Urafiki wakati mwingine unakuja naturally, ukiachana na huu ambao tayari unakuwa na mtu pembeni ambae unamuona kama mnaweza kuwa mna-share vitu pamoja.
Wakati wa upweke mtu anaweza kujitenga na jamii, akaamua kwenda mbali kukaa sehemu ya peke yake. Lakini ajabu hata huki mbali anapokwenda, bado anaweza kupata rafiki.
Urafiki unakuja pale ambapo mtu amezoea kwenda mbali kutuliza kichwa chake kujiepusha na kelele za mijini, siku akirudi tena pale alipozoea kukaa peke yake, ghafla anamkuta mtu mwingine nae amekaa pale pale.
Mwanzo mnakuwa kama hamuaminiani kwasababu hamfahamiani. Lakini baada ya muda mchache story kati yenu zinaanza, baada ya hapo urafiki unakuwa umeshajitengeneza.