Je, tunahitaji Vazi la Taifa?

Angalia Avatar yangu utajuwa mimi ni kutoka Taifa gani.

Ni utambulisho wa Uraia wako. Kama mimi hilo ni vazi la taifa letu la Oman.
Wewe na taifa lako mnadhani mnanufaika vipi na kuwa na vazi la taifa, manufaa ambayo mngeyakosa kama msingalikuwa nayo?
 
Angalia Avatar yangu utajuwa mimi ni kutoka Taifa gani.
u
Ni utambulisho wa Uraia wako. Kama mimi hilo ni vazi la taifa letu la Oman.

je hilo vazi ulilovaa lilipatikana kwa watu kukaa kama kamati na kubuni au limejitokeza automatically kihistoria? ni upuuzi mtupu unaofanyika hapa TZ kwa kuunda kamati kubuni vazi la taifa, kitu kama hicho inabidi kitokee automatically kulingana na historia ya taifa husika, ni kama vile lugha ya kiswahili ni kielelezo kimojawapo cha utamaduni(taifa) letu lakini lugha hii hakuna watu waliokaa kama kamati na kuibuni bali imetokea automatically kwa sababu mbalimbali za kihistoria na ndivyo ambavyo vazi la taifa linavyotakiwa litokee!
 
Mradi ulioshindwa kabla ya kuanza! Hivi mnategemea kuna kitu hapo? Vazi la taifa ni utamaduni na utamaduni hauundiwi mezani kama tunavyotaka kuaminishwa.

Wakijitahidi sana tegemeeni mavitenge na itakuwa mradi wa ulaji wa majizi fulani kama kawaida. Mwenye macho haambiwi tazama!
 
mambo mengine ni ulaji 2
mmeshindwa hata kutengene
shati, hilo vazi linatengenezwa na
kitambaa toka kiwanda gani? Na viwanda ha2na.
 
Mi ndio maana napendekeza Tanzania iingie kwenye maajabu saba mapya kabisa ya dunia.
Wewe pamoja na matatizo yote tuliyo nayo, watu kitu wanachoona cha maana ni kuunda kamati kutafuta vazi la taifa!
Halafu? Ina maana tukishapata hilo vazi ndio matatizo yetu ya elimu duni, uhaba wa madawa, miundombinu mibovu, ufisadi, umeme n.k yatakuwa yamekwisha? Hebu msinitie hasira..
 
kuna mtandao umezani mchakato huu..kwa wale wenye kutaka kupiga kura kuhusu vazi hili la taifa.kaa mkao wa kula huduma hii ni bule kabisa.
 
katika kitu ambayo naona serikali inapoteza nayo muda ni swala la vazi la kitaifa,kwanza ni swala ambalo hata hilo vazi likipatikana itakuwa ni kazi bure,leo hii na matatizo yote haya bado mtu eti ujivalishe vazi la taifa?likusaide nni?

Hii ni project ya Nchimbi and company, na matatizo yote tunayokabiliana nayo tunaona vazi la taifa ni priority. Mtu wa kijijini atafaidika vipi na vazi Hilo la taifa. Tusche ulimbukeni tufanye kazi zenye Tija kwa wananchi. Wafanyeni wananchi washibe, wapate matibabu, wapate maji, waondokane na ujinga, sio kutuletea viini macho vya vazi la taifa.
 
chukua herufi za kwanza za makabila yote - tengeneza maumbo/maumbile! ama ngao mbalimbali za makabila! kitambaa murua kabisa!

halafu waachie ndugu wananchi waamue watafanyia nini vitambaa hivyo -- toa miaka mitatu. Ule mtindo utakaokuwa umebebwa na wengi - ndio vazi lenyewe hilo! Usasa/Ukale vyote vitachanganika humo! Ndio itakuwa hali halisi! halafu, hivyo vizazi vijavyo ndio vitakuwa vinaangalia historia yake.
 
lakini mkuu hadi sasa mchakato unaonekana kuanza na hauna uelekeo huo ulioutaja..labda utume meseji nyingi kadri utakavyoweza kuwabadilisha wahusika wakuu wa mchakato.
 
tupe uzoefu wako kuhusu India n.k, wao mavazi yao yanatofautiana kulingana na hadhi? Pia kuhusu hayo magome ya miti kutoka bukoba hasahasa kiziba bado wana elimu hii..yatakubalika kwa hawa vijana wa mjini na hawa wawakilishi wetu(viongozi wapenda suti)? Pia hawa wadau watatumia mria mfumo wa kutuma meseji bure kupendekeza vazi/kitambaa..sasa mimi nina shaka kama waTanzania wa vijijini watashiriki kikamilifu..

ndo maana nimesisitiza kamati izunguke na kutafiti..watakuja na kitu.
Haina haja ya kuwa sceptical,eti uhakika utaalamu wa Wahaya bado upo ama la.. Halafu sikusema litatofautiana kulingana na hadhi ya mtu,someni vyema.. Au kaulize kwa Mnigeria yeyote gharama ya nguo yao ya kitaifa,amu mhindi yeyote muulize Sari hata huko kwao India inauzwaje,kaulize utasikia.. Halafu watu wanadhani ni kama nguo ya kuvaliwa ukienda sokoni au shopping,ni nguo ya heshima sana. Huenda ukaivaa mara moja katika miezi hata sita. Zaidi ni kwamba wataboresha ujuzi watakaojifunza wa njia za asili za kupata vitambaa hivyo.. Na wewe unashauri njia ya ujumbe kupiga kura,sidhani kama ni lazima,labda kama watashindwa kuja na kitambaa ama mshono wa aina moja.
 
lakini mkuu hadi sasa mchakato unaonekana kuanza na hauna uelekeo huo ulioutaja..labda utume meseji nyingi kadri utakavyoweza kuwabadilisha wahusika wakuu wa mchakato.
kukubalika kwa vazi la taifa na kwenyewe ni shughuli tofauti na kuchagua! nadhani kwa sasa tukubali uhalisia wa mchakato huu - maana ulikuwa wazi kwa kitambo
 
Unajua bwana naipenda sana nchi yangu manake imekaa kikomed komed hivi huwa inanipa burudani kwa vituko. Haiishi vituko. Yaani nchi ina akili kama za sekondari tena form tu. AAAA Tanzania, Mambo yanayohusisha tuvikao na tukamati we are very good, eti kamati ya vazi la taifa. Kama tunataka kujulikana kuna vitu vingi vya kututangaza tumeviharibu sasa tunaibuka na vituko. Mfano, MICHEZO, TANZANITE, ML.KILIMANJARO, MBUGA ZA WANYAMA, MADINI, NK. Acheni usanii. Huo ni ulaji mwingine.
 
1. Swala zima la vazi la taifa kupangwa kwa kamati lina matatizo. Vazi la taifa litatoka kwa watu.

2. Serikali inaweza kuchangia kwa kuweka mazingira ambayo yanaweza kustawisha kuwepo kwa vazi la taifa. Kwa mfano, kwa kufufua sekta ya viwanda vya nguo nchini, na kuacha designers wenyewe washindane, vazi litakalopendwa na wengi kama lina muonekano wa kitaifa automatically litakuwa la taifa. Hatukuwa na kamati ya kupanga wanawake wavae khanga au vitenge, ni vitu vinavyotokea organic tu. Huwezi kupanga mipango miingi ya vazi la taifa wakati huna hata viwanda vidogo vidogo tu vya nguo, achilia mbali textile mills.
 
Mi ndio maana napendekeza Tanzania iingie kwenye maajabu saba mapya kabisa ya dunia.
Wewe pamoja na matatizo yote tuliyo nayo, watu kitu wanachoona cha maana ni kuunda kamati kutafuta vazi la taifa!
Halafu? Ina maana tukishapata hilo vazi ndio matatizo yetu ya elimu duni, uhaba wa madawa, miundombinu mibovu, ufisadi, umeme n.k yatakuwa yamekwisha? Hebu msinitie hasira..

Well said mkuu
 
Back
Top Bottom