JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 6,835
- 14,213
Mimi nafikiri kwenye ishu Asange,kuna Mengi kuliko yanayotufikia machoni,Wanabodi,
Yule Mwandishi Julian Asange wa WikiLeaks, ametiwa nguvuni nchini Uingereza kwa kutakiwa na Marekani, sasa sisi Tanzania, tujifunze kwa kitachompata, tukitumie kujifanyia tathmini ya Press Freedom yetu, usikute sisi tuna press freedom kubwa kuliko UK na US, zaidi ya magazeti kufungiwa na vituo vya TV kutozwa faini, kwa hivi karibuni sijawahi kusikia Mwandishi wa habari wa Tanzania kukamatwa na kushitakiwa kwa alichoandika, ukiondoa enzi zile za Adam Mwaibabile "Mwana".
Media za Tanzania tuna kilio kikubwa cha kulakamikia kuminywa au kunyimwa uhuru, "freedom of the press", na wananchi wetu wanakosa haki ya kupata habari, "the right to information" mfano kuyajua mahela ya vote 20 ambayo kila Ripoti ya CAG ikiibuka, inaibuka nayo, na kila siku tunawaangalia waandishi wa nchi za wenzetu haswa UK na US kuwa wako huru zaidi.
Baada ya Asange kudakwa, Marekani inaitaka Uingereza iwakabidhi Asange ili wao ndio washughulike nae, somo kubwa la kujifunza hapa ni kufuatilia kwa makini, nini kitamkuta Asange, jee Uingereza itamkabidhi kwa Marekani washungulike nae au itamkingia kifua katika kulinda na kutetea uhuru wa habari?.
Kwa upande wa sisi media ya Tanzania, tunalalamika kuwa hatuko huru wakati waandishi wenyewe wa type ya Asange, wa kuibua ma vitu kama Stan Katabalo, hatuna!, sisi wengi wa waandishi wetu, tunakalia kuandika habari za mikutano, warsha, seminar, na makongamano na kuzikunja zile brown ..., badala ya kuandika investigative stories, sasa uhuru wa habari tunaoutafuta ni uhuru gani?.
Ripoti ya CAG imetoka ikiibua madudu kibao, ya matumizi mabaya ya fedha za umma, tungekuwa na serious media, by now, tungeishajua for sure ile 1.5B ilikwenda wapi na imefanyia nini!, au hata kujua tuu hizi fedha zinazochotwa kila siku hazina bila idhini ya Bunge na kutumbukizwa kwenye Vote 20, mule huwa zinakwenda kufanyia nini?. Inamaana hiyo Vote 20, wao hawana mpango kazi, kila siku wanafanya kazi kwa zimamoto, then serious media ingeonyesha basi hata huo moto uliozimwa isije kuwa ni mchwa tuu anatafunia Vote 20?.
Kama UK inayojitapa kwa Press Freedom sasa inamshikilia Asange, sisi kwetu kuna Mwandishi gani amewahi kushikiliwa kwa maandishi yake ukiondoa kifo cha Daudi Mwangosi, na kupotea kwa Azory Gwanda na Ben Saanane wetu humu jf, jee kuna Mwandishi gani au media gani inaripoti investigative stories za kuhalalisha kutaka uhuru zaidi?.
Somo la kukamatwa kwa Asange kutupe funzo usikute sisi Tanzania tuna press freedom kubwa kuliko ya UK na US ila tumekosa waandishi wa kuitumia hii freedom kikamilifu.
Jumamosi Njema
Paskali
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari mjini Morogoro, JamiiForums ndani ya Nyumba
Wanabodi, Mei 3 kila mwaka, ni siku ya kimataifa ya kusherehea siku ya Uhuru wa Habari, Media Freedom Day, ambapo hapa nchini, kitaifa siku hii inasherehekewa kwa muda wa siku 2, mjini Morogoro toka katika hoteli ya Nashera ambapo Jamiiforums pia inashiriki, na tayari nimeishamuona Mkuu Max...www.jamiiforums.com
Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija
Wanabodi, Naangalia kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari kinachorushwa na Star TV, ambapo mwandishi Mkongwe, Deo Masakilija, amealikwa. Dotto Bulendu ameanza kwa hoja 'Je media imetimiza wajibu wake ipasavyo katika kuwabaini hawa watu wasiojulikana wanaohusika na matukio ya utekaji, utesaji...www.jamiiforums.com
Media kuikosoa Serikali: Je, Tanzania tuna Strong Media au Strong Journalists wenye Uwezo huo?
Wanabodi, Declaration of Interest: mwanzisha mada ni mwandishi wa habari mstaafu ambaye amehudumu kwenye tasnia hii as active media kwa zaidi ya miaka 27, hivi sasa ni mstaafu akiendelea kuhudumu as passive media kama mwandishi/mtangazaji was kujitemea kupitia kampuni ya PPR. Serikali zote...www.jamiiforums.com
Uhuru wa Habari Tanzania: Je, Vyombo Viko Huru? Je, Waandishi wa Habari wako huru? Wanathaminiwa?.
Wanabodi Leo ni Siku ya Kimataifa ya kuadhimisha Uhuru wa Habari. Kwa Tanzania, maadhimisho rasmi yanafanyikia jijini Mwanza, katika kuadhimisha siku hii kwa Tanzania tunaadhimisha nini haswa?. Wakati tukiadhimisha hicho tunachoadhimisha, hakuna ubaya tukitafakari baadhi maswali haya... 1.Jee...www.jamiiforums.com
Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa
Mkuu The Boss, bahasha ni dunia nzima mpaka Ikulu inatembeza bahasha, hiyo PCCB yenyewe na mpaka Polisi wanatembeza bahasha halali kama wanavyotembezewa!. dunia nzima kivipi? waandishi wa kenya wanapokea bahasha? marekani? uingereza? south africa?????www.jamiiforums.com
Hivi kweli,unavujishiwa siri za jeshi uwanja wa vita,ambazo katika zikiwekwa wazi,zinaweza kuweka usalama wa nchi pabaya,unaweza kuleta mgogoro wa kidiplomasia kati ya nchi na nchi,
Huyu jamaa,pamoja na Edward Snowden,walivujisha mambo mabaya ambayo yanafanywa na taasisi za kiusalama,na kiinteligensia katika kuilinda USA.
Taarifa kama hizo ukiziweka wazi,wala usaidii wasomaji wako,unaweza kuiweka nchi nzima katika matatizo makubwa,kwa ufupi kuna vitu ambavyo havitakiwi kuwekwa hadharani,kama bajeti na manunuzi ya jeshi au idara ya usalama wa Taifa.
Mwandishi wa habari ukikurupuka ukazivujisha,inabidi yakukute makubwa.
Ubaya ni kwamba kwa huku kwetu Afrika,na TZ,wakubwa wanaweza wakakuambia huo mradi(kama meremeta) ni wa usalama wa Taifa,kumbe ni chaka LA kupiga pesa ya umma bila kuulizwa.huku kwetu uadirifu ni zero,wanakuambia wameua majambazi katika mapambano,kumbe watu wamekuwa executed,kisa wanaipinga serikali.
Na huko kwa wenzetu,Asange atakuwa na mawakili wake,uwezi kulinganisha na hapa bongo.
Sent using Jamii Forums mobile app