Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,703
- 218,246
Tundu Lissu amefika kwenye Msiba wa Lowassa kuhani na kuwapa pole Wafiwa , ambapo amemmwagia sifa Lowassa na kuzungumza kwamba baada ya Nyerere Lowassa ndiye Mwanasiasa aliyefuatia kwa Ushawishi .
Amedai kwamba wanasiasa wengi waliokufa na hawa waliopo walipata umaarufu baada ya kuwa Marais , lakini bado hawakumzidi Lowassa ambaye hakuwahi kuwa Rais na hata huo Uwaziri mkuu wake ulikuwa wa miaka miwili tu .
Tundu Lissu amesema pamoja na kuhudhuria msiba wa Lowassa lakini amekuja pia kumfariji Mama Regina Lowassa ambaye alikuwa Mwalimu wake miaka 41 iliyopita alipokuwa Kidato cha kwanza .