Je, Tundu Lissu anazo sifa za kuwa Rais wa Tanzania?

Magufuli pekee ndio alionyesha kuiweza hii nchi.

Mtu kama polepole, Bashiru wanaweza.

Tundu haeleweki anataka nini.
 
Ni kama Kenya vile, wana katiba mpya saafi, maseneta, counties, ugatuzi na mahakama saafi, lakini sera za uchumi, chakula na usalama ni zilezile za Jomo Kenyatta. Maisha yao yanazidi kuwa mabaya kiuchumi. Lazima tuwe na uhakika tunataka nini wakati gani.
 
Kuacha kutuambia atafanya nini juu ya wezi wa mali ya umma, maji, uchukuzi, elimu, ajira, umeme, gharama za maisha, chakula, hali ya hewa, masoko, mitaji, technolojia, nk.
Yaani hivi vitu ulivyotaja hapa viongozi wengi wa kiafrika wamefeli kuvifanya, na hawawezi, hata walio nje ya system wakipewa hawawezi kuvifanya. Kwa kifupi Afrika ipo kwenye mkwamo mkubwa. Na inaweza kuchukua hata karne kutoka hapa tulipo kwenye mkwamo.

Yaani afrika Raisi hata akiwa na dhamira njema atashindwa tu kuleta maendeleo na kujenga nchi kwakuwa amezungukwa na ndugu, jamaa na marafiki ambao wanataka kunufaika kupitia taasisi ya uraisi. Watoto wa maraisi , wakwe , ndugu na jamaa wanataka kukwepa kodi kwa kupitia jina la Raisi. Yaani Afrika ina safari ndefu sana.
 
Wanazo zote na za ziada ndio maana uchaguzi wa mwaka tulimshauri Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Ila kwa uchaguzi wa 2025, niliwaomba Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! hivyo iwapo CCM itamsimamisha mgombea Mwanamke, TL asigombee maana itakuwa ni aibu kushindwa na Mwanamke!.

Unless kama sauti hii ni yake YEYE, Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke then TL agombee, wapambane!.

P
Tz kwa sasa , lazima badilisha , chama kinachounda serikali ili kuweza toka tulipo ,mfano Zambia mnaona jinsi nchi ilivyotulia ,Rais anajua kwa nini yuko pale, tabili uchwara sijui mwanamke tupa kule
 
Yaani hivi vitu ulivyotaja hapa viongozi wengi wa kiafrika wamefeli kuvifanya, na hawawezi, hata walio nje ya system wakipewa hawawezi kuvifanya. Kwa kifupi Afrika ipo kwenye mkwamo mkubwa. Na inaweza kuchukua hata karne kutoka hapa tulipo kwenye mkwamo.

Yaani afrika Raisi hata akiwa na dhamira njema atashindwa tu kuleta maendeleo na kujenga nchi kwakuwa amezungukwa na ndugu, jamaa na marafiki ambao wanataka kunufaika kupitia taasisi ya uraisi. Watoto wa maraisi , wakwe , ndugu na jamaa wanataka kukwepa kodi kwa kupitia jina la Raisi. Yaani Afrika ina safari ndefu sana.
kubadilisha chama na mgombea inafanana kabisa na kubadilisha walaji wapwa tu ila mwananchi atabaki palepale au atazidi kurudi nyuma zaidi. maTatizo yetu makubwa ni sio katiba Mpya, bali viongozi imara na waadilifu, mitaji, teknolojia, masoko huru kwa bidhaa zetu na mifumo mibaya ya dunia ya manunuzi. Yaani lazima uwe na dola ili upate bidhaa kama mafuta, mitumba, magari, matrekta, nk. Shida inakuja kwenye namna ya kuipata hiyo dolla.
 
Anazipita hizo sifa, tunataka Rais anayeelewa nini umuhimu wa Katiba hasa kwenye check and balance ya mihimili yote mitatu, Kuheshimu utawala wa sheria - kifupi tunataka Rais ajaye awe na werevu wa Sheria ili atupitishe salama kwenye transition yetu toka ujamaa uliofeli kuelekea kwenye uwekezaji wa mitaji.

Lissu ni jibu pekee, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu aligomea kifo chake.
 
Urais ndio kazi rahisi Sana Kama utateua watu wenye akili kwenye taasisi za serikali. Na Kama utazungukwa na washauri wenye Nia njema na nchi.
Idd Amin alishakua rais
Marcia's Nguema alikua rais
Kuku Gbendu WaZabanga Mobutu Sese Seko.
Tito Okello
Samwel Kanyon Doe alikuwaga rais.
Yule bwege shit aliyejipachika u emperor na hata hili jinga lililo oa kikongwe kule ufaransa Ni rais.
Tundu Lissu anasifa nzuri kuliko wote Hawa.
 
Wanazo zote na za ziada ndio maana uchaguzi wa mwaka tulimshauri Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Ila kwa uchaguzi wa 2025, niliwaomba Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! hivyo iwapo CCM itamsimamisha mgombea Mwanamke, TL asigombee maana itakuwa ni aibu kushindwa na Mwanamke!.

Unless kama sauti hii ni yake YEYE, Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke then TL agombee, wapambane!.

P
CCM msiangaike 2025 mpeni Askofu Josephat Gwajima!!
Wengine waliobaki,watatutumbukiza shimoni!
 
MaTatizo yetu makubwa ni sio katiba Mpya, bali viongozi imara na waadilifu, mitaji, teknolojia, masoko huru kwa bidhaa zetu na mifumo mibaya ya dunia ya manunuzi. Yaani lazima uwe na dola ili upate bidhaa kama mafuta, mitumba, magari, matrekta, nk. Shida inakuja kwenye namna ya kuipata hiyo dolla.

Ni kweli matatizo yetu sio katiba mpya. Umekiri kwamba tunahitaji viongozi imara na waadilifu, najaribu kuwaza kwa sauti huenda pia hii katiba inatoa huo mwanya wa kupata viongozi wa siyo imara na waadilifu, hapo unaonaje?

Je wewe kwa upande wako Unadhani nini kinazuia kupata hiyo dola yenye nguvu ya kubadilisha hali ya mambo ikiwemo kupambana na hiyo mifumo mibaya ya dunia ya manunuzi?

Je hauoni kwamba kuwa na dola yenye uwezo wa kupambana na mifumo mibaya ya manunuzi ya dunia ni sawa na kuwa against na wakubwa wa dunia?

Na kwanini wanasiasa wa afrika wanan'gan'gania kushika dola hali yakuwa wanafahamu fika kuwa hawawezi kubadili hali ya mambo?

Mwisho nini kifanyike kuipata dola ya aina hiyo?

Funguka mkuu tujifunze.
 
Urais ndio kazi rahisi Sana Kama utateua watu wenye akili kwenye taasisi za serikali. Na Kama utazungukwa na washauri wenye Nia njema na nchi.
Idd Amin alishakua rais
Marcia's Nguema alikua rais
Kuku Gbendu WaZabanga Mobutu Sese Seko.
Tito Okello
Samwel Kanyon Doe alikuwaga rais.
Yule bwege shit aliyejipachika u emperor na hata hili jinga lililo oa kikongwe kule ufaransa Ni rais.
Tundu Lissu anasifa nzuri kuliko wote Hawa.
Anasema nini kuhusu haki za mashoga?
 
Back
Top Bottom