Je, Tanzania tuna Media Freedom kubwa kuliko UK na US? Tushuhudie kitachompata Julian Assange wa WikiLeaks! Tujifunze kwake

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
40,535
2,000
Wanabodi,

Yule Mwandishi Julian Asange wa WikiLeaks, ametiwa nguvuni nchini Uingereza kwa kutakiwa na Marekani, sasa sisi Tanzania, tujifunze kwa kitachompata, tukitumie kama shamba darasa la kujifanyia tathmini ya Press Freedom yetu, usikute sisi tuna press freedom kubwa kuliko UK na US, zaidi ya magazeti kufungiwa na vituo vya TV kutozwa faini, kwa hivi karibuni, ukiomuondoa Mkuu Maxence Melo wa jf, anayesubuliwa na kesi lukuki mahakamani, sijawahi kusikia Mwandishi mwingine yoyote wa habari wa habari wa Tanzania kukamatwa na kushitakiwa kwa alichoandika, ukiondoa enzi zile za Adam Mwaibabile "Mwana".

Japo Media za Tanzania tuna kilio kikubwa cha kulalamikia kuminywa kwa uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza, "freedom of the press" and "freedom of expression" , kiukweli ni sisi media wenyewe na waandishi wa habari, tunaoshindwa kuutumia kikamilifu uhuru tulionao, hivyo kupelekea wananchi wetu wanakosa haki ya kupata habari, "the right to information" mfano kuyajua mahela ya vote 20 ambayo kila Ripoti ya CAG ikiibuka, inaibuka nayo, na kila siku tunawaangalia waandishi wa nchi za wenzetu haswa UK na US jinsi walivyo sharp kuyaibua madudu na kuwaona kama wenzetu wako huru zaidi, sisi media zetu, nini kinatushinda?!.

Baada ya Asange kudakwa, Marekani inaitaka Uingereza iwakabidhi Asange ili wao ndio washughulike nae, somo kubwa la kujifunza hapa ni kufuatilia kwa makini, nini kitamkuta Asange, jee Uingereza itamkabidhi kwa Marekani washungulike nae au itamkingia kifua katika kulinda na kutetea uhuru wa habari?.

Kwa upande wa sisi media ya Tanzania, tunalalamika kuwa hatuko huru wakati waandishi wenyewe wa type ya Asange, wa kuibua ma vitu kama Stan Katabalo, hatuna!. Sisi wengi wa waandishi wetu, tunakalia kuandika habari za mikutano, warsha, seminar, na makongamano na kuzikunja zile naniliu za little brown ..., (naomba nisimalizie kwa heshima ya waandishi wenzangu), kazi yetu sasa ni badala ya kuandika habari za uchunguzi, investigative stories, sasa media zote, waandishi wote tunaishia kufanya reportage tuu, na sana sana kwa habari za kusifu, shangwe na kuomba mapambio ya kumsifu mfalme na vazi lake la ajabu!. We have totally no critical media in Tanzania, no news analysis, sisi media tumekwama wapi na kupigia kelele hatuna uhuru wa uhuru wa habari, wakati ni sisi wenyewe tunashindwa kutimiza wajibu wetu, huo uhuru tunaoutafuta ni uhuru gani?!..

Ripoti ya CAG imetoka ikiibua madudu kibao, ya matumizi mabaya ya fedha za umma, tungekuwa na serious media, by now, tungeishajua for sure ile 1.5B ilikwenda wapi na imefanyia nini!, au hata kujua tuu hizi fedha zinazochotwa kila siku hazina bila idhini ya Bunge na kutumbukizwa kwenye Vote 20, mule ndani ya vote 20, humo huwa zinakwenda kufanyia nini?!. Inamaana hiyo Vote 20, wao hawana mpango kazi, kila siku wanafanya kazi kwa zimamoto?!. Huu ni uthibitisho kuwa Tanzania hatuna any serious media ingeonyesha basi hata hayo majivu tuu ya huo moto, unaozimwa na fedha za zimamoto ndani ya vote 20, uliozimwa, ili kuthibitisha ni kweli kulikuwa na moto, isije kuwa ni mchwa tuu anatafunia hiyo Vote 20?.

Kama UK inayojitapa kwa Press Freedom sasa inamshikilia Asange, sisi kwetu kuna Mwandishi gani amewahi kushikiliwa kwa maandishi yake ukimuondoa Max wa JF?. Na tukiachana na kifo cha Daudi Mwangosi, na kupotea kwa Azory Gwanda na Ben Saanane wetu humu jf, jee kuna Mwandishi gani mwingine au media gani inaripoti investigative stories za kuhalalisha kutaka uhuru zaidi?.

Somo la kukamatwa kwa Asange kutupe funzo usikute sisi Tanzania tuna press freedom kubwa kuliko ya UK na US ila tumekosa media na waandishi mahiri wenye na ability, capacity and capability ya kuitumia hii freedom iliyopo kikamilifu, na kuisaidia jamii!. Nikisema media ya Tanzania ni hopeless media, nitakuwa niwaonea?.

Jumamosi Njema
Paskali
 

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
14,207
2,000
Mkuu Paschal nimekuelewa Sana kwa hili hata mfano mzuri upo Kenya Wana waandishi wa habari za uchunguzi wazuri Sana.

Tatizo ninaloliona bongo Ni kukosekana kwa weledi pamoja na kutamalaki kwa rushwa katika media karibu 70%.

Kwa mfano kipindi cha sekeseke la Makonda kuwataja drug dealers nilishangaa Sana jinsi pesa chafu zilivyomwaga ili tu kuwasafisha wahusika na kumchafua Makonda..badala waandishi wa habari wangeingia kufanya uchunguzi wa kina wao wakaanza kujifanya watetezi na kutunga stories nyingi nje ya kilichotarajiwa.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
40,535
2,000
Sasa mkuu Pascal Mayala tujadili nini cha maana hapa?

Umeshasema mwenye hata kuandika tu habari za maana kwa sasa hamuwezi kwa sababu ya hofu je ni vipi unataka tujilinganishe na nchi hizo?
Nimeuliza jee Tanzania ni hatuna uhuru wa kuandika, au ni hatuna waandishi wa kuandika habari za uchunguzi?.

Ili kuhalalisha media tunatishwa media ziandike basi mambo mazito tuone serikali inaigopa. Ripoti ya CAG imetoka ikiibua madudu kibao, media gani imekwenda deep, nakutolea mfano mdogo tuu wa Vote 20?

P
 

Don Clericuzio

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
16,972
2,000
Leo nadhani akili zangu zimegoma kuelewa.

BTW: Nachojua, Assange alikuwa ana-leak informations ambazo ni classified.

Hapa kwetu hata zile ambazo siyo classified hutakiwi kuziandika, mfano mdogo ni hii report ya CAG, leo hii Bunge linagoma kupublish vitabu vyote, website imekuwa shut down.

Wabunge wa chama tawala hawataki hata CAG atajwe na wabunge pinzani nk.

Uzuri wewe unayeandika haya uko kwenye Media.

Nina mtu ambaye yuko kwenye print media na ni gazeti ambalo liko very prominent, anakwambia kabla hamjaprint ni lazima font ferd itumwe kwa utawala ili wakuruhusu kuiprint, kila siku.

Naamini hilo la kutuma font ferd unalijua.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
40,535
2,000
Mkuu Paschal nimekuelewa Sana kwa hili hata mfano mzuri upo Kenya Wana waandishi wa habari za uchunguzi wazuri Sana
Tatizo ninaloliona bongo Ni kukosekana kwa weledi pamoja na kutamalaki kwa rushwa katika media karibu 70%
Kwa mfano kipindi Cha sekeseke la makonda kuwataja drug dealers nilishangaa Sana jinsi pesa chafu zilivyomwaga ili TU kuwasafisha wahusika na kumchafua makonda..badala waandishi wa habari wangeingia kufanya uchunguzi wa kina wao wakaanza kujifanya watetezi na kutunga stories nyingi nje ya kilichotarajiwa.
Mkuu Ndege John, kwanza nakubaliana na wewe, kwenye media hatuwezi kujilinganisha na Kenya, wametuacha mbali.

Lakini kwenye hili la Makonda kuwataja watu majina was not right, na hiyo ya 70% ya rushwa kuwasafisha pia sikubaliani na wewe kwa sababu ili kupata% ni lazima kuwe na data, hiyo data ya hadi kufikia 70% imepatikanaje?.

Yes rushwa ipo kila mahali, ila nakuomba usichanganye na vile vibahasha vyetu halali mkaviita rushwa
P
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
40,535
2,000
Leo nadhani akili zangu zimegoma kuelewa.

BTW: Nachojua, Assange alikuwa ana-leak informations ambazo ni classified.

Hapa kwetu hata zile ambazo siyo classified hutakiwi kuziandika, mfano mdogo ni hii report ya CAG, leo hii Bunge linagoma kupublish vitabu vyote, website imekuwa shut down.

Wabunge wa chama tawala hawataki hata CAG atajwe na wabunge pinzani nk.

Uzuri wewe unayeandika haya uko kwenye Media.

Nina mtu ambaye yuko kwenye print media na ni gazeti ambalo liko very prominent, anakwambia kabla hamjaprint ni lazima font ferd itumwe kwa utawala ili wakuruhusu kuiprint, kila siku.

Naamini hilo la kutuma font ferd unalijua.
Hilo la font fed ninalijua the editor in Chief wa government media ni yule mpangaji wetu wa nyumba kubwa hivyo hiyo ni haki yake kwa media yake
P
 

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
12,004
2,000
Tuna kipi cha kujifunza kutoka kwa nani? Asange au US na UK? Binafsi hapo umenichanganya.

Waandishi wajifunze nini kwa Asange wakati hata hakuwa mwandishi wa habari?

Unaposema tuna waandishi wa warsha na maandamano unasahau kinachowapata hao waandika maandamano?
 

mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,859
2,000
Demokrasia na freedom of press hua zinauelekeo mmoja
Unakiri kuwa kuna mambo mengi tu hamjui na hamna guts za kufuatilia (sababu ni no democracy),unakiri kuna habari nyeti nyingi tu lakini hamjui access mpate vipi kwa sababu hamna transparency ambalo ni zao la democracy etc etc

Issue ya Assenga inaonekana serious kwa sababu ali jeopardise national security(CIA,KGB ,M16 etc) na sio machapisho yanayowahusisha politicians individually (kama ilivyo huku, anza tu kufuatilia kesi ya kangi lugola ilifutwaje ,au zile hela za combat lakini hazikuletwa ingawa ni issue ambayo ilifanywa na organized crime na sio taasisi ya police...utaona utakavyofanywa)
 

Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,149
2,000
Demokrasia na freedom of press hua zinauelekeo mmoja
Unakiri kuwa kuna mambo mengi tu hamjui na hamna guts za kufuatilia (sababu ni no democracy),unakiri kuna habari nyeti nyingi tu lakini hamjui access mpate vipi kwa sababu hamna transparency ambalo ni zao is democracy etc etc

Issue ya Assenga inaonekana serious kwa sababu ali jeopardise national security(CIA,KGB ,M16 etc) na sio machapisho yanayowahusisha politician individually (kama ilivyo huku, anza tu kufuatilia kesi ya kangi lugola ilifutwaje ,au zile hela za combat lakini hazikuletwa ingawa ni issue ambayo ilifanywa na organized crime na sio taasisi ya police...utaona utakavyofanywa)

Mkuu taarifa gani ya wikileaks ambayo ina jeopardize national security?

huzo intelligency agency for 50yrs now watu wanazisema mpaka kuzichezea movies


issue ya wikileaks inaumiza mtu individual na ku expose maovu
 

Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,019
2,000
Nimeuliza jee Tanzania ni hatuna uhuru wa kuandika, au ni hatuna waandishi wa kuandika habari za uchunguzi?.

Ili kuhalalisha media tunatishwa media ziandike basi mambo mazito tuone serikali inaigopa. Ripoti ya CAG imetoka ikiibua madudu kibao, media gani imekwenda deep, nakutolea mfano mdogo tuu wa Vote 20?

P
Paskal, swali lako trick sana ila na vitu viwili tu huku kuna mwandishi aliaanza kuandika tu nasikia sijui mwaka hatujui yuko wapi kule yule jamaa kashikwa tu kituo cha kwanza mahakamani hakuna kitu sijui uchunguzi bado unaendelea.

Halafu yule anataka kushtakiwa sababu sio kaandika nini ila kudokoa na kesi ya rape sijui ila yule utamuona nje tu kule sheria ziko sasa kipimo acha mwandishi huku afanye hata robo ya robo aliyoandika yule halafu ndio tutapima kama tuko sawa au tumewazidi.
 

Escrowseal1

JF-Expert Member
Dec 17, 2014
2,797
2,000
Nimeuliza jee Tanzania ni hatuna uhuru wa kuandika, au ni hatuna waandishi wa kuandika habari za uchunguzi?.

Ili kuhalalisha media tunatishwa media ziandike basi mambo mazito tuone serikali inaigopa. Ripoti ya CAG imetoka ikiibua madudu kibao, media gani imekwenda deep, nakutolea mfano mdogo tuu wa Vote 20?

P
Tujifunze na sisi kama nchi kuwapigia mayowe maana ingekuwa kwetu wangeshaanza mayowe.sasa ni zamu yetu
 

Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,019
2,000
Mkuu taarifa gani ya wikileaks ambayo ina jeopardize national security?

huzo intelligency agency for 50yrs now watu wanazisema mpaka kuzichezea movies


issue ya wikileaks inaumiza mtu individual na ku expose maovu
Kosa sio habari kosa Hacking kudokoa mtandao wa mtu tu hata site ni kosa ila sababu sheria au mahakama kule wako vizuri huyu jamaa atashinda tu.
 

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
3,917
2,000
Wanabodi,

Yule Mwandishi Julian Asange wa WikiLeaks, ametiwa nguvuni nchini Uingereza kwa kutakiwa na Marekani, sasa sisi Tanzania, tujifunze kwa kitachompata, tukitumie kujifanyia tathmini ya Press Freedom yetu, usikute sisi tuna press freedom kubwa kuliko UK na US, zaidi ya magazeti kufungiwa na vituo vya TV kutozwa faini, kwa hivi karibuni sijawahi kusikia Mwandishi wa habari wa Tanzania kukamatwa na kushitakiwa kwa alichoandika, ukiondoa enzi zile za Adam Mwaibabile "Mwana".

Media za Tanzania tuna kilio kikubwa cha kulakamikia kuminywa au kunyimwa uhuru, "freedom of the press", na wananchi wetu wanakosa haki ya kupata habari, "the right to information" mfano kuyajua mahela ya vote 20 ambayo kila Ripoti ya CAG ikiibuka, inaibuka nayo, na kila siku tunawaangalia waandishi wa nchi za wenzetu haswa UK na US kuwa wako huru zaidi.

Baada ya Asange kudakwa, Marekani inaitaka Uingereza iwakabidhi Asange ili wao ndio washughulike nae, somo kubwa la kujifunza hapa ni kufuatilia kwa makini, nini kitamkuta Asange, jee Uingereza itamkabidhi kwa Marekani washungulike nae au itamkingia kifua katika kulinda na kutetea uhuru wa habari?.

Kwa upande wa sisi media ya Tanzania, tunalalamika kuwa hatuko huru wakati waandishi wenyewe wa type ya Asange, wa kuibua ma vitu kama Stan Katabalo, hatuna!, sisi wengi wa waandishi wetu, tunakalia kuandika habari za mikutano, warsha, seminar, na makongamano na kuzikunja zile brown ..., badala ya kuandika investigative stories, sasa uhuru wa habari tunaoutafuta ni uhuru gani?.

Ripoti ya CAG imetoka ikiibua madudu kibao, ya matumizi mabaya ya fedha za umma, tungekuwa na serious media, by now, tungeishajua for sure ile 1.5B ilikwenda wapi na imefanyia nini!, au hata kujua tuu hizi fedha zinazochotwa kila siku hazina bila idhini ya Bunge na kutumbukizwa kwenye Vote 20, mule huwa zinakwenda kufanyia nini?. Inamaana hiyo Vote 20, wao hawana mpango kazi, kila siku wanafanya kazi kwa zimamoto, then serious media ingeonyesha basi hata huo moto uliozimwa isije kuwa ni mchwa tuu anatafunia Vote 20?.

Kama UK inayojitapa kwa Press Freedom sasa inamshikilia Asange, sisi kwetu kuna Mwandishi gani amewahi kushikiliwa kwa maandishi yake ukiondoa kifo cha Daudi Mwangosi, na kupotea kwa Azory Gwanda na Ben Saanane wetu humu jf, jee kuna Mwandishi gani au media gani inaripoti investigative stories za kuhalalisha kutaka uhuru zaidi?.

Somo la kukamatwa kwa Asange kutupe funzo usikute sisi Tanzania tuna press freedom kubwa kuliko ya UK na US ila tumekosa waandishi wa kuitumia hii freedom kikamilifu.

Jumamosi Njema
Paskali
Paskali,
Hebu jaribu kuangalia vyomb vinavyotuma wawakilishi katika press conference za wapinzani.
Hebu chunguza humu ndani miaka mitatu iliyopita tulivyokuwa tunachangia humu,pekua na uangalie
Kaangalie takwimu za waandishi waliopoteza maisha Kenya kwa kujihususha na habari za kiuchunguzi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom