Je tuhahitaji tena Ze Utamu?

Je tuhahitaji tena Ze Utamu?

Status
Not open for further replies.
Ninapoandika soma kwa kutumia lens ili uone vizuri, nazimia watu kama Hunter S. Thompson, upo?!!? Mvivu wa kufikiria wewe na ndio maana unasikiliza watu kama Rush na Hannity.......kakojoe ukalale, muda wa kucheza gololi ushakwisha!😎

Huyo mwindaji(Hunter) ndio nani? Sijawahi kumsikia hata siku moja. Kwa upande mwingine wewe unamjua Rush na sasa hivi najua una flip back and forth kati ya Hannity na TNT...unabisha?
 
ALL IN ALL,pamoja na ubaya wake,huyu UTAMU ni kichwa,what else can explain hii uproar,na nchi kuingia in a state of panic kwa ku order utamu awe blocked in tanzania.if only angetumia huu ujuzi kwa maendeleo ya nchi tungenufaika

100% mzee!

Kwa namna nyingine,zeutamu ni muendelezo ya yale yanayoonekna kuwagusa wengi (mostly negatively) lakini wanaishia kupiga mayowe tu.Manji na Rostam Aziz ni mifano hai.Na mfano mwingine nu uchafuzi wa maadili unaoendeshwa na Shigongo.

Wakati ishu za Manji na Rostam ni more political,economic oriented,hii ya Shigongo ni ya kijamii zaidi japo pia kuna economic motives.

Sidhani kama huyu jamaa atawezekana,simply bcoz ameshambaza kirusi chake.Mbona serikali ilishapiga marufuku vijarida vyenye hadithi na michoro (angalia kwa makini hapo:HADITHI NA MICHORO) lakini hiyo haikusaidia kumzuia Shogongo na magazeti yake kuweka uchafu wao hadharani?Tatizo ni kwamba Shigongo ni mwanamtandao ambaye from time to time magazeti yake yanatumiwa kuwachafua walengwa flani wa watawala.And as long as anatimiza matakwa ya watawala,magazeti ya Shigongo yanaendelea kuwa best- sellers,sio in monetary terms pekee bali pia best-sellers wa uchafu katika jamii.

Kwani mhusika wa zeutamu akikamatwa ndio fikra zake,mtazamo wake au mawazo ya aina yake nayo yatakuwa yamekamatwa?Na hata ifiungiwa,what stops it from re-appearing under a new name as it was the case hapo mwanzoni?Huyu jamaa (if ni mmoja,which I doubt) is simply making use of what MANY OF US are fond of....udaku,uzushi,mjungu,ngono,picha za uchi,jig-jig,nk.

Na unajua kwanini,for instance,website/blog za picha zinatembelewa na watu wengi zaidi kuliko zenye hard news,opinion,analysis,commentary,etc?Coz majority are fond of pics,which could also also be indicative of uzembe wa kusoma.Na katika hizo pics zinazoibua comments nyingi zaidi ni za akina dada,mkao mbaya,shepu ya utata,nk nk.Kukiwa na picha ya Wole Soyinka,Prof Shivji,etc,it's likely usikute comment hata moja.


By the way,kama ALIYECHAFULIWA yuko kimya,why should we be bothered?
 
Last edited:
Waendesha mtandao Ze Utamu wasakwa

  • Ni baada ya kuwadhalilisha viongozi

Thursday, 23 April 2009 16:29
Na Said Mwishehe
Majira


JESHI la Polisi nchini limesema linafanya uchunguzi wa kina zaidi ili kubaini wanaojihusisha na mtandao wa kompyuta unajulikana kama Ze utamu ambao unatumika kudhalilisha watu wakiwemo viongozi wa ngazi za juu.

Hatua hiyo ya Jeshi la Polisi imetokana na kukithiri kwa picha mbalimbali za kudhalilisha kupitia mtandao huo.

Siku za hivi karibuni mtandao huo umekuwa ukitumia nafasi ya uhuru wa vyombo vya habari , kudhalilisha viongozi jambo ambalo ni kinyume cha ustaarabu na maadili ya jamii.

Akizungumza na Majira jana kwa njia ya simu mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi(jina tunalo) alisema kuwa mtandao huo umefikia mahali ambapo hautavumiliki tena na kazi inayoendelea sasa ni kuwasaka wahusika wake.

"Tumeona jinsi mtandao huo unavyodhalilisha viongozi wetu, sisi kama Jeshi la Polisi hatutavumulia, uchunguzi wa kina umeanza na muda sio mrefu mtasikia nini tumekifanya kwa watu hao,"alisema ofisa huyo.

Mbali ya kuchunguza wahusika Jeshi hilo pia linafuatilia kwa undani kupata wamiliki wa mtandao huo ambapo kutokana na vitendo vyake hautavumiliwa tena.

Tume ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA), imekiri kuwepo vitendo mbalimbali vya udhalilishaji kupitia mtandao huo na kuahidi kulishughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo.

" Tumeona hili, tunachokifanya sasa (jana mchana) tunakutana kikao cha dharura kujadili suala hilo kwa undani," alisema mmoja wa maofisa wa Tume hiyo aliyeomba kutoandikwa jina gazetini ambaye pia hakutaka kufafanua hatua watakazochukua kudhibiti tatizo hilo.

Wakizungumza na gazeti hili, wananchi mbalimbali walilaani vikali kitendo kilichofanywa na mtandao huo na kutaka upigwe marufuku sambamba na wahusika wake kukamatwa mara moja popote walipo na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

"Sisi kama Watanzania, hatubali vitendo hivi vya kipuuzi na fedheha kupitia mtandao huo viendelee vyombo vya dola vichukue hatua za haraka kuwakamata wote wanaojihusisha na mtandao huo ," alisema mama aliyejitambulisha kwa jina la Bi. Hawa Majaliwa .

Mwananchi mwingine aliyeomba kutoandikwa jina mkazi wa Upanga jijini Dar es Salaam, alisema hatua iliyofikia na mtandao huo haivumiliki na itashangaza kama vyombo vya dola vitashindwa kuwanasa wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria
 
Wanacheza hao...kama huo mtandao unaendeshwa kutokea nje ya nchi watafanya nini? Hivi wanadhani Mzee Ze Utamu hana contingency arrangements in case wanai-hack site yake?

Eti huo mtandao umefikia ambapo hauwezi kuvumiliwa tena. Ina maana wote walioanikwa huko ilikuwa inavumilika? Mapumbavu sana haya majitu. If the whole thing had been nipped in the bud we wouldn't be here in the first place.

ZeUtamu haiendi kokote. Long live ZeUtamu na hapa ndipo watakapodhihirika kuwa ni wapumbavu.
 
Dah, naona sasa serikali imekosa kazi ya kufanya. Hii kweli ni nchi ya kipumbavu na watu waso na upeo.
 
kwanza huu mtandao wa ze utamu una virus sana, kwa nini lkn? Mie nilikuwa nauchungulia chungulia, lkn siku hizi kuna virus balaa. Leo nimekwenda huko baada ya kuona hii thread, niliyokuta huko ni aibu tupu kwa viongozi.
 
Naona sasa mambo ya Animal Farm yanatimia!
"All animals are equal, but some animals are more equal than others."
Walipokua wanadhalilishwa wananchi ilikua bomba! Sasa imekua tatizo.
 
Huyo mwindaji(Hunter) ndio nani? Sijawahi kumsikia hata siku moja. Kwa upande mwingine wewe unamjua Rush na sasa hivi najua una flip back and forth kati ya Hannity na TNT...unabisha?

Ukim-google Hunter S. Thompson utaelewa alikuwa ni mtu wa namna gani....Alipojiua aliacha ka-note kanasomeka hivi, "No More Games. No More Bombs. No More Walking. No More Fun. No More Swimming. 67. That is 17 years past 50. 17 more than I needed or wanted. Boring. I am always bitchy. No Fun - for anybody. 67. You are getting Greedy. Act your old age. Relax - This won't hurt."

Halafu mshkaji wake artist Ralph Steadman wrote:

"...He told me 25 years ago that he would feel real trapped if he didn't know and that he could commit suicide at any moment. I don't know if that is brave or stupid or what, but it was inevitable. I think that the truth of what rings through all his writing is that he meant what he said. If that is entertainment to you, well, that's OK. If you think that it enlightened you, well, that's even better. If you wonder if he's gone to Heaven or Hell - rest assured he will check out them both, find out which one Richard Milhous Nixon went to - and go there. He could never stand being bored. But there must be Football too - and Peacocks..."

Jamaa ndio creator wa Gonzo journalism......nimemaliza kuangalia Olbermann na sasa nipo na Rachel maddow.
 
Naona sasa mambo ya Animal Farm yanatimia!
"All animals are equal, but some animals are more equal than others."
Walipokua wanadhalilishwa wananchi ilikua bomba! Sasa imekua tatizo.

Wanataka kutuletea udikteta wa maoni, cha ajabu kuna watu hapa ktk karne hii wanashabikia...kazi kweli!
 
I will go outdoors to get some ulanzi/mbege/komoni.
Ha ha ha ha!!!
Hahah NN ni bitozi angalia asije kuacha kuongea na wewe maana unamuharibia pozi(JOKING)
 
Binafsi nimesikitishwa na kuogopa sana juu ya uhodari wa hawa watu kutuma picha kama zile kwa jamii ya watu wenye akili na wenye mitazami tofauti juu ya kiongozi huyu mkuu wa nchi.

Kama kumbukumbu zangu ni sahihi, wakina dada wengi sana wamekuwa wakidhalilishwa na mtandao huu na kutoa malalamiko yao juu ya hii blog, lakini nadhani vyombo vya usalama havikutilia mkazo wala hawakuona umuhimu wa kufuatilia. hawakujua kuwa baadaye hili lingeweza kutokea hata kama si kwa mkuu wa nchi illa kwa kiongozi mwingine.

Nahdani ni fundisho kwetu sote kuwa jambo likitokea amablo ni kinyume cha maadili na haki za binadamu .... wahusika wasiangalie limetokea kwa nani ili wa-act equally kwa kila mtu.

Ni wazazi wangapi wameumizwa na hii blog?? mambinti zao wakitolewa picha za utupu, kwani hawa wazazi wamewatuma mabinti zao wawe malaya?? Na je umalaya wa hawa mabinti unawadhuru vipi wamiliki wa hii blog?? Nadhani umalaya mtu anafanya dhidi yake mwenyewe na mwili yake na its nobody's business.

Hii blog imeshadhaliisha wanawake na jamii nzima vya kutosha na hili jambi lilifumbiwa macho.
 
Kama kweli Mkulu wa nchi amfanya kale kamchezo ni hatari. Mimi siamini sana,lakini kama ni kweli ni fedheha si kwa yeye tu, hata kwa watanzania wote.
Ni aibu kubwa tutaficha wapi macho yetu? Mtu aliyepost ile picha tunaomba awe na uhakika na alichopost kwani kama si kweli ni hatari sana wakuu.
 
Mawazo yako ni hatari mno jamaa, sidhani kama unaelewa ukubwa wa unachokizungumzia....ingekuwa China hata hii JF isingekuwepo hewani!!

Acha ma-emotions ndugu, sheria na demokrasia ya kusema isipindishwe kwa furaha za wachache! Kwani kosa la utamu hasa ni nini?

Angalia mteremko wenye utelezi hapo mbele, binafsi hata mshua wangu akitundikwa kwa zeutamu, siwezi kuchukua msimamo kama wako!!! Sisi ni binadamu, hii ni 2009 na huu ndio mtandao wa intaneti, ni kama kokolo (kwa wale wa kanda ya ziwa)...samaki na mijimawe vyote vinavuliwa.......

Kumbe kwako Utamu hawana tatizo! basi tuishie hapa. Sjasema serikali iwe dicteta kama ya China! ninachosema kama kila kudhibiti kitu ni udikteta, basi neno kudhibiti ni sawa na udikteta.
 
Ze Utamu jaribuni kuwa na mipaka, hakuna uhuru usio na mipaka. Watanzania tunaenda wapi? Na wewe uliye-post hiyo picha una akili timamu?????
 
Dawa ni kuacha kwenda huko! Ukienda disco usianze kushangaa watu wakiwa nusu uchi hiyo ndiyo starehe ya huko hutaki hiyo zipo sehemu nyingi tu ikiwemo makanisani . Sasa mmenifanya hata mie niende huko kuangalia, picha yenyewe! Ni yauwongo kabisa!
 
Hakuna anayekubaliana na kitendo hicho cha kuchafuliwa Mhe. Rais. Hapa tunajadili issues nzito zinazolitafuna Taifa letu sio ushenzi kama ule. Kama kuna mtu anayewafahamu basi awasaidie Polisi. Pole Mhe. Vijana wako hao adamu imekwenda sokoni.
 
Nakubaliana na we kabisa hatuna maadili lakini nafikiri inapaswa pia kukumbuka kuwa mtu huadhibiwa kulingana na kosa alilofanya. Tunaequate uhuru na democrasia za Marekani na nchi nyingine lakini tunasahau kuwa wao pia wana limit kwa maana ya kwamba unaadhibu with evidence. Mf. Issue ya Clinton na Monica Lewinsky vikatuni, picha zilichorwa kupotray issue ile kwa maana ya kwamba walimchora akiwa katika lile tukio au lolote lingine linalopotray issue ile but kwa huyu je amefanya lolote kufanana na picha hiyo? lolote ambalo tuna proof nalo? Nisingeumia wala kusema lolote kama ningekuta ametolewa akibebwa na mtu aliyelabiwa kama fisadi au kitu kama hicho akiwa na nguo zake but not vile.

Jiweke wewe kwenye nafasi ya mtoto wake, mkewe, mjukuu wake au hata mzazi wake kama kujivika utanzania kumekushinda.

Tukio lililo tokea kweli ni baya. Lakini watu wengi limewagusa baada ya mkulu kuguswa. Mimi hapo ndiyo nakuwa tofauti. Kuna watu ambao ni kweli wanafanya haya mambo machafu wakiwekwa hadharani ili wabadirike sioni ubaya kwani wamewekwa kwa mabaya yao. Japo sina uhakiki wa hao wanaoyaweka ya wenzao ni wasafi kiasi gani!

Nchi hii imebadirika sana kwani zamani ulikuwa unaweza kusikia vitu vya ajabu ajabu kama sasa? Au kwakuwa tumekuwa na vyombo vingi vya habari? Sidhani kwani hata vyombo vyetu percent kubwa coverage yao ya habari inafanana.

Watu siku hizi wanataka kuwa kama western lakini kuna wengine ambao hilo hawalikubali hapo ndiyo unapokuja mtafaruku. Mfano huku kwetu vitu kama commision vilikuwa hakuna lakini tumesikia ya kwenye radar japo ilikuwa kubwa lakini huko ulaya wao ni kitu cha kawaida huku ni rushwa(Ubepali na ujamaa unagongana), Nguo za ajabu ajabu maungo yote yanakuwa nje (uzungu na uafrika unagongana), mikorogo, watu miili yao hawaithamini tena kwani picha za siku hizi balaa tupu (uzungu na uafrika unagongana) na mengine mengi.

Hivyo lazima tufike mahali tuwe na mjadala wa kitaifa ili tuweke mipaka yetu. Mbona huko uarabuni wameweka mipaka na hata wazungu wakienda baadhi ya nchi wanajifunga mapaka ijabu sembese hapa! Tunaitaji standard zetu katika kila kitu maisha, maadili, elimu, kazi na mengine mengi mpaka na kwenye siasa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom