Je, ukataji tiketi wa mabasi ya mkoani kupitia mtandao una changamoto zozote?

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,834
18,835
Habari zenu wakuu,

Nataka kusafiri kwenda mkoani na tiketi ya basi nishazoea kukata manual lakini siku hizi ni mtandaoni, ila nilisikia madereva wakitaka kugomea huu utaratibu lakini sikusiukia iliishia wapi.

Je, bado wanakata tiketi za mtandaoni au baada ya ule muito wa mgomo ilisitishwa?

Je, ukikata tiketi hizi kuna changamoto gani unaweza kukumbana nazo?

Ni hayo tu wakuu, naomba majibu kwa wenye ufahamu.
 
Basi sio kama ndege ndugu. Unaweza ukakata tiketi ya kitu cha ajabu mpaka mwenyewe ukashangaa. Mi uwa nikifika front, baada ya kuliona gari lenyewe linalondoka muda huo ndo nakata tiketi.
 
Basi sio kama ndege ndugu.unaweza ukakata tiketi ya kitu cha ajabu mpaka mwenyewe ukashangaa.mi uwa nikifika front, baada ya kuliona gari lenyewe linalondoka muda huo ndo nakata tiketi.
kwa hiyo sio lazima ukate mtandaoni sio?
 
Habari zenu wakuu,

Nataka kusafiri kwenda mkoani na tiketi ya bgasi nishazoea kukata manual lakini siku hizi ni mtandaoni, ila nilisikia madereva wakitaka kugomea huu utaratibu lakini sikusiukia iliishia wapi.

Je, bado wanakata tiketi za mtandaoni au baada ya ule muito wa mgomo ilisitishwa?

Na je, ukikata tiketi hizi kuna changamoto gani unaweza kukumbana nazo?

Ni hayo tu wakuu, naomba majibu kwa wenye ufahamu.
Inategemea unaenda mkoa gani? Mfano kwa sisi tunaopenda safari za Dom , shabiby unakata tiketi mtandaoni fresh tuu, hamna shida yoyote mkuu
Ila ushauri wa wengine pia ni muhimu nenda kituoni
 
Moja ya changamoto niliiona na ikawa issiue ni Kampuni ya Ester Luxury unakta ticket ya Luxury matokeo basi linakuja unaingia ndani unakuta ni semi luxury. Nauliza Luzury ni sh ngapi konda anajibu hovyo kiwa haimuhusu nikaulize ofcn. Hapo ni alfajiri kituo ni cha njiani. Yaani hii kitu wasiooangalia abiria wanaibiwa live.
 
Only from khm to shy bus frester ndo walifanya Ile ya kimtandao Kama serikali inavyotaka.

Zile booking za mtandao hazina mana hapa Tanzania wafanyabiashara wengi hawajui Nini maana ya internet matajiri wengi bado wanatumia visimu vya tochi akiwa na smartphone anaitumia kwa ajili ya WhatsApp, Facebook na kuchek matokeo LiveScore
 
Back
Top Bottom