Nonchalant
JF-Expert Member
- May 10, 2015
- 293
- 388
Baadhi ya Malengo na faida mfumo wa ukataji wa tiketi za bus kielektroniki nchini
▪️Kuwa na udhibiti katika sekta ya usafirishaji.
Wasafirishaji kuwa na ushindani wenye tija, Mfano kwa sasa nauli zinazowaongoza ni za mwaka 2013 lakini hawazitumii. Basi la daraja la juu (luxury) anauza bei ya daraja la kati (semi luxury). Basi la daraja la kati (semi luxury) kuuza bei ya daraja la chini (ordinary)
Mfano. DAR-MWANZA semi luxury ni TZS 61400, Ordinary 42600. Kwa sasa mpiga debe/ wakala anauza semi luxury kwa nauli ya 45000 mmiliki anapewa 25000-35,000. Ordinary auze bei gani?
Mawakala na wapiga debe wanachukua fedha nyingi sana tena isiyolipiwa kodi ambayo alistahili kuipata mmiliki wa basi/mwekezaji.
NAULI
▪️Kwa sasa mpiga debe ni kama share holder wa mwekezaji. Ili hali halipi kodi, haweki mafuta, hanunui tairi, hanunui vipuli, na hana msaada wowote kwa mmiliki zaidi ya kukamata abiria wanaosafiri na kusema ni abiria wake.
▪️Kuwa na Udhibiti wa sekta pia, nauli zitadhibitiwa kutopandishwa hovyo au kushushwa kupita kiasi.
Nauli zinapopandishwa kupita viwango elekezi ni kosa kisheria na huumiza wananchi.
Pia zinaposhushwa kupita viwango elekezi humtia hasara mwekezaji kupelekea kufilisika na kufungwa kwa biashara. Wengi tumeona kampuni nyingi zinaanzishwa na kufa kutokana na kukosa udhibiti na kuwepo kwa ushindani usio kuwa na tija kwa wamiliki wa mabasi.
Ajabu ni kwamba wamiliki hawa nauli elekezi zinazotumika ni za mwaka 2013 na hazitumiki, wanatumia robo ya nauli mpaka nusu ya nauli elekezi kisha wanalalama kwa nini mafuta yanapanda nauli hazipandi! Fedha nyingi zinapotea kwa kukosa udhibiti hasa kwa wapiga debe na mawakala.
FLOAT:
▪️Hii inamwezesha mmiliki kupokea fedha yake kwa wakati. Tiketi yoyote itakayouzwa katika kituo chochote kwa wakala/mpiga debe/ofisi yoyote, pesa yote itakwenda kwa akaunti ya mmiliki bank muda huohuo.
Mmiliki ataidhibiti pesa yake wakati wote tofauti na ilivyo sasa
▪️Wakala atabaki na cash ambayo atapaswa kuirudisha kwenye float ili aweze kuendelea kuuza tiketi. Itawasaidia sana wamiliki kupata fedha zao kwa wakati kuondoa wizi na ubadhirifu unaofanywa na mawakala/wapiga debe.
▪️Lakini pia pesa zinapoenda bank cash flow yote ya mmiliki bank yake itatambua hivyo kumwezesha mmiliki kukopeshwa kwa urahisi.
▪️Kwa njia hii itafungua milango ya ajira kwa mawakala, madereva, makondakta, waasibu, mafundi n.k tena ajira zenye tija kuliko kuendelea kufanya udalali, na wizi wa kuwaibia wamiliki. Fedha yote ataipokea mmiliki na kuidhinisha ifanye kupanga matumizi kwa ajili ya kampuni yake.
Ajabu jingine kwa sasa wakala ndiye anayepokea fedha yote ya mmiliki, kuipangia matumizi kisha kuamua utume kiasi gani kwa mmiliki.
▪️Mmiliki wa basi au mwekezaji atakapotoa ajira rasmi, atawezesha wafanyakazi wake wote kulipa kodi (PAYE) ya serkali, hifadhi zao katika mifuko ya hifadhi ya jamii, na Mmiliki wa bus atalipa kodi stahiki pasipo kukadiriwa wala kuiibia serikali kwa sababu mapato yake yote yatajulikana
▪️Mmiliki hana ulazima wa kuweka float ya gari zima kama inavyosemekana yaani siti zote za bus. Kwani abiria watajinunulia tiketi wenyewe waapo nyumbani, kazini au mahala popote hivyo kiasi cha float kitakua ni kidogo sana baada siti kadhaa kununuliwa mtandaoni.
▪️Lakini pia sio lazima kuweka float ya siti zote. Wakala wa mmiliki anaweza kupewa kiasi kidogo cha float. Mfano kwa gari ya nauli ya tzs 30,000 wakala apewe Tzs 300,000 kwa masharti, mfano kila atakapouza siti 7 ambazo ni Tzs 210,000
arudishe cash aliyoipata katika namba yake ya float. Hii itarahisha sana badala kuweka mamilioni katika float kama wanavyodhani.
Suala la float ni la muda tu kwani litaondoka kabisa pale wananchi watakapofahamu namna kununua tiketi online wenyewe.
▪️NJIA NYINGINE ZISIZOMTAKA MMLIKI KUTUMIA FLOAT, ni kutoa bili kwa abiria anapokuja ofisini/kwa wakala atapewa bili ya tiketi yake alipe mwenyewe kwa kutumia mitandao ya MPESA, TIGOPESA, kwa control number/reference number/kumbukumbu namba. Baada ya malipo atapewa tiketi yake kwa kuprintiwa au sms.
Tasisi nyingi za kiserikali na binafsi zinatumia njia hizi kwa sasa mfano TRA, TANESCO, Bill za maji, Hospitali, bank, TANAPA, Maduka ya online n.k
Tunapomaswa sisi kama nchi kuondoa mifumo ya cash inayoleta na inayoendeleza urasimu, wizi katika maofisi na biashara zetu. Wananchi/wahitaji huduma wajilipie wenyewe kwa kutumia mitandao badala ya kwenda kupanga foleni kupata huduma.
TAKWIMU
▪️Serikali yetu itapata takwimu halisi katika seka ya usafirishaji, adadi ya bus zinazosafiri katika ruti fulani, idadi ya abiria wanaosafiri kwa siku/mwezi/mwaka hivyo kuweza kutoa kipaumbele katika utoaji wa huduma. Mfano kuongeza kuruhusu wawekezahi zaidi katika ruti/njia nyenye upungufu. Kipaumbele cha matengezo ya barabara au hata kuziboresha zaidi n.k
NJIA ZA KUNUNUA TIKETI YA BASI
▪️Namna mwananchi anavyoweza kujinunulia teketi awapo nyumbani/ofisini n.k
Bonyeza link
Tiketi Mtandao - Apps on Google Play
Pakua application ya tiketi mtandao kutoka playstore kisha tafuta unapotoka, unapokwenda na tarehe ya safari. utachagua basi, siti uipendayo na kufanya malipo.
Nitaonyesha njia nyingine hapo badaee
Baadhi ya route zinazopatikana katika tiketi mtandao kwa sasa
DAR ES SALAAM-DODOMA
DODOMA-DAR ES SALAAM
DAR ES SALAAM-MBEYA
DAR ES SALAAM-TANGA
DAR ES SALAAM-MTWARA
DAR-LINDI
TANGA-DAR ES SALAAM
TANGA-ARUSHA
TANGA-MOSHI
DODOMA-MOSHI
DODOMA-ARUSHA
Hizi ni baadhi tu,
Njia nyingine zitaongezwa hivi karibuni.
Wamiliki wengi wangependa kuona mfumo huu unafanya kazi ili waweze kupata udhibiti wa biashara zao na faida, kwachache wenye maslahi ya wizi, tena wasio na kampuni ya bus ndio wenye kukwamisha jambo hili lenye tija kwa taifa letu na wafanyabiashara wenyewe na wananchi.
Changamoto hutatuliwa....
TUIJENGE NCHI YETU.
Tutaendelea kuelimishana.......