Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,909
- 3,231
Picha ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (ICC), Balozi Mahmoud Thabiti Kombo na Naibu Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), Mame Mandiaye Niang, pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Umoja wa Afrika (AU) jijini Addis Ababa, Februari 14, 2026, imezua mjadala mzito.
Picha hiyo ilichapishwa kwenye ukurasa wa X wa ICC iliwaonyesha viogozi wakiwa na wasaidizi wao katika kikao, amacho hata hata hivyo haikujuliakan walizungumza nini.
Hata hivyo Niang alikutana na viongozi wengine katika mkutano huo, jambo lililoelezwa na watetezi wa Serikali ya CCM kuwa, kilikuwa ni kikao cha kawaida. Kama kilikuwa ni kikao cha heri, mbona Wizar aya Mabi ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki hawakuichapisha hiyo picha kwenye kurasa zao?
Iwe ni kikao cha kawaida au kisiwe cha kawaida, inatambulika kuwa Novemba 2025 muungano wa kimataifa wa wanasheria na makundi ya haki za kibinadamu walifungua kesi ICC, wakiiomba kumchunguza Rais wa Tanzania, na serikali yake kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu unaodaiwa kufanywa wakati wa uchaguzi Mkuu wa hivi karibuni.
Waraka wa ombi kwa ICC unamtuhumu Rais Samia Suhulu Hassan na maofisa wengine wa ngazi za juu kwa kuhusishwa moja kwa moja na vifo vya raia wakati wa maandamano ya baada ya uchaguzi.
Kwa hiyo, kwa vyovyote vile maongezi kati ya Niang na Balozi Kombo yalihusu kesi hiyo. Inawezekana ni katika hali ya kutaka kujua mwenendo wa shauri hilo limefikia wapi ili ikiwezekana wajipange.
Inawezekana pia ni mwendelezo wa Waziri Kombo kukutana na wadau mbalimbali katika nchi tofauti tangu baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 uliogubikwa na vurugu zilizosabaisha mauaji, majeruhi na uharibifu wa mali.
Katika hali inayoonekana kuwa ni kutuliza hali ya mambo katika uga wa kimataifa, Waziri Kombo amekuwa akisafiri huko na huko akikutana na viongozi anaofanikiwa kuwapata.
Kwa mfano alikwenda nchini Marekani mwishoni mwa maka jana na kukutana na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guteres pamoja na wanasiasa mbalimbali wakiwamo maseneta. Hata hivyo swali likabaki, mbona hakufanikiwa kuonana hata na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Antonio Rubio?
Ikumbukwe kwamba mwishoni mwa mwaka 2025 Serikali ya Marekani ilitoa taarifa ikieleza kuwa inatathmini kwa kina uhusiano wake na Tanzania, kwa kile inachodai kutoridhishwa na matukio ya ukandamizwaji wa uhuru wa dini na uhuru wa kujieleza nchini unaofanywa na Serikali.
Kama hiyo haitoshi mataifa mbalimbali ya Ulaya na Scandinavia, yenye balozi zake nchini, yalilaani mauaji ya raia katika maandamano ya Oktoba 29, 2025 huku wakizitaka mamlaka kukabidhi miili ya marehemu ili wakazike.
Kupitia tamko lao la pamoja, balozi za Uingereza, Canada, Norway, Uswisi, Ubelgiji, Denmark, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Poland, Slovakia, Hispania, Uswiswi na Ujumbe wa Umoja wa Ulaya (EU), zimeeleza kuhuzunishwa na vifo vilivyotokana vurugu za Oktoba 29.
Balozi Kombo pia ametembelea mataifa mengine kama Russia, Umoja wa Ulaya (EU) na Vatican kutafuta ushawishi, ambapo ameonekana akifanya vikao na viongozi mbalimbali wa mataifa hayo.
Kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kuwa tayari mchakato wa kesi hiyo umeanza na kwamba tayari kumekuwa na mawasiliano ya barua kutoka ICC kuja Tanzania.
ipango yaendelea kusukwa
Katika kukabiliana na hali hiyo, Rais Samia amechukua hatua kadhaa zinazotajwa kuwa ni kujihami na mashitaka yawe ni ya ICC au shutuma zozote kutoka mataifa na mashirika ya kimataifa.
Hatua hiyo ji pamoja na kuunda Tume ya Kuchunguza Uvunjifu wa Amani wakati wa uchaguzi Oktoba 29, 2025 inayoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande. Hata hivyo, tume hiyo ikekosolewa na wadau wakisema haiku huru, wakitaka uchunguzi huru ufanyike na vyokbo vya kimataifa.
Hatua nyingine inayotajwa ni kumhamisha aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi Palamagamba Kabudi na kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum).
Kabudi ambaye ni profesa wa sheria, anatajwa kusogezwa Ikulu ili kusaidia michakato mbalimbali ikiwemo ya kisheria na kazi kubwa inayomsubiri ni hiyo kesi ya ICC ili asaidie utaalamu wake kupmbana na janga hilo.
Mikakati mingine inayotajwa ni kufuatilia uchaguzi wa majaji wa ICC unaotarajiw akufanyika ifikapo Desemba 2026, ambapo Baraza la Nchi Wanachama (Assembly of States Parties) litachagua majaji sita wa ICC katika kikao chake cha 25 kitakachofanyika kuanzia Desemba 7 hadi 17, 2026.
Kwa mujiu wa tovuti ya ICC, vigezo vya uteuzi wa majaji hao kwa mujibu wa Kifungu cha 36(3)(a) cha Rome Statute, majaji wanapaswa kuwa na maadili ya juu, kutokuwa na upendeleo, kuwa waadilifu na kuwa na sifa zinazohitajika kuteuliwa katika nafasi za juu za mahakama katika nchi zao.
Inaelezwa na wachmbuzi wa masuala ya kimataifa kuwa, kupatikana kwa majaji hao kutatoa picha ya hali itakavyokuwa na itaipa nafasi Serikali ya Tanzania kufanya ushawishi (lobbying) kwa nchi mbalimbali ili zisaidie kuongeza nguvu kwenye kesi hiyo endapo itafika mbali.
Utaratibu wa kesi ICC
Kwa mujibu wa BBC, ICC huchunguza tu pale ambapo mamlaka za taifa hazianzishi ama kutekeleza mashtaka kwa usahihi. Kesi zinaweza pia kupelekwa kupitia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Mwendesha mashtaka wa ICC, anaweza kuanzisha uchunguzi na mashtaka, lakini yote yanapaswa kuidhinishwa na majaji. Kisha jopo la majaji husikiliza mashahidi na ushahidi kabla ya kutoa hukumu.
Ikiwa mshtakiwa anathibitishwa ama kukutwa na hatia, ICC inaweza kutoa kifungo cha jela, faini au adhabu nyinginezo zinazokubalika kisheria.
Hata hivyo, ICC haina polisi wake, hivyo inategemea mamlaka za kitaifa kushirikiana katika kukamata na kupeleka washukiwa The Hague, Uholanzi, ilipo Mahakama hiyo.
Updates....
ICC kutua nchini
Na Mwandishi Wetu
MAHAKAMA ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinal BCC), iliyopo The Hague nchini Uholanzi, imeanza kufanyia kazi, "kesi iliyowasilishwa na wanaharakati dhidi ya serikali ya Tanzania, MwanaHALISI fimeelezwa.
Mkuu wa shirika moja lisilo la kiserikali la kimataifa, linalofanys kazi zake nchini, ameeleza louwa amejulishwe kwamba kesi dhidi ya Serikali ya Tanzania, ni miongoni mwa mashauri 12 yatakayofanyiwa kazi na ICC katika mwaka huu wa 2026.
Anasema amejulishwa na watu waliopeleka malalamiko, kwamba ICC imeorodhesha malalamiko dhidi ya serikali ya Tanzania. kuwa miongoni mwa mashitaka yatakayofanyiwa kazi mwaka huu
"Ni kweli kwamba katika mwaka huu (2026), miongoni miwa kesi 12 ambazo ICC itazifanyia kazi, moja wapo inahusu Tanzania, amefafanua
JCC Ameongeza, Inapokea mamla kawa maelfu ya malalamiko, kutoka ulimwenguni kote. Kila mwaka yaweza kupokea hata kesi 1,000 (elfu moja), kutegemeana na hali ilivyokuwa
Anasema, "Hivyo kuona kesi yenu inashughulikiwa lova haraka kiasi hiki, ni jambo la kufurahisha. Kuna watu wamelalamika miaka mitano sasa, bado suala lao halijafanyiwa
Anasema, kinachotakiwa lowa sasa, ni wananchi wenye ufahamu wa kilichotendeka, kuweka ushahidi wao vizori, ili wachunguzi wa ICC watakapokuja nchini, wapatiwe ushirikiano.
Kupatikana lewa taarifa kwamba JCC inafanyia kazi malalamiko dhidi ya Serikali, kumekuja siku mbili baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mohammed Thabit Kombo, kukutana na Mame Mandiaye Niang, Naibu Mwendesha Mashitaka Mkuu wa mahakama hlyo.
Mkutano kati ya Balozi Kombo na mikai wa mahakama ya ICC, ulifanyika mwishoni mwa wiki, mjini Addis Ababa nchini Ethiopia
Niang allapishwa kushika wadhifa wa Naibu Mwendesha Mashitaka wa ICC, tarehe 7 Machi 2022
Mohammed Thabit Kombe Waziri wa Mambo ya Nje.
Ni raia wa Senegal Amewahi kashikua nafasi mbalimbali katika mfumo wa kusimamia hald nchini mwake, ikiwamo kuwa Muendesha Mashtaka mk kwenye mahakama ya rufani na pia amewahi kuzwa afisa wa sheria katika Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kambari ya Rwanda (ICTH)
Atmekuwa mwakilishi wa Kanda wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ua Dawes za Kulevya na Uhalifu (UNODC) Kusini mau Afrika, Jaji katika Mahakama za Rulas kwenye Mahakama ya Kimataifa ya makosa ya Jiriai ya Yugoslavia ya zamani na ICTR.
Hata hivyo, haikuweza kufahamia mara moja, kilichotadiliwa kwenye mkutano huo kwa undani, ingawa afisa mmoja kutoka wizara ya mambo ya nje, ameliambia gazeti hil kuwa viongozi hao wawili na ujumbe wao, saalizungumzia kuwapo kwa sham hảo
Malalamiko dhidi ya serikali, yamewasilishwa kwenye ofisi ya Mwendesha Mashitaisa Mioa wa ICC na shirika moja lisilo la kiserikali nchini Kenya na baadhi ya raia wa Tanzania waishio nchini Italia na Marekani.
Wanaharakati hao wanaituhumu Serikali kwa uhalifu dhidi ya binadamu na mauji ya halaiki, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa 29 Oktoba mwaka jana.
Katiks uchaguzi huo, walalamikaji wanasema, mamla
ya wanarichi waliuawa lovenye maandamano ya kupinga uchaguzi huo kufanyika, wakishinikiza mabadiliko kwenye tume ya uchaguzi
Aidha, malalamiko dhidi ya serikali yariahusishwa na madai kuwapo kwa Vitendo vya utekaji. utesail na mauaji ya raia, vilivyoshamiri nchini lowa zaidi ya miaka mitatu sasa. Walalamikaji wameomba
ICC kuanzisha uchunguzi ili kuwafungulia mashtaka baadhi ya viongozi waandarnizi wa serikali. wanaowatuhumu kusababisha mauaji hayo
Walalarnikaji wanadai kuwapo miili iliyokawa kwenye kaburi la pamoja: baadhi ya miill ya watu waliofariki kutokabidhiwa kwa ndugu zao, kuzihifadhi kwa mujibu wa taratibu walizojiwekea Warsdai pia lovamba baadhi ya majeruhi hawakupatiwa matibabu, baada ya kutelekezwa kwenye vituo vya polisi na au hospitali kuzuiwa kuwatibu.
Shirika la Kenya na Watanzania waishio ughaibuni wanadai, "Vitendo vilivyofanyika nchini Tanzania, kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa 29 Oktoba na mauaji na ukatili uliotokea, ni kinyume na sheria za lomataifa
"Vitendo hivyo, ni ukiukwaji wa hali za binadamu unaohitajä kufanyiwa uchanguzi wa lina na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ICC, wameeleza walalamikaji kwenye harus уво вла ICC
Walalamikaji warsawatuhumu maafisa waandamizi wa serikali, kuhusishwa moja kwa moja na vifo vya rais wakati we maandamano ya siku ya uchagul
Walalamikaji wanawakilishwa kwenye mahakama hiyo na mawakili kadhaa wa kimustaifa, wakiongozwa na Juan Carlos Gutierrez, mavenye ofisi zake huko Madrid, Hispanis
Kwa mujibu wa Gutierrez, mahakama ICC imeombwa kachukua hatua za haraka kwa kufanuta kazi malalamiko yaliyowasilishura
Katika malalarmiko aliyowasilisha The Hague, tarehe 13 Novemba 2025, Guti rrez anasema, "Wakati wa kuchukua hatua ni sasa
Anaongeza, "Waathirika wa Tanzania, waldwamo waandamanaji waliouawa kwa kudai uadilifu wa uchaguzi, wanaharakati waliotoweka kwa kutetea haki za binadamu, waandishi wa habari walioteswa kwa kuandika ukweli, Wamasai wa asili walionyang'anywa ardhi za mababu, jamii za Waislamu zilizoharibiwa na ugaidi, wamesubiri kwa muda wa kutosha kupata haki
Akisisitiza hoja yake, Gutirmez anasema. "Kila sila ya kuchelewa ni siku nyingine ya kutokuadhibiwa. Ni siku nyingine ambayo uhalifu unaendelea. Ni siku nyingine ambayo ushahidi unaharibiwa na siku nyingine ambayo mashahidi wanatishiwa na kunyamaza.
Serikali mara kadhaa imeeleza hatua ilizochukua baada ya vurugu ikiwemo kuunda tume ya uchunguzi, inayoongozwa Jaji Miauu wa mstaafu, Chande Odvuman, ili kupata ukweli wa chanzo cha machafuko na vifo vilivyotokea.
Kandwa kwa tume hiyo, kumekuja wakati Kamisherma Mkuu wa Haki za Binadamu wа Mataifa (OHCHR), Umoja wa Volker Turk, akishinikiza kufanyika uchunguzi huru wa mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanyika wakati wa uchaguzi huo.
Kamishena Türk alisema, anahimiza mamlaka ya Tanzania kutoa taarifa kuhusu hatima ya wote waliopotea na kukabidhi miili ya waliouawa kwa familia zao, ili wapate maziko ya heshima.
Amesema, UN imeshindwa kuthibitisha lova uhuru takwimu za majeruhi kutokana na hall) tete ya usalama na kuzirmwa kwa mitandao, mara baada ya machafuko hayo.
Anasema, "Lakini hakuna shaka kwamba kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu umefanyika nchini Tanzania.
Shirika la Utangazaji la Marekani (CCN), lilidai kuwa ya watu waliofariki imechuku na vikosi vya usalama na kaszik lewenye makaburi ya pamoja
Serikali ilijibu madai ya CC kwa kusema, chombo hicho c habari cha kimataifa, kimerip taarifa za upande mmoja na zisizozingatia weledi. CCN imekana madai hayo.
Maandamano yaliyoenea ne nzima siku ya uchaguzi na sil zilizofusta, yaliandaliwa kwa kikubwa na vijana, yalichoch kupitia mitandao ya kijamii rala wa Tanzania waishio nje nchi.
