Je, Tunaweza Kuwa Marafiki!?

Je, Tunaweza Kuwa Marafiki!?

Every human is a COMPETITION!
... Urafiki uende na TAHADHARI!
Kutoka WhatsApp: kaka Mshana nisaidie kushare ujumbe wangu kwenye mada yako ya marafiki...!

Nimesimama hapa leo nikiwa na moyo uliopasuka vipande vipande, moyo unaovuja damu ya majonzi ambayo siwezi kuifuta.
Hakuna maumivu makali duniani kama pale unapogeuka nyuma na kuona mkono uliokuchoma kisu ni ule ule ulioulisha, ulioubeba, na kuufariji wakati wa shida.

Wale niliowaita ndugu, wale niliowaita marafiki, wale niliowafungulia milango ya siri za maisha yangu, wamegeuka kuwa chanzo cha giza langu nene!!!.
Najuta. Najuta kwa nini sikuona alama za mapema. Najuta kwa nini nilipuuza sauti ya ndani iliyoniambia nishituke.

Nilijitoa mzima mzima, nikawapa uaminifu wangu wote, nikadhani upendo wangu ungetosha kuwalinda.
Lakini leo, nimebaki peke yangu kwenye magofu ya urafiki wetu, nikilia machozi ya majuto kwa kupoteza muda, nguvu, na hisia zangu kwa watu wasiostahili.

Maumivu haya ni funzo gumu sana, lakini yameacha kovu lisilofutika moyoni mwangu.
 
Back
Top Bottom