Je tuhahitaji tena Ze Utamu?

Je tuhahitaji tena Ze Utamu?

Status
Not open for further replies.
Hakuna anayekubaliana na kitendo hicho cha kuchafuliwa Mhe. Rais. Hapa tunajadili issues nzito zinazolitafuna Taifa letu sio ushenzi kama ule. Kama kuna mtu anayewafahamu basi awasaidie Polisi. Pole Mhe. Vijana wako hao adamu imekwenda sokoni.

Ni kweli tusitoke kwenye mada za muhimu zaidi na kutumia muda mwingi kwenye huu uchafu. MAADILI YAKILEKEBISHWA HAYA YOTE HAYATATOKEA HIVYO VIONGOZI INABIDI WAKUBALI MAMBO YAREKEBISHWE VINGINEVYO UTAKUTA SIKU PICHA YA MKULU SASA MWANAE NDIYO ANAMREKEBISHA...KAMA HATUTAKUWA MAKINI NA VIONGOZI WETU KUBADILIKA.
 
nasikia tu mnapiga makelele....mbona sijaweza kuiona hiyo picha jamani??? naona the site is down au imefanyiwa mambo????nikiweza kuiona nitatoa maoni kamili....i knew the story...
 
Yaani watu wanasubiri hadi picha za viongozi ndio wanaona kuwa ZeUtamu haifai wakiwekwa walalahoi mbona mnakaa kimya
Leo ndio mnaona haifai ina maana siku zote huko nyuma kabla hawajamweka Rais alikuwa inafaa?
 
nasikia tu mnapiga makelele....mbona sijaweza kuiona hiyo picha jamani??? naona the site is down au imefanyiwa mambo????nikiweza kuiona nitatoa maoni kamili....i knew the story...

Fungua site hiyo'mbona inafunguka?labda server kwako iko chini.acha nikutumie kwenye PM.
 
Last edited:
Ze Utamu?....siamini nilichokiona, kama kweli ni mgawanyiko wa fikra mbadala basi wa huyu mwenye hii blog nahisi angestahili kuwa monitor/kiranja wa wagonjwa pale Mirembe Hosp.
Kuna vitu ambavyo hata katika "100th World Countries" haviwezi kutokea, ni udhalilishaji wa kiongozi wa nchi kupindukia na ni udhalilishaji wa taifa kwa ujumla...nionavyo mimi, nahisi labda kuna mkono wa mafisadi wenye malengo ksisiasa wanaosupport upuuzi huu.....
Stop, stop, stop,,..........wamiliki na wahusika wote wasakwe kama ilivyo kwa wahujumuuchumi, kwani hawa ni wahujumu taifa.

Vichaa ni watu, na shida kaumbiwa binadamu si mbwa............poleni watanzania wenzangu wenyemapenzi mema mlioathirika na ufedhuli huu.

Stay Blessed
 
Fungua site hiyo'mbona inafunguka?labda server kwako iko chini.acha nikutumie kwenye PM.

Kisale, hata mimi nafungua sioni kitu, ebu nitumie kwenye PM ili nikishaona niweze kuchangia kupambana na utovu wa nidhamu unaosemekana kufanyika!!!
 
Yaani watu wanasubiri hadi picha za viongozi ndio wanaona kuwa ZeUtamu haifai wakiwekwa walalahoi mbona mnakaa kimya
Leo ndio mnaona haifai ina maana siku zote huko nyuma kabla hawajamweka Rais alikuwa inafaa?

Belo,

Mitanzania ndivyo tulivyo....! unafiki mtupu, kukurupuka every where, kuzima moto kwa petrol.....very tired kwa kweli!
 
Naona kaogopa kaitoa, ujanja una viwango vyake kumbe!!
 
Kisale, hata mimi nafungua sioni kitu, ebu nitumie kwenye PM ili nikishaona niweze kuchangia kupambana na utovu wa nidhamu unaosemekana kufanyika!!!

Itabidi nifanye mpango nikutumie kwa sababu tunamshukuru Mungu,naona wameiondoa hiyo picha kwenye hiyo site kwa sasa.
 
Yaani watu wanasubiri hadi picha za viongozi ndio wanaona kuwa ZeUtamu haifai wakiwekwa walalahoi mbona mnakaa kimya
Leo ndio mnaona haifai ina maana siku zote huko nyuma kabla hawajamweka Rais alikuwa inafaa?

mkuu kwani wewe unalizwa na kila msiba? kuna mingine unatoa pole tu unatambaa sasa hapa kaguswa mzazi ndomaana watoto wote wanalia! na asiye lia basi ni yule aliyekuwa anamwona mzazi wake nuksi!
 
Napinga udhalilishaji ilofanywa na Ze Utamu, lakini lazima pia niseme
sasa tujifunze, na serikali ijifunze sio kwa sababu mkuu wa nchi
amedhalilishwa ndo eti wanaamka.

Utamu kaleta madhara makubwa sana ila kwa sababu labda hatuguswa
kama hili ndo maana tulikuwa kimya tu.

Nimekaa muda nikimfikiria huyu utamu ama hakika huyu mtu ana roho ya chuma.
 
Sio the utamu tu sasa hivi hata magazeti ya shigongo yanapitilizwa nayo yapigwe marufuku. Maadili hakuna. Stupid!
 
pich ile inasikitisha sana

Assume yule wa juu ya meza ni wewe yaani sura yako,ungejisikiaje? Una ndugu, marafiki na watu mbali mbali wanaokufahamu na wanaangalia mambo ya utamu!
Je wangekutetea umeonewa au kwasababu zao binafsi wengine wataanza kusema kumbe jamaa ndo alivyo!..
Kama kusikitisha utamu haijaanza kusikitisha jana wala leo bali tangia imeanzishwa!..
 
Ningeendeleza kuchekea chekea watu tu, kuendeleza upole na kutokuwa na msimamo na chochote nikifanyacho ili watu wasione kama nimebadilika wasije wakafikiri niliwekwa mezani kweli. Halafu ningepunguza safari za uarabuni ili watu wasije wakadhani kuna chochote huko maana ndio kwenyewe kwa hayo mambo ya mezani.
 
Yaani watu wanasubiri hadi picha za viongozi ndio wanaona kuwa ZeUtamu haifai wakiwekwa walalahoi mbona mnakaa kimya
Leo ndio mnaona haifai ina maana siku zote huko nyuma kabla hawajamweka Rais alikuwa inafaa?

Mkubwa heshima mbele,

Umeshasema viongozi tena raisi. Mimi nafikiri kwa issue ya rais sidhani hata kama wewe mwenyewe imekufurahisha mwana. Tukiachilia Ushabiki wa kisiasa na kiitikadi ila jamaa wamefika mbali sana. Kwa mtu ambaye anatuwakilisha kwenye Dhifa za kimataifa na kuiongoza nchi yetu yenye amani sidhani kama ni busara kwa ujinga walioufanya.

Ni kweli kwamba wengi wananchi walalahoi wamewekwa ila sasa kwa ukawaida wengi wao yaonekana ni chuki baina ya wao kwa wao au za kimapenzi.
 
JESHI la Polisi nchini linawasaka wamiliki wa mtandao unaojulikana kama ZE UTAMU ambao unakwenda kinyume na maadili za Kitanzania.

Jeshi hilo limetowa tamko kuwa wapo kwenye mikakati mikali ya kubaini wamiliki na wanaoendesha mtandao huo kwa nia ya kuwatia hatiani kwa kile kinachodaiwa kuwa wanadhalilisha watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa nchi.

Msemaji wa jeshi hilo amesema kuwa kutokana na vitendo vinavyofanywa na wamiliki wa mtandao huo Jeshi hili halitavumilia na limeamua kuwasaka moja kwa moja watu hao.

Amesema kuwa mtandao huo umekuwa ukitumia nafasi ya uhuru wa vyombo vya habari kwa kutoa picha mbalimbali za kudhalilisha na za ngono ikiwemo na kukashifu viongozi.

Amesema kuanzia jana Maofisa wa Polisi ikiwemo na Tume ya Uchunguzi wa Mawisiliano wanakutana kwa kujadili kwa kina suala hilo ikiwemo na kubaini wamiliki.

Amesema hatua iliyofikia ya mtandao huo kudhalilisha wananchi pia na kutotoa maadili mazuri kwa jamii vitendo hivyo havitavumiliwa na Jeshi hilo.

Pia baadhi ya wananchi waliyohojiwa na NIFAHAMISHE walisema kuwa hatua iliyochukuliwa na JEshi la Polisi ni la msingi kwa kuwa Mtandao huo ulikuwa unaweka picha za kipuuzi na fedheha kwa umma wa Watanzania.

“Tunaomba wasakwe haraka iwezekanavyo ili mkondo wa sheria ushike mahali pake kwa kuwakamata wote wanaojihusisha na mtandao huo”.

Source: Nifahamishe.com
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom