Je, Tundu Lissu anazo sifa za kuwa Rais wa Tanzania?

Kwanini hizo sifa aulizwe kuwa nazo Tundu Lissu, na wengine wote kasoro Mwalimu Nyerere wasiwe wameulizwa kama wanazo?

Hebu chukulia mfano wa huyu tuliye naye sasa, halafu nipe sifa hata moja tu ya kipekee inayomtambulisha kuwa na sifa za urais?

Kwa maoni yangu, Tundu Lissu anazo sifa kumzidi Mwinyi, Kikwete na ningesema hata Magufuli, isingekuwa uigizaji wa uzalendo aliojaribu kuuonyesha.
 
Rais wa nchi yetu awe na sifa zipi? Je, ni nani anazo sifa nyingi za kuwa Rais ajae? Je, Mh. Tundu Lissu anazo sifa hizo pia?
Hakuna sifa kuu kwa kiongozi wa nchi kuwa nayo inayozidi UZALENDO kwa nchi yake.

Kwa hiyo napendekeza uanzie kwenye sifa hiyo.

Kiongozi wa nchi ni muhimu awe na dira inayomwongoza ni wapi nchi anayoiongoza iende na kwa mipango gani na wakati maalum. Siyo maswala ya kubahati sha tu

Kiongozi ni lazima awe na imani na wananchi wake, kwamba hawa watu ndio walio na uwezo wa kujiletea maendeleo na kubadilisha hali duni ya maisha yao. Hayo mengi sana tunayopigiwa kelele kuhusu uwekezaji, hiyo ni kuongezea tu juu ya juhudi zetu wenyewe

Kiongozi ni atakayeheshimu na kujali mali za taifa hili. Asiyekuwa na uvumilivu kabisa katika kutapanya mali za nchi yetu bila ya mpango maalum. Madini yote sasa karibu yamesombwa, lakini ukiuliza ni miradi ipi iliyobadilishwa na madini hayo, hupati jibu hata moja.

Zipo sifa nyingi..., kiongozi anayeweza kujieleza na watu wakaelewa anachozungumzia kwa lugha inayoeleweka; n.k.,
 
Rais wa nchi yetu awe na sifa zipi?

Je, ni nani anazo sifa nyingi za kuwa Rais ajae? Je, Tundu Lissu anazo sifa hizo pia?
Ukisema Sifa naona kwa Tanzania hilo neno sifa halipo hasa kwa sababu kwa katiba hii Rais lazima atoke CCM. Labda neno la kutumia ni hili, "Chance" ya kuwa Rais wa Tanzania. Lazima uwe CCM (katiba ya sasa), Makamo wa Rais(Rais akifa), Jaji Mkuu (katiba ya sasa), Mbunge, Waziri, ----- (descending----).

Mengine yote hayo ni kuganga njaa.
 
Rais wa nchi yetu awe na sifa zipi?

Je, ni nani anazo sifa nyingi za kuwa Rais ajae? Je, Tundu Lissu anazo sifa hizo pia?
Tundu Lissu anaweza akafanya kwa ufanisi kazi za kutumwa lakini siyo kuwa mwamuzi wa mwisho.

Ana element za Ki-Magufuli kujisikia kuwa yeye ndiyo ana akili kuliko wengine na ni bora kuliko wengine. Hizo ndiyo typical characteristics za ma DIKTETA. Nadhani hata risasi alizopigwa na Magufuli zilitokana na kwamba fuse zinazofanana zili react zilipokutana.

Urais inahitaji mtu humble, mwenye akili iliyotulia, anayefikiria jambo mara 2, anayetafuta ushauri kwa wengine, asiye mropokaji, anaye muogopa Mungu kwa vitendo na asiyependa dhuluma.

Samia hadi 2030
 
Kwanini hizo sifa aulizwe kuwa nazo Tundu Lissu, na wengine wote kasoro Mwalimu Nyerere wasiwe wameulizwa kama wanazo?

Hebu chukulia mfano wa huyu tuliye naye sasa, halafu nipe sifa hata moja tu ya kipekee inayomtambulisha kuwa na sifa za urais?

Kwa maoni yangu, Tundu Lissu anazo sifa kumzidi Mwinyi, Kikwete na ningesema hata Magufuli, isingekuwa uigizaji wa uzalendo aliojaribu kuuonyesha.
Ni zipi ipi (zipi) za ziada anazo TL?
 
Rais wa nchi yetu awe na sifa zipi?

Je, ni nani anazo sifa nyingi za kuwa Rais ajae? Je, Tundu Lissu anazo sifa hizo pia?
hana sifa stahiki kwa nafasi hiyo maoni yangu na mtazamo wangu.
si muaminifu,
si mzalendo, uzalendo wake wa mashaka.
si mstahimilivu
si muungwana
ana majivuno na dharau kupindukia,
amepungukiwa hekima na Busara,
si mtarabibu wala mstaarabu,
ni mbishi asie na utii,
hana mipango bali lawama,
haaminiki kitaifa bali ng'ambo kwa watwana,
ana uchu na tamaa mno,
ni mbinafsi hatari,
ni mpenda fujo sana,
ana chuki na wanaotofautiana nae kimtazamo,
ni mjeuri mwenye elimu
ana hasira iliyofichika.

nadhani Mbowe anafaa zaidi.
ni mstahimilivu,
Mzalendo asiye na shaka,
si mbishi,
ni mtulivu, mwenye hekima na Busara
hajivuni na wala haringi,
muongea kwa utaratibu na ustaarbu,
Hatukani wala kukejeli mtu,
Hana chuki wala habagui wenye tofauti na mtazamo wake.
si mbinafsi.
Anaaminika kitaifa na kimataifa
Jamaa ni muungwana sana,


nakuja kumalizia ngoja nipande daladala kwanza...........
 
Rais wa nchi yetu awe na sifa zipi?

Je, ni nani anazo sifa nyingi za kuwa Rais ajae? Je, Tundu Lissu anazo sifa hizo pia?
TAL ni mwanaharakati na kwasababu hiyo hafai kuwa Rais wa nchi, anafaa kuwa labda Waziri Mkuu Ili awe na mtu anaye m moderate kwenye tabia yake ya uharakati
 
Lissu ana vigezo vyote kuwa Rais ila ni wakati sasa chama kimfanyie branding na kimtafutie PR officer.

Kama walivyosema wachangiaji hapo juu lissu na JPM wana tofauti ndogo sana in terms of haiba.

Mnyika alikua hivyo zamani ila naona alipikwa na Mbowe Sasa yupo composed and matured kuliko zamani.

Lissu pia akiwa managed vizuri akajua mipaka ya kauli zake, kupima madhara ya Kila jambo kisiasa na kuwa "statesman" anayeweza ku bond vizuri na watu wa vyama vyote basi hakuna mtu atamzuia kuingiza ikulu.
 
Back
Top Bottom