Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 371,594
- 860,737
Yanapozidi moyoni inabidi kuyatoa hdharani.. Lakini katika kuyatoa hakikisha unakuwa makini kwakuwa mwisho wa siku inabidi ubaki kuwa wewe!
Yatoe lakini kwa tahadhari kubwa kwakuwa privacy yako ni kubwa na ni muhimu kuliko changamoto unazopitia... Ili mwisho wa siku usibaki na majuto yasiyo na rivasi!
Je ni wangapi kati yetu wanatambua maumivu ya wengine?
Changamoto zao?
Maumivu yao?
Hofu zao?
Vita zao? (Za kiroho na za kimwili?
Hao wengine wanaweza kuwa
Ndugu
Jamaa
Marafiki
Wapenzi nk..
Kuna wakati mtu hahitaji suluhu bali anahitaji mtu wa kumsikiliza tu.. Lakini anayemwamini na ambaye hatamuangusha
Kuna wakati nyuma ya tabasamu zetu
Nyuma ya mafanikio yetu
Nyuma ya ndoto zetu.. Kuna jinamizi kubwa la maumivu linatuandama na kunyonya furaha zetu..!
Siku inaweza kuwa ndefu lakini usihisi yale maumivu ya ndani.. Unaweza kupita mahali na kupata moja mbili za mawazo na ukachangamka kwa muda
LAKINI unaporudi home..
Unapobadili nguo na kufunga mlango lile jinamizi la upweke na maumivu linakuvaa upya😪
Kuna kitu unatamani kitokee lakini hakipo
Kuna mtu unatamani umuone lakini haiwezani
Unatamani uandike.. Lakini huwezi kuandika kila kitu..
Sijui mnanielewa?