Je, Tanzania tuna Media Freedom kubwa kuliko UK na US? Tushuhudie kitachompata Julian Assange wa WikiLeaks! Tujifunze kwake

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,321
2,000
..Tafadhali Pascal Mayalla..tafadhali sana.
..wewe una heshima hapa JF.
..vijana wanakuamini ktk mabandiko yako.
..sasa siyo vizuri ukawapoteza namna hii.
..mgogoro wa Julian Asange unahusu KUDUKUA na kusambaza mawasiliano nyeti ya SEREKALI ya Marekani.
..ungewatendea haki vijana hawa wanaokuheshimu kama ungefafanua alichofanya Julian Asange, halafu ukalinganisha kama waTz tuna uhuru wa kufanya jambo linalokaribiana na alichofanya.
..au kwanini usituletee clip za MAHOJIANO kati ya VIONGOZI wa nchi za wenzetu na VYOMBO VYA HABARI halafu tuone kama na sisi tuko HURU na tuna WELEDI kiasi gani.
Mkuu Joka Kuu, heshima mbele.
Amini usiami kwa Tanzania tatizo ni letu sisi waandishi, wala usiende mbali hadi ulaya kwa Asange, nenda tu hapo jirani zetu Kenya kwa Mohammed Amin na Jicho Pevu, sisi tunashindwa nini?.
Nimesema waandishi wetu wengi ni reporters tuu kazi kubwa ya media zetu ni kuripoti matukio na pressvm conferences, mikutano, semina, warsha na makongamano. Hutuzami deep na hatuna competent team za kufanya IJ.

Tangu awamu ya 5 imeingia madarakani, fungu la Vote 20, ndilo linaloongoza kuchota fedha hazina bila ya idhini ya Bunge na bila kuidhinishwa na CAG, this time limechota zaidi ya bilioni 900. Tungekuwa na serious media, zamani wangeshutumia IJ kujua hizi fedha za vote 20 ambazo hazikuidhinishwa na Bunge, zinafanyia nini?.

Kabla Lissu hajadhambuliwa , kuna mtu alisema kuhusu tunadukua simu mtu fulani, intelligence agencies zote duniani zinadukua sio simu tuu, hata tailing, emails hadi private lives, lakini haya mambo huwa hayasemwi.

Akakamilisha kwa kumuita mdukuliwa ni msaliti na kusema msaliti hawezi kuachwa hivi hivi akasurvive na kutolea mfano usaliti vitani huwa wanafanywa nini.

Baada ya muda mfupi Lissu kashambuliwa. Tungekuwa na serious media, aliyemtaka maneno hayo angeulizwa alimaanisha nini


Ninachosema hapa kama hizi serious media zipo, zifanye tuone.
Kwa vile hatuna then inawezekana kabisa sisi tuko huru kuliko UK na US ila hatuna competent person who can do some serious stuff.
P
 

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,250
2,000
Kweli me naona Mayalla usifananishe issue ya Julian aisee Yale sio level ya Africa, kwavyovyote yule anatumia hackers kitu ambacho ni kosa la jinai. Kwa hacking tu unaweza kuiba hata Banks ndo maana kukawa na mifumo ya Security. Hizo habari anazo zisema mayala ni uchunguzi wa kuhoji sources lkn huwezi kuvunja na kufungua vilivyofungwa bila ruhusa ya wahusika huo ni ujambazi, ndo alipoangukia Julian.
Kipindi cha JK Kubenea alipata wapi taarifa za Ikulu?mbona alitetewa kuwa ni uhuru wa habari?kwanini huyu jamaa akamatwe na watu waliomtetea Kubenea?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Orketeemi

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
3,112
2,000
Achana naye huyo, analeta ukada. Yaani upuuzi wa Makonda wa kuutetea kweli?
Mkuu Ndege John, kwanza nakubaliana na wewe, kwenye media hatuwezi kujilinganisha na Kenya, wametuacha mbali.

Lakini kwenye hili la Makonda kuwataja watu majina was not right, na hiyo ya 70% ya rushwa kuwasafisha pia sikubaliani na wewe kwa sababu ili kupata% ni lazima kuwe na data, hiyo data ya hadi kufikia 70% imepatikanaje?.

Yes rushwa ipo kila mahali, ila nakuomba usichanganye na vile vibahasha vyetu halali mkaviita rushwa
P

Wema ni akiba.
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,059
2,000
wa hivi karibuni sijawahi kusikia Mwandishi wa habari wa Tanzania kukamatwa na kushitakiwa kwa alichoandika
Pascal, wote sasa hivi si wanaandika kwa kumsifia Magufuli, watashitakiwa kwa lipi? Waandishi nyinyi mnaongoza kwa uoga baada ya Azory kupotea.

Wewe ulijaribu kuwa huru, kilikupata nini? huko Bunge ukapelekwa na Tangu muda huo ukaamua kujikalia kimywa au kuunga mkono juhudi kiujanja ujanja!... ukiwa na nai ya kukosoa lkn ka woga kanakufanya usite kuandika ubaya, maoni huru uliyonayo
 

mangelengele

JF-Expert Member
Nov 4, 2014
1,299
2,000
Kipindi cha JK Kubenea alipata wapi taarifa za Ikulu?mbona alitetewa kuwa ni uhuru wa habari?kwanini huyu jamaa akamatwe na watu waliomtetea Kubenea?

Sent using Jamii Forums mobile app
Uchungizi haukuonyesha km kubenea alihack information inawezekana kuna mtu alivujisha taarifa zikamfikia kubenea. Sidhani km hilo ni kosa la mwandishi, hilo ni tatizo la maafisa wa usalama kuwa taarifa hazitoki nje. Lkn Julian anakiuka sheria za kimtandao ambazo mataifa yote wanaheshimu. Majasusi huwa wana hack baadhi ya information kwa matumizi yao ya kiusalama, huwa hawapublish. Hata zile email za Hilary, sio km alikua anaziaccess peke yake, mashirika mengi ya kijasusi huwa yanazipata ila hawawezi kuanika kwa raia wa kawaida.
 

obseva

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
542
1,000
Nimeuliza jee Tanzania ni hatuna uhuru wa kuandika, au ni hatuna waandishi wa kuandika habari za uchunguzi?.

Ili kuhalalisha media tunatishwa media ziandike basi mambo mazito tuone serikali inaigopa. Ripoti ya CAG imetoka ikiibua madudu kibao, media gani imekwenda deep, nakutolea mfano mdogo tuu wa Vote 20?

P
Sidhani Pascal ila mazingira ya kuandika habari za kiuchunguzi yamebinywa. Kumbuka wakati Ndugu Ulimwengu alipoanza kuandika makala zake za uchunguzi, akifuatiwa na Mwana halisi, na wengine nini kiliwakuta??. Pia kumbuka kukua kwa aina fulani ya uandishi ni mazingira na kama mazingira hayaruhusu huwezi ona kukua kwa aina hiyo ya uandishi.

Na mara nyingi waandishi wa Tanzania wanaandika kufutana na nani yuko madarakani na anataka nini, hata uandishi wako wewe mwenyewe umebalika sana sio wa Pascal yuleee na wote waliosoma maandishi yako ya kabla wanajua ni influensi ya mazingira. Hivyo kiufupi demokrasia ya kuandika inaendani na demokrasia ya uhuru wa kujieleza na uhuru wa watu kutafuta platform nyingi wawezavyo ilikuandika na kutoa mawazo yao kwa mujibu wa sheria zinazo waongoza.
Sijui kama tanzania tunasheria inayoruhusu na kulinda investigative journalism?
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,321
2,000
Kigogo India Asange wetu, kama anatafutwa akamatwe, na tusubiri kwanza akamatwe, maana sikuwahi kusikia kama wale wasiojulikana kumshambulia Tundu Lissu wakitafutwa hivi, ila akipatikana, tusubirie nini kitamkuta
P.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,321
2,000
Wanabodi,
Leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa habari, kila mwaka sisi waandishi huwa tunakutana mahali kwa siku 2 na kujadili mambo mbalimbali kuhusu uhuru wa habari, na katika mkusanyiko huo, serikali, vyama vya habari na Taasisi za habari hutoa matamko kede kede kuhusu uhuru wa habari, lakini kwa mwaka huu, kufuatia janga la Corona, hakuna maadhimisho yoyote rasmi ya kukutana, ila nilitegemea wizara ya habari, vyama vya habari na mashirika na Taasisi za habari zitoe matamko mbalimbali.

Bado sijabahatika kuona tamko lolote!, ila usikute zile speech huwa zinaandaliwa kwa ajili ya presentations kwenye kongamano hotelini, safari na per diem!, leo hakuna safari, no trip, no per diem, no hotel gathering, hivyo this time hata speech tuu hakuna?!.

Nawatakia waandishi wenzangu, maadhimisho haya ya kimya kimya, nawashauri wale wafadhili mbalimbali wa tukio hili, kwa vile hatukusafiri, wala kula na kulala hotelini, then naomba hao wafadhili watutumie tuu hizo per diem, tutahama majumbani mwetu na kuhamia hotelini 3 days kisha tutatoa matamko.

Paskali
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,321
2,000
Wanabodi,

Media za Tanzania tuna kilio kikubwa cha kulakamikia kuminywa au kunyimwa uhuru, "freedom of the press", na wananchi wetu wanakosa haki ya kupata habari, "the right to information" mfano kuyajua mahela ya vote 20 ambayo kila Ripoti ya CAG ikiibuka, inaibuka nayo, na kila siku tunawaangalia waandishi wa nchi za wenzetu haswa UK na US kuwa wako huru zaidi.

Baada ya Asange kudakwa, Marekani inaitaka Uingereza iwakabidhi Asange ili wao ndio washughulike nae, somo kubwa la kujifunza hapa ni kufuatilia kwa makini, nini kitamkuta Asange, jee Uingereza itamkabidhi kwa Marekani washungulike nae au itamkingia kifua katika kulinda na kutetea uhuru wa habari?.

Ripoti ya CAG imetoka ikiibua madudu kibao, ya matumizi mabaya ya fedha za umma, tungekuwa na serious media, by now, tungeishajua for sure ile 1.5B ilikwenda wapi na imefanyia nini!, au hata kujua tuu hizi fedha zinazochotwa kila siku hazina bila idhini ya Bunge na kutumbukizwa kwenye Vote 20, mule huwa zinakwenda kufanyia nini?. Inamaana hiyo Vote 20, wao hawana mpango kazi, kila siku wanafanya kazi kwa zimamoto, then serious media ingeonyesha basi hata huo moto uliozimwa isije kuwa ni mchwa tuu anatafunia Vote 20?.


Jumamosi Njema
Paskali
Naendelezea hapahapa~~chochote chenye public interest kina mawazo na maamuzi yanayotoka kwa watu kwa ajili ya watu,mwenyekiti wa ccm ndiye anejigeuza kuwa mwenyekiti wa Tanzania,yeye ndiye anayeamua nini kiwe for public interest na kipi kisiwe,alipomtimua mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali baada ya mkaguzi huyo kusimamia public interest wewe Pascal Mayalla hukumgombeza magufuli au kumkumbusha kuwa pesa iliyopotea ni ya umma,na mkaguzi ndiye jicho la umma,unamshangilia mwizi halafu unaongea habari za public interest,fool
Mkuu Capt Tamar ,
Asante,
Ubarikiwe
Japo sina uhakika, kwavile siwezi kusoma mabandiko ya watu wote humu, lakini humu JF, mimi ni miongoni mwa tuliomuongelea sana CAG, Ofisi ya CAG na Ripoti za CAG!.
Nakutakia Jumapili Njema
P
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,321
2,000
Brightone Chonjo
Snowden amuomba Trump amuachie Julian Assange kizuizini nchini United Kingdom kabla hajahukumiwa.
Snowden ni mdukuzi (Hacker) ambaye alikuwa ameajiriwa na serikali ya marekani kitengo cha ujasusi yani (CIA) alifukuzwa kazi baada ya ku kopi na kusambaza habari za siri za marekani na ndipo alipo kimbilia Russia walipo mpa hifadhi mpaka sasa, amemuomba raisi anae maliza muhula wake Trump kumuachia Assange ambaye huyu ni ni raia wa Australia ambaye kazi yake ni mwandishi wa habari lakini anauwezo wa kuhariri na kutoa kwa uma na bado ni mwanaharakati hasa kwa mabo ya marekani .
Ambapo aliweka hadharani habari za vita mauaji na matumizi ya silaha mbalimbali za marekani kwenye magazeti ya marekani kama washington post na new york times ambapo kikawaida hilo ni kosa kubwa sana la kiusalama wa taifa (National security ), yani kwa tanzania tukute habari za jeshi zile nyeti kwenye Nipashe hahaha, sasa ukiangalia hapa maana yake Snowden alikuwa anadukua anampa rafiki yake Assange anaweka kwenye magazeti , ufahamu kuwa Assange alisha shikwa kwa makosa mengine ya kiudhalilishaji wa kingono na sweden alipo achiwa akapata hifadhi UK na ndipo alipo shikwa na serikali ya kule baada ya marekani kutoa tamko kuwa anamadai ya kuweka hadharani habari nyeti hapo ikiwa ni 2016 kwenye uchaguzi wa marekani ambapo WikiLeaks waliposti baadhi ya habari hizo....lakini 23 may 2019 ndipo alipo kamatwa UK uchunguzi ukiendelea na endapo atagundulika na makosa atafungwa miaka 175.
mwezi uliopita patna wake stella ali post picha za watoto wake wawili twiter kwamba wanamhitaji nyumbani.
#wikileaks #snowden #FreeAssange #Classfiedinformation #Confidential #Russiatoday
Mkuu snow snow , karibu na mitaa hii .
P
 

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
4,629
2,000
Wanabodi,

Yule Mwandishi Julian Asange wa WikiLeaks, ametiwa nguvuni nchini Uingereza kwa kutakiwa na Marekani, sasa sisi Tanzania, tujifunze kwa kitachompata, tukitumie kujifanyia tathmini ya Press Freedom yetu, usikute sisi tuna press freedom kubwa kuliko UK na US, zaidi ya magazeti kufungiwa na vituo vya TV kutozwa faini, kwa hivi karibuni sijawahi kusikia Mwandishi wa habari wa Tanzania kukamatwa na kushitakiwa kwa alichoandika, ukiondoa enzi zile za Adam Mwaibabile "Mwana".

Media za Tanzania tuna kilio kikubwa cha kulakamikia kuminywa au kunyimwa uhuru, "freedom of the press", na wananchi wetu wanakosa haki ya kupata habari, "the right to information" mfano kuyajua mahela ya vote 20 ambayo kila Ripoti ya CAG ikiibuka, inaibuka nayo, na kila siku tunawaangalia waandishi wa nchi za wenzetu haswa UK na US kuwa wako huru zaidi.

Baada ya Asange kudakwa, Marekani inaitaka Uingereza iwakabidhi Asange ili wao ndio washughulike nae, somo kubwa la kujifunza hapa ni kufuatilia kwa makini, nini kitamkuta Asange, jee Uingereza itamkabidhi kwa Marekani washungulike nae au itamkingia kifua katika kulinda na kutetea uhuru wa habari?.

Kwa upande wa sisi media ya Tanzania, tunalalamika kuwa hatuko huru wakati waandishi wenyewe wa type ya Asange, wa kuibua ma vitu kama Stan Katabalo, hatuna!, sisi wengi wa waandishi wetu, tunakalia kuandika habari za mikutano, warsha, seminar, na makongamano na kuzikunja zile brown ..., badala ya kuandika investigative stories, sasa uhuru wa habari tunaoutafuta ni uhuru gani?.

Ripoti ya CAG imetoka ikiibua madudu kibao, ya matumizi mabaya ya fedha za umma, tungekuwa na serious media, by now, tungeishajua for sure ile 1.5B ilikwenda wapi na imefanyia nini!, au hata kujua tuu hizi fedha zinazochotwa kila siku hazina bila idhini ya Bunge na kutumbukizwa kwenye Vote 20, mule huwa zinakwenda kufanyia nini?. Inamaana hiyo Vote 20, wao hawana mpango kazi, kila siku wanafanya kazi kwa zimamoto, then serious media ingeonyesha basi hata huo moto uliozimwa isije kuwa ni mchwa tuu anatafunia Vote 20?.

Kama UK inayojitapa kwa Press Freedom sasa inamshikilia Asange, sisi kwetu kuna Mwandishi gani amewahi kushikiliwa kwa maandishi yake ukiondoa kifo cha Daudi Mwangosi, na kupotea kwa Azory Gwanda na Ben Saanane wetu humu jf, jee kuna Mwandishi gani au media gani inaripoti investigative stories za kuhalalisha kutaka uhuru zaidi?.

Somo la kukamatwa kwa Asange kutupe funzo usikute sisi Tanzania tuna press freedom kubwa kuliko ya UK na US ila tumekosa waandishi wa kuitumia hii freedom kikamilifu.

Jumamosi Njema
Paskali

Yaani Watanzania siku hizi ni siasa za mashindano tu kila tatizo letu tukiwa nalo badala ya kulitatua ni kujaribu kushindanisha. Tukishidwa hoja siku hizi msemo ni tuachie nchi yetu😂 na ndiyo maana mijadala ya hivi yote inaishia tuachie nchi yetu! Kaeni na mabeberu wenu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom