mweusi, inakuja roho ya mweupe na kadhalika. Wote hao wahinga wa vita. Vita vinatafuna uhai. Kuna vita Nigeria. Kuna vita Somalia. Kuna vita Kongo. Kuna vita Msumbiji. Kuna vita Ukraine na kiboko cha vita vyote hivyo ni vita ya Palestina. Huko Gaza tunaweza kufikiria kupanda viazi vitamu au viazi mviringo kwa jinsi vifusi vinavyozidi kulundikana.

Kifupi, hakutakuwa na taabu ya kupanga matuta tutakapoanza upanzi wetu.

Yote haya ni kwa nini? Ni kwa sababu kuna chuki. Kuna chuki majumbani. Kuna chuki vitongojini. Kuna chuki kati ya dini. Kuna chuki kati ya nchi. Kuna chuki kati ya Waafrika. Kuna chuki kati ya Wasemiti. Kuna chuki kati ya watu weupe na kadhalika. Wanadamu wanachukiana. Hawataki kusikilizana na kupatana. Hawataki kumaliza tofauti zao kwa amani. Watu wanajinasibu kwa maneno na maandishi tu kuwa ni watu wa dini za amani wakati ukweli si hivyo. Zilongwa mbali, zitendwa mbali. Sijui anadanganywa nani?

Kutoka Kukong’otana hadi Msamaha
Kuna safari aliyotufanyiza Yesu ambayo wengine hawana muda wa kuisikiliza ikisimuliwa. Kwa kuwa hatutaki kumsikiliza Yesu, tutasadikishwa na maafa makubwa. Lakini ajabu ni kwamba kenge hasikii hadi atoke damu puani! Ni hivi kuna safari kutoka kwa mtu aliyekuwa anaitwa Mfalme Hammurabi, hadi Torati hadi Yesu Kristo. Nisikilizeni na mniamini.

Enzi za Hammurabi – Kukong’otana
Mosi ni enzi za Hammurabi. Enzi zile za miaka 1750 K.K., kabla ya kuanzishwa kwa Dini ya Kiyahudi, mfalme mmoja aliyeitwa Hammurabi wa huko Mashariki ya Kati, alipendekeza dawa ya kumaliza magomvi kati ya watu kuwa ni kukong’otana kwa vipigo vya mbwa, yaani kupiga mpaka mtu akome kwa kupigwa. Yaani kwamba mkosefu akong’otwe kupita kile alichotenda. Yaani, kwa mfano, yaya akimdondosha mtoto, yaya huyo anyongwe kusudi akome na wengine wote watakaosikia habari hiyo wasithubutu hata siku moja kuwadondosha watoto wa watu.

Mintarafu mauaji, Hammurabi alipendekeza mtu akimuua mtu mmoja, alipwe kwa kuuawa na kwa mtu mmoja aliyemuua wauawe jamaa zake sabini – mmoja kwa sabini. Amri za Hammurabi hazikumaliza uovu wowote duniani.

Enzi za Torati – Malipo Sawa kwa Sawa
Baada ya enzi za Hammurabi ikaja enzi ya pili. Mnamo mwaka 1250 K.K. iliingia Torati. Wayahudi walishangilia sana maana Torati ilitaka mkosefu asilipwe zaidi ya kile alichokosea isipokuwa alipe sawa sawa kabisa na kile alichofanya.

Wayahudi waliiona enzi hii kuwa enzi za haki sana. Kisasi kikahesabiwa kuwa haki ya mtu, enzi ya kulipana sawa kwa sawa. Yaani kwa mfano, kama mtu alimtoboa mwenzake jicho la kushoto, na yeye aletwe mahakamani na atobolewe jicho la kushoto vile vile.

Kama mtu alimvunja mwenzake mkono wa kulia karibu na kiwiko, na yeye aletwe mahakamani avunjwe mkono wa kulia karibu na kiwiko vile vile. Kama mtu alimvunja mwenzake mguu wa kushoto karibu na nyonga, na yeye aletwe mahakamani avunjwe mguu wa kushoto karibu na nyonga. Kama mtu alimuua mtu fulani na yeye aletwe mahakamani kisha auawe vile vile.

Hii ndiyo ilikuwa kanuni ya jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu, kuteketeza kwa kuteketeza (moto kwa moto), jereha kwa jeraha, chubuko kwa chubuko na uhai kwa uhai. Kwa Kiingereza kanuni hii huitwa “tit for tat” (Kut 21:24). Kanuni hii haikumaliza uovu wowote duniani. Kauli iliyokomeshea mambo hapa ni “Moto kwa moto” badala ya “Dawa ya moto ni maji.”

Enzi za Yesu na Agano Jipya – Kupendana na Kusameheana
Mwaka 1 Mwaka wa Bwana, Yesu Kristo, Mwana wa Mungu akatujia ulimwenguni na kutufundisha mambo mengi. Katika yote akatupa amri kuu ya mapendo: “Tumpende Mungu kwa moyo wetu wote, kwa roho yetu yote na kwa akili yetu yote” na kwa upande mwingine akatuagiza tumpende jirani yetu kama tunavyojipenda wenyewe (Mt 22:37-40). Katika kumpenda Mungu alimaanisha mambo matano: kumwabudu, kusali, kuweka nadhiri au ahadi na kuzitimiza, kutoa sadaka na zaka na kufanya toba. Na katika kumpenda jirani alimaanisha mambo 14: matendo saba ya huruma kwa miili ya wenzetu na matendo saba ya huruma kwa roho za wenzetu.

Kwa matendo saba ya huruma kwa miili ya wenzetu Yesu alimaanisha: kuwalisha wenye njaa, kuwapa cha kunywa wenye kiu, kuwakaribisha wageni, kuwavika wasio na nguo, kuwatazama wagonjwa, kuwatazama wafungwa na kuwazika wafu.

Kwa matendo saba ya huruma kwa roho za wenzetu Yesu alimaanisha: kuwafundisha wajinga, kuwashauri wenye mashaka, kuwaonya wakosefu, kuvumilia magumu, kuwavumilia wasumbufu, kuwafariji wenye dhiki na kuwaombea wazima na wafu. Haya yote ndiyo yanaoitwa UKRISTO.

Ndipo yeyote anayemkubali Yesu kwa dhati anakuwa “mwana wa Mungu” kwa maana kwamba anakuwa mwana wa upendo, mtu mwenye kusamehe, mtu mwenye kuheshimu uhai wa wengine. Wakristo tunawiwa mfano mzuri hapa. Ilipasa tulipo sisi pasiwepo magomvi wala vita vyo vyote. Lakini, si mara haba, masakubimbi na malipyoto hufaulu kutuingiza hata sisi kwenye magomvi na vita. Loh! Hapo huwa tunamfedhehesha Yesu, Mungu wetu na walimu wetu mwema.

Wengine wetu huwa na maneno machafu kana kwamba wamefia samaki vinywani mwao na wengine wetu wakali na wauaji kupita mbogo.
Mintarafu kukoseana Yesu alitutaka tuache UHAMMURABI na UTORATI. Alitaka watu tusameheane 7 x 70.

Maandiko yetu Matakatifu yanabanisha haya katika Mt 18:21-35 na Rum 12:3-21. Kifupi Yesu alitaka watu tusameheane kama tunavyosamehewa na Mungu Baba yetu (Mt 6:12. Alitutaka mtu akipigwa shavu la kushoto ageuzie hata shavu la kulia na anayelazimishwa kwenda na mtu maili moja akubali kwenda hata maili mbili (Mt 5:38-42).

Tungemwelewa vyema Yesu alitaka watu tusidaiwe chochote na mtu isipokuwa upendo, tusilipe ovu kwa ovu. Kifupi alitutaka katika uovu, tusifukuzane na mwenda wazimu (Rum 12:14-21).

Kwa kutatua migogoro yetu, Yesu alitupa mchakato wake bora: kukaa na kuongea wawili yenu. Ikishindikana alisema kuwaalika mashahidi wawili watatu. Ikishindikana hapo basi ni kukaa kitako na Kanisa. Hatimaye, ikishindikana hapo basi ni kuachana pasipo kupigana, yaani kila mtu akashike hamsini zake lakini huku mkiombeana kila mtu arudi kwenye utimamu wa kufikiri vyema pamoja na kutubu (Mt 18:15-18).

Walimwengu Wanahusudu Kisasi
Ajabu lakini ni kwamba wanadamu walimkataa Yesu, wakapendelea giza kuliko mwanga (Yn 1:3-8) na mbaya zaidi wengine wakaja na dini zao za ajabu ajabu. Dini zinazomkubali kabisa Hammurabi na kuwa na visasi.

Wakacheka dawa aliyopendekeza Yesu mintarafu magomvi. Wanadamu wakamcheka Yesu na habari yake ya upendo na msamaha. Wakamwona Yesu lofa. Wakamwona Yesu hamnazo. Sawa! Dini hizo zote zikawa zinarejea kwenye UHAMMURABI yaani kwenye kanuni za kukong’otana kwa vipigo vya mbwa (visasi vikali mno) au kwenye UTORATI, yaani kulipana sawa kwa sawa, kanuni ambazo zilipwaya hapo mwanzo. Dini hizi zikawa bure kabisa. Sasa? Ndiyo maana leo hii kukong’otana ni kwingi mno. Na bado kama hatutaki kumsikiliza Yesu katika kupendana na kusameheana, tutamalizana!

Bado mpaka Wote Tumkubali Yesu
Humu barani Afrika, Ukraine na Palestina mambo moto. Kweli mpambe wa mauti ni kiburi. Msinibishe. Popote pale ukikiona kiburi kinakuja ujue mauti anafuata. Wanadamu tutamalizana mpaka akubaliwe Yesu Mwana wa Mungu na ujumbe wake wa upendo na msamaha. Kifupi, ni mpaka msamaha ni kupotezea bure tu, wala si ulofa. Watu waupokee na kuuishi Ukristo. Bila hivyo, hakuna amani ulimwenguni isipokuwa vitakuwa vita kwa mbele, yaani vita juu ya vita.

Kwa kuwa hatuitaki busara ya upendo na amani, ulimwengu utamjua Yesu ni nani, kama siyo tungali hai basi tungali tunashushwa makaburini mwetu! Hivi kumkaidi Yesu, Mungu na Mwana wa Mungu kuna faida gani kama tunakufa hivi? Mungu tunusuru na janga hili la kukataa au kuchelewa kumjua Mungu na Mwanao. Narudia na kusisitiza. Dini yenye dawa ya magomvi yetu yote ulimwenguni ni UKRISTO PEKE YAKE! Tuendelee tu kubisha tushindwe kusalimika. Hadi sasa kuna faida gani? Tunamkataa Yesu sisi na tunakufa sisi. Basi, shauri letu!

Mzee wenu Pd. Titus Amigu
 
Waliokuwa wanamkataa Yesu watamjua Yesu sasa. Nadhani tangu hivi karibuni, kila dakika kumi Mungu anapokea roho ya marehemu fulani, mhinga wa vita. Ikija roho ya mtoto, inakuja roho ya mtu mzima. Ikija roho ya kijana, inakuja roho ya mzee. Ikija roho ya mrefu, inakuja roho ya mfupi. Ikija roho ya mnene, inakuja roho ya mwembamba. Ikija roho ya mweusi, inakuja roho ya mweupe na kadhalika. Wote hao wahinga wa vita. Vita vinatafuna uhai. Kuna vita Nigeria. Kuna vita Somalia. Kuna vita Kongo. Kuna vita Msumbiji. Kuna vita Ukraine na kiboko cha vita vyote hivyo ni vita ya Palestina. Huko Gaza tunaweza kufikiria kupanda viazi vitamu au viazi mviringo kwa jinsi vifusi vinavyozidi kulundikana. Kifupi, hakutakuwa na taabu ya kupanga matuta tutakapoanza upanzi wetu.
Yote haya ni kwa nini? Ni kwa sababu kuna chuki. Kuna chuki majumbani. Kuna chuki vitongojini. Kuna chuki kati ya dini. Kuna chuki kati ya nchi. Kuna chuki kati ya Waafrika. Kuna chuki kati ya Wasemiti. Kuna chuki kati ya watu weupe na kadhalika. Wanadamu wanachukiana. Hawataki kusikilizana na kupatana. Hawataki kumaliza tofauti zao kwa amani. Watu wanajinasibu kwa maneno na maandishi tu kuwa ni watu wa dini za amani wakati ukweli si hivyo. Zilongwa mbali, zitendwa mbali. Sijui anadanganywa nani?

Kutoka Kukong’otana hadi Msamaha
Kuna safari aliyotufanyiza Yesu ambayo wengine hawana muda wa kuisikiliza ikisimuliwa. Kwa kuwa hatutaki kumsikiliza Yesu, tutasadikishwa na maafa makubwa. Lakini ajabu ni kwamba kenge hasikii hadi atoke damu puani! Ni hivi kuna safari kutoka kwa mtu aliyekuwa anaitwa Mfalme Hammurabi, hadi Torati hadi Yesu Kristo. Nisikilizeni na mniamini.

Enzi za Hammurabi – Kukong’otana
Mosi ni enzi za Hammurabi. Enzi zile za miaka 1750 K.K., kabla ya kuanzishwa kwa Dini ya Kiyahudi, mfalme mmoja aliyeitwa Hammurabi wa huko Mashariki ya Kati, alipendekeza dawa ya kumaliza magomvi kati ya watu kuwa ni kukong’otana kwa vipigo vya mbwa, yaani kupiga mpaka mtu akome kwa kupigwa. Yaani kwamba mkosefu akong’otwe kupita kile alichotenda. Yaani, kwa mfano, yaya akimdondosha mtoto, yaya huyo anyongwe kusudi akome na wengine wote watakaosikia habari hiyo wasithubutu hata siku moja kuwadondosha watoto wa watu. Mintarafu mauaji, Hammurabi alipendekeza mtu akimuua mtu mmoja, alipwe kwa kuuawa na kwa mtu mmoja aliyemuua wauawe jamaa zake sabini – mmoja kwa sabini. Amri za Hammurabi hazikumaliza uovu wowote duniani.

Enzi za Torati – Malipo Sawa kwa Sawa
Baada ya enzi za Hammurabi ikaja enzi ya pili. Mnamo mwaka 1250 K.K. iliingia Torati. Wayahudi walishangilia sana maana Torati ilitaka mkosefu asilipwe zaidi ya kile alichokosea isipokuwa alipe sawa sawa kabisa na kile alichofanya.
Wayahudi waliiona enzi hii kuwa enzi za haki sana. Kisasi kikahesabiwa kuwa haki ya mtu, enzi ya kulipana sawa kwa sawa. Yaani kwa mfano, kama mtu alimtoboa mwenzake jicho la kushoto, na yeye aletwe mahakamani na atobolewe jicho la kushoto vile vile. Kama mtu alimvunja mwenzake mkono wa kulia karibu na kiwiko, na yeye aletwe mahakamani avunjwe mkono wa kulia karibu na kiwiko vile vile. Kama mtu alimvunja mwenzake mguu wa kushoto karibu na nyonga, na yeye aletwe mahakamani avunjwe mguu wa kushoto karibu na nyonga. Kama mtu alimuua mtu fulani na yeye aletwe mahakamani kisha auawe vile vile.
Hii ndiyo ilikuwa kanuni ya jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu, kuteketeza kwa kuteketeza (moto kwa moto), jereha kwa jeraha, chubuko kwa chubuko na uhai kwa uhai. Kwa Kiingereza kanuni hii huitwa “tit for tat” (Kut 21:24). Kanuni hii haikumaliza uovu wowote duniani. Kauli iliyokomeshea mambo hapa ni “Moto kwa moto” badala ya “Dawa ya moto ni maji.”

Enzi za Yesu na Agano Jipya – Kupendana na Kusameheana
Mwaka 1 Mwaka wa Bwana, Yesu Kristo, Mwana wa Mungu akatujia ulimwenguni na kutufundisha mambo mengi. Katika yote akatupa amri kuu ya mapendo: “Tumpende Mungu kwa moyo wetu wote, kwa roho yetu yote na kwa akili yetu yote” na kwa upande mwingine akatuagiza tumpende jirani yetu kama tunavyojipenda wenyewe (Mt 22:37-40). Katika kumpenda Mungu alimaanisha mambo matano: kumwabudu, kusali, kuweka nadhiri au ahadi na kuzitimiza, kutoa sadaka na zaka na kufanya toba. Na katika kumpenda jirani alimaanisha mambo 14: matendo saba ya huruma kwa miili ya wenzetu na matendo saba ya huruma kwa roho za wenzetu.
Kwa matendo saba ya huruma kwa miili ya wenzetu Yesu alimaanisha: kuwalisha wenye njaa, kuwapa cha kunywa wenye kiu, kuwakaribisha wageni, kuwavika wasio na nguo, kuwatazama wagonjwa, kuwatazama wafungwa na kuwazika wafu.
Kwa matendo saba ya huruma kwa roho za wenzetu Yesu alimaanisha: kuwafundisha wajinga, kuwashauri wenye mashaka, kuwaonya wakosefu, kuvumilia magumu, kuwavumilia wasumbufu, kuwafariji wenye dhiki na kuwaombea wazima na wafu. Haya yote ndiyo yanaoitwa UKRISTO. Ndipo yeyote anayemkubali Yesu kwa dhati anakuwa “mwana wa Mungu” kwa maana kwamba anakuwa mwana wa upendo, mtu mwenye kusamehe, mtu mwenye kuheshimu uhai wa wengine. Wakristo tunawiwa mfano mzuri hapa. Ilipasa tulipo sisi pasiwepo magomvi wala vita vyo vyote. Lakini, si mara haba, masakubimbi na malipyoto hufaulu kutuingiza hata sisi kwenye magomvi na vita. Loh! Hapo huwa tunamfedhehesha Yesu, Mungu wetu na walimu wetu mwema. Wengine wetu huwa na maneno machafu kana kwamba wamefia samaki vinywani mwao na wengine wetu wakali na wauaji kupita mbogo.
Mintarafu kukoseana Yesu alitutaka tuache UHAMMURABI na UTORATI. Alitaka watu tusameheane 7 x 70. Maandiko yetu Matakatifu yanabanisha haya katika Mt 18:21-35 na Rum 12:3-21. Kifupi Yesu alitaka watu tusameheane kama tunavyosamehewa na Mungu Baba yetu (Mt 6:12. Alitutaka mtu akipigwa shavu la kushoto ageuzie hata shavu la kulia na anayelazimishwa kwenda na mtu maili moja akubali kwenda hata maili mbili (Mt 5:38-42). Tungemwelewa vyema Yesu alitaka watu tusidaiwe chochote na mtu isipokuwa upendo, tusilipe ovu kwa ovu. Kifupi alitutaka katika uovu, tusifukuzane na mwenda wazimu (Rum 12:14-21).
Kwa kutatua migogoro yetu, Yesu alitupa mchakato wake bora: kukaa na kuongea wawili yenu. Ikishindikana alisema kuwaalika mashahidi wawili watatu. Ikishindikana hapo basi ni kukaa kitako na Kanisa. Hatimaye, ikishindikana hapo basi ni kuachana pasipo kupigana, yaani kila mtu akashike hamsini zake lakini huku mkiombeana kila mtu arudi kwenye utimamu wa kufikiri vyema pamoja na kutubu (Mt 18:15-18).

Walimwengu Wanahusudu Kisasi
Ajabu lakini ni kwamba wanadamu walimkataa Yesu, wakapendelea giza kuliko mwanga (Yn 1:3-8) na mbaya zaidi wengine wakaja na dini zao za ajabu ajabu. Dini zinazomkubali kabisa Hammurabi na kuwa na visasi. Wakacheka dawa aliyopendekeza Yesu mintarafu magomvi. Wanadamu wakamcheka Yesu na habari yake ya upendo na msamaha. Wakamwona Yesu lofa. Wakamwona Yesu hamnazo. Sawa! Dini hizo zote zikawa zinarejea kwenye UHAMMURABI yaani kwenye kanuni za kukong’otana kwa vipigo vya mbwa (visasi vikali mno) au kwenye UTORATI, yaani kulipana sawa kwa sawa, kanuni ambazo zilipwaya hapo mwanzo. Dini hizi zikawa bure kabisa. Sasa? Ndiyo maana leo hii kukong’otana ni kwingi mno. Na bado kama hatutaki kumsikiliza Yesu katika kupendana na kusameheana, tutamalizana!

Bado mpaka Wote Tumkubali Yesu
Humu barani Afrika, Ukraine na Palestina mambo moto. Kweli mpambe wa mauti ni kiburi. Msinibishe. Popote pale ukikiona kiburi kinakuja ujue mauti anafuata. Wanadamu tutamalizana mpaka akubaliwe Yesu Mwana wa Mungu na ujumbe wake wa upendo na msamaha. Kifupi, ni mpaka msamaha ni kupotezea bure tu, wala si ulofa. Watu waupokee na kuuishi Ukristo. Bila hivyo, hakuna amani ulimwenguni isipokuwa vitakuwa vita kwa mbele, yaani vita juu ya vita.
Kwa kuwa hatuitaki busara ya upendo na amani, ulimwengu utamjua Yesu ni nani, kama siyo tungali hai basi tungali tunashushwa makaburini mwetu! Hivi kumkaidi Yesu, Mungu na Mwana wa Mungu kuna faida gani kama tunakufa hivi? Mungu tunusuru na janga hili la kukataa au kuchelewa kumjua Mungu na Mwanao. Narudia na kusisitiza. Dini yenye dawa ya magomvi yetu yote ulimwenguni ni UKRISTO PEKE YAKE! Tuendelee tu kubisha tushindwe kusalimika. Hadi sasa kuna faida gani? Tunamkataa Yesu sisi na tunakufa sisi. Basi, shauri letu!
Mzee wenu Pd. Titus Amigu
Mbona inafahamika kuwa, Yesu ni Bwana?

malaika wanimba na kusujudu Yesu ni Bwana.....

malaika wanasifu huko mbinguni Yesu ni Bwanaa.....

amewabadilisha yesu, Yesu ni Bwana.....

usiku na mchana kunaimbwa Yesu ni Bwana....

anaburudishaaa Yesu, Yesu ni Bwana......
 
Jumapili ilitakiwa humu kuwe na mada fupi fupi tu, mtu unaandika paragraph nne kama unaomba msamaha kwa mkeo
 
umeandika Matakataka Matupu. China,japan,korea, Huko Hawamjui Huyo Yesu, Je Hakuna Amani?
Na Wapo Mbali Kuliko Ninyi Mnaoshinda Makanisani Kuomba,

Moderator Angalieni Matumizi Ya Hizi Badge,zinaleta Attention Kumbe Mtu Kaandika Matakataka T
Tu,
 
Haya mambo yangepelekwa jukwaa la dini hawa kondoo wakutane huko .
 
Sijasoma hii habari ndefu (itakuwa matumizi mabaya ya muda) kwahio nimesoma heading tu huenda swali langu likawa nje ya mada...., Je kipindi cha Yesu anaishi kulikuwa hakuna Vita ?

Kwanza naweza kusema tumekuwa civilized zaidi kuna watu walikuwa watumwa enzi za yesu (imani kwamba watu hawalingani na wengine ni watwana) hao sijui unaweza kuwaambia nini their life was not any better
 
Hizi dini hizi...aiseee.

Ili uelewe na kuamini maandiko ni lazima ujizime data, au uondoe ubongo kwenye fuvu na ujaze kinyesi.
 
Sasa ulimwengu utamjua Yesu ni nani. Lakini vita hivi ni fursa ya Ukristo kuzishinda dini zingine. Laiti tungelimakinika na fursa hii!
Waliokuwa wanamkataa Yesu watamjua Yesu sasa.

Nadhani tangu hivi karibuni, kila dakika kumi Mungu anapokea roho ya marehemu fulani, mhinga wa vita. Ikija roho ya mtoto, inakuja roho ya mtu mzima. Ikija roho ya kijana, inakuja roho ya mzee. Ikija roho ya mrefu, inakuja roho ya mfupi. Ikija roho ya mnene, inakuja roho ya mwembamba. Ikija roho ya mweusi, inakuja roho ya mweupe na kadhalika. Wote hao wahinga wa vita. Vita vinatafuna uhai. Kuna vita Nigeria. Kuna vita Somalia. Kuna vita Kongo. Kuna vita Msumbiji. Kuna vita Ukraine na kiboko cha vita vyote hivyo ni vita ya Palestina. Huko Gaza tunaweza kufikiria kupanda viazi vitamu au viazi mviringo kwa jinsi vifusi vinavyozidi kulundikana.

Kifupi, hakutakuwa na taabu ya kupanga matuta tutakapoanza upanzi wetu.

Yote haya ni kwa nini? Ni kwa sababu kuna chuki. Kuna chuki majumbani. Kuna chuki vitongojini. Kuna chuki kati ya dini. Kuna chuki kati ya nchi. Kuna chuki kati ya Waafrika. Kuna chuki kati ya Wasemiti. Kuna chuki kati ya watu weupe na kadhalika. Wanadamu wanachukiana. Hawataki kusikilizana na kupatana. Hawataki kumaliza tofauti zao kwa amani. Watu wanajinasibu kwa maneno na maandishi tu kuwa ni watu wa dini za amani wakati ukweli si hivyo. Zilongwa mbali, zitendwa mbali. Sijui anadanganywa nani?

Kutoka Kukong’otana hadi Msamaha
Kuna safari aliyotufanyiza Yesu ambayo wengine hawana muda wa kuisikiliza ikisimuliwa. Kwa kuwa hatutaki kumsikiliza Yesu, tutasadikishwa na maafa makubwa. Lakini ajabu ni kwamba kenge hasikii hadi atoke damu puani! Ni hivi kuna safari kutoka kwa mtu aliyekuwa anaitwa Mfalme Hammurabi, hadi Torati hadi Yesu Kristo. Nisikilizeni na mniamini.

Enzi za Hammurabi – Kukong’otana
Mosi ni enzi za Hammurabi. Enzi zile za miaka 1750 K.K., kabla ya kuanzishwa kwa Dini ya Kiyahudi, mfalme mmoja aliyeitwa Hammurabi wa huko Mashariki ya Kati, alipendekeza dawa ya kumaliza magomvi kati ya watu kuwa ni kukong’otana kwa vipigo vya mbwa, yaani kupiga mpaka mtu akome kwa kupigwa. Yaani kwamba mkosefu akong’otwe kupita kile alichotenda. Yaani, kwa mfano, yaya akimdondosha mtoto, yaya huyo anyongwe kusudi akome na wengine wote watakaosikia habari hiyo wasithubutu hata siku moja kuwadondosha watoto wa watu.

Mintarafu mauaji, Hammurabi alipendekeza mtu akimuua mtu mmoja, alipwe kwa kuuawa na kwa mtu mmoja aliyemuua wauawe jamaa zake sabini – mmoja kwa sabini. Amri za Hammurabi hazikumaliza uovu wowote duniani.

Enzi za Torati – Malipo Sawa kwa Sawa
Baada ya enzi za Hammurabi ikaja enzi ya pili. Mnamo mwaka 1250 K.K. iliingia Torati. Wayahudi walishangilia sana maana Torati ilitaka mkosefu asilipwe zaidi ya kile alichokosea isipokuwa alipe sawa sawa kabisa na kile alichofanya.

Wayahudi waliiona enzi hii kuwa enzi za haki sana. Kisasi kikahesabiwa kuwa haki ya mtu, enzi ya kulipana sawa kwa sawa. Yaani kwa mfano, kama mtu alimtoboa mwenzake jicho la kushoto, na yeye aletwe mahakamani na atobolewe jicho la kushoto vile vile.

Kama mtu alimvunja mwenzake mkono wa kulia karibu na kiwiko, na yeye aletwe mahakamani avunjwe mkono wa kulia karibu na kiwiko vile vile. Kama mtu alimvunja mwenzake mguu wa kushoto karibu na nyonga, na yeye aletwe mahakamani avunjwe mguu wa kushoto karibu na nyonga. Kama mtu alimuua mtu fulani na yeye aletwe mahakamani kisha auawe vile vile.

Hii ndiyo ilikuwa kanuni ya jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu, kuteketeza kwa kuteketeza (moto kwa moto), jereha kwa jeraha, chubuko kwa chubuko na uhai kwa uhai. Kwa Kiingereza kanuni hii huitwa “tit for tat” (Kut 21:24). Kanuni hii haikumaliza uovu wowote duniani. Kauli iliyokomeshea mambo hapa ni “Moto kwa moto” badala ya “Dawa ya moto ni maji.”

Enzi za Yesu na Agano Jipya – Kupendana na Kusameheana
Mwaka 1 Mwaka wa Bwana, Yesu Kristo, Mwana wa Mungu akatujia ulimwenguni na kutufundisha mambo mengi. Katika yote akatupa amri kuu ya mapendo: “Tumpende Mungu kwa moyo wetu wote, kwa roho yetu yote na kwa akili yetu yote” na kwa upande mwingine akatuagiza tumpende jirani yetu kama tunavyojipenda wenyewe (Mt 22:37-40). Katika kumpenda Mungu alimaanisha mambo matano: kumwabudu, kusali, kuweka nadhiri au ahadi na kuzitimiza, kutoa sadaka na zaka na kufanya toba. Na katika kumpenda jirani alimaanisha mambo 14: matendo saba ya huruma kwa miili ya wenzetu na matendo saba ya huruma kwa roho za wenzetu.

Kwa matendo saba ya huruma kwa miili ya wenzetu Yesu alimaanisha: kuwalisha wenye njaa, kuwapa cha kunywa wenye kiu, kuwakaribisha wageni, kuwavika wasio na nguo, kuwatazama wagonjwa, kuwatazama wafungwa na kuwazika wafu.

Kwa matendo saba ya huruma kwa roho za wenzetu Yesu alimaanisha: kuwafundisha wajinga, kuwashauri wenye mashaka, kuwaonya wakosefu, kuvumilia magumu, kuwavumilia wasumbufu, kuwafariji wenye dhiki na kuwaombea wazima na wafu. Haya yote ndiyo yanaoitwa UKRISTO.

Ndipo yeyote anayemkubali Yesu kwa dhati anakuwa “mwana wa Mungu” kwa maana kwamba anakuwa mwana wa upendo, mtu mwenye kusamehe, mtu mwenye kuheshimu uhai wa wengine. Wakristo tunawiwa mfano mzuri hapa. Ilipasa tulipo sisi pasiwepo magomvi wala vita vyo vyote. Lakini, si mara haba, masakubimbi na malipyoto hufaulu kutuingiza hata sisi kwenye magomvi na vita. Loh! Hapo huwa tunamfedhehesha Yesu, Mungu wetu na walimu wetu mwema.

Wengine wetu huwa na maneno machafu kana kwamba wamefia samaki vinywani mwao na wengine wetu wakali na wauaji kupita mbogo.
Mintarafu kukoseana Yesu alitutaka tuache UHAMMURABI na UTORATI. Alitaka watu tusameheane 7 x 70.

Maandiko yetu Matakatifu yanabanisha haya katika Mt 18:21-35 na Rum 12:3-21. Kifupi Yesu alitaka watu tusameheane kama tunavyosamehewa na Mungu Baba yetu (Mt 6:12. Alitutaka mtu akipigwa shavu la kushoto ageuzie hata shavu la kulia na anayelazimishwa kwenda na mtu maili moja akubali kwenda hata maili mbili (Mt 5:38-42).

Tungemwelewa vyema Yesu alitaka watu tusidaiwe chochote na mtu isipokuwa upendo, tusilipe ovu kwa ovu. Kifupi alitutaka katika uovu, tusifukuzane na mwenda wazimu (Rum 12:14-21).

Kwa kutatua migogoro yetu, Yesu alitupa mchakato wake bora: kukaa na kuongea wawili yenu. Ikishindikana alisema kuwaalika mashahidi wawili watatu. Ikishindikana hapo basi ni kukaa kitako na Kanisa. Hatimaye, ikishindikana hapo basi ni kuachana pasipo kupigana, yaani kila mtu akashike hamsini zake lakini huku mkiombeana kila mtu arudi kwenye utimamu wa kufikiri vyema pamoja na kutubu (Mt 18:15-18).

Walimwengu Wanahusudu Kisasi
Ajabu lakini ni kwamba wanadamu walimkataa Yesu, wakapendelea giza kuliko mwanga (Yn 1:3-8) na mbaya zaidi wengine wakaja na dini zao za ajabu ajabu. Dini zinazomkubali kabisa Hammurabi na kuwa na visasi.

Wakacheka dawa aliyopendekeza Yesu mintarafu magomvi. Wanadamu wakamcheka Yesu na habari yake ya upendo na msamaha. Wakamwona Yesu lofa. Wakamwona Yesu hamnazo. Sawa! Dini hizo zote zikawa zinarejea kwenye UHAMMURABI yaani kwenye kanuni za kukong’otana kwa vipigo vya mbwa (visasi vikali mno) au kwenye UTORATI, yaani kulipana sawa kwa sawa, kanuni ambazo zilipwaya hapo mwanzo. Dini hizi zikawa bure kabisa. Sasa? Ndiyo maana leo hii kukong’otana ni kwingi mno. Na bado kama hatutaki kumsikiliza Yesu katika kupendana na kusameheana, tutamalizana!

Bado mpaka Wote Tumkubali Yesu
Humu barani Afrika, Ukraine na Palestina mambo moto. Kweli mpambe wa mauti ni kiburi. Msinibishe. Popote pale ukikiona kiburi kinakuja ujue mauti anafuata. Wanadamu tutamalizana mpaka akubaliwe Yesu Mwana wa Mungu na ujumbe wake wa upendo na msamaha. Kifupi, ni mpaka msamaha ni kupotezea bure tu, wala si ulofa. Watu waupokee na kuuishi Ukristo. Bila hivyo, hakuna amani ulimwenguni isipokuwa vitakuwa vita kwa mbele, yaani vita juu ya vita.

Kwa kuwa hatuitaki busara ya upendo na amani, ulimwengu utamjua Yesu ni nani, kama siyo tungali hai basi tungali tunashushwa makaburini mwetu! Hivi kumkaidi Yesu, Mungu na Mwana wa Mungu kuna faida gani kama tunakufa hivi? Mungu tunusuru na janga hili la kukataa au kuchelewa kumjua Mungu na Mwanao. Narudia na kusisitiza. Dini yenye dawa ya magomvi yetu yote ulimwenguni ni UKRISTO PEKE YAKE! Tuendelee tu kubisha tushindwe kusalimika. Hadi sasa kuna faida gani? Tunamkataa Yesu sisi na tunakufa sisi. Basi, shauri letu!

Mzee wenu Pd. Titus Amigu
Waafrica dini zimewaharibu sana .mmekuwa kama mazombi.asilimia kubwa ya wakristo wako africa ndo inaongoza kwa magonjwa vita njaaa huyo yesu mbona asiwasaidie
 
Back
Top Bottom