- Inaonekana kuingia bungeni kwako ndio mwanzo na mwisho wa dunia, samahani sio wote wenye hizo ndoto, ni zako tu! sisi tunatafuta hela kwanza siasa itakuja baadaye hatuna haraka nayo kama wewe!
- Na kama kuna bunge duniani linaloweza kuigiliwa kwa njia hii basi hilo sio bunge ila ni kilabu cha pombe cha walevi walevi hivi, hapa tunatota maoni yetu kulingana na ishu iliyopo mezani, na sio lazima wote tuwe na mawazo kama yako mkuu, ya kufurahia hii picha isiyo na heshima kabisa mbele ya jamii!
- Wazee wetu kama Society zetu, wengi hawajui kama Europe na US ni mabara tofauti, Nigga kwa akwaida huwa hajui kama Africa ina nchi zaidi ya 45, huwa anafikiri ni nchi moja tu, kama wazee wetu huamini kuwa mbongo yoyote anayeenda Ulaya, ni lazima akutane na wabongo wengine, huwa hawajui kwamba kuna nchi nyingi mbali mbali na miji tofauti na sio rahisi kwa wabongo walioko majuu kuonana, na sisi mabingwa wa Internent tunaofahamika na jamii hapa tumelowa maji machafu kwa sababu sio rahisi kuwashawishi wanaotusikia na Internent kwamba hatuhusiki na haya ya ajabu, tukipita sasa itkuwa huyu naye ni wa huko Internent ni fedheha kubwa sana kwa sisi wastaarabu na wapenda ukweli, hizi za picha zingekua za ukweli isingekuwa taabu,
- Narudia tena kwamba leo ni siku ya giza kwangu binafsi, sikutegema kwamba one day katika uhai wangu, kama M-Tanzania niliyelelewa kizalendo, niliyezaliwa bongo na kutahiriwa kitamaduni kijijini kwetu, na kufundishwa madhara ya utawala wa mkoloni nikiwa Primary School, nikafundishwa namna ya kujitegemea nikiwa Secondari, nikafundishwa kufanya kazi nikiwa JKT, nikaenda Ulaya na kujionea faida za kutopitia utumwa katika maisha yangu kama weusi wa US, kama wa-Surinam wa Holland, kama weusi wa Arabuni. Mwalimu akanipa elimu kuhusu utaifa wangu, akanipa nationality, akanipa ID, baada ya miaka 14 majuu siku moja nikarudi bongo nikiwa nimeelewa uzuri na utamu wa maisha yangu ya kibongo na mapungufu yake, na uzuri na mapungufu ya maisha ya majuu, bado bongo ni tambarare, lakini kwenda majuu na kurudi nyumbani na this kind of education, ya kumuweka uchi kiongozi wa taifa kama alivyofanyiwa leo ni aibu yetu wananchi wote wa Tanzania, licha ya wale tu tunaoingia kwenye mitandao.
- Kwa wale mnaoshangilia ni haki yenu, isiyokuwa haki yenu ni ku-question haki za wengine kutoshangilia, mnachotakwia kutufundisha hapa kwenye uwanja huu wa Great Thinkers ni vipi this thing inaweza kutusaidia taifa na maendeleo yake, na hasa vipi hii new ideology yenu inakwenda samba samba na masilahi yetu kitaifa.
- Kumbuka kwa shujaa huenda kilio, lakini kwa muoga siku zote huwa ni kicheko!
FMES!