Je, Tanzania tuna Media Freedom kubwa kuliko UK na US? Tushuhudie kitachompata Julian Assange wa WikiLeaks! Tujifunze kwake

Kumfananisha Asange ambae anadukua habari za CIA na kuwauzia KGB wafanyie kazi na ninyi mnaochambua vizuri katiba na vipengele vyake mamlaka aliyonayo CAG nadhani kuna utofauti hapo...Asange ndio alitoa siri ya Nchi moja ndogo kutunza fedha za matajiri kimagumashi na kuonesha account zao pamoja na fedha zilizomo humo kwa hiyo pamoja na kwamba ni Mwandishi wa habari Source ya habari zake ndio tatizo..
 
Mkuu Mayalla usipige propaganda, kwa alichokifanya Assange angekua mwandishi wa habari wa kitanzania basi hata hati ya kukamatwa isingehitajika, angeokotwa tu kwenye viroba huko coco beach.
Hivyo basi wenzetu wanao uhuru wa habari na ndio maana jamaa atashtakiwa na hukumu itatolewa kwa haki mahakamani

--------
angalia baadhi tu ya tuhuma zake
"The indictment alleges that in March 2010, Assange engaged in a conspiracy with Chelsea Manning, a former intelligence analyst in the US Army, to assist Manning in cracking a password stored on US Department of Defense computers connected to the Secret Internet Protocol Network (SIPRNet), a US government network used for classified documents and communications.
"Manning, who had access to the computers in connection with his duties as an intelligence analyst, was using the computers to download classified records to transmit to WikiLeaks.
"Cracking the password would have allowed Manning to log on to the computers under a username that did not belong to him. Such a deceptive measure would have made it more difficult for investigators to determine the source of the illegal disclosures.
"During the conspiracy, Manning and Assange engaged in real-time discussions regarding Manning's transmission of classified records to Assange. The discussions also reflect Assange actively encouraging Manning to provide more information.
"During an exchange, Manning told Assange that 'after this upload, that's all I really have got left.' To which Assange replied, 'curious eyes never run dry in my experience'.
"Assange is charged with conspiracy to commit computer intrusion and is presumed innocent unless and until proven guilty beyond a reasonable doubt.
"If convicted, he faces a maximum penalty of five years in prison. Actual sentences for federal crimes are typically less than the maximum penalties. A federal district court judge will determine any sentence after taking into account the US Sentencing Guidelines and other statutory factors."
 
Nakubaliana na wewe hasa kuanzia paragraph ya nne...ukweli lazima usemwe nchi hii hakuna waandishi wa caliber ya Asange ...hata wakiachwa free bado wataendelea kuripoti useless informations...na kwa maoni yangu hii inasababishwa na poor quality ya training lakini pia uwezo mdogo na njaa hivyo ni rahisi sana kutokuwa na focus
Kama utakumbuka CAG kwenye press yake aliwaambia kuwa wasipotoa..yeye atatoa....hakuwa mjinga..ni kwamba anawajua akili zao vizuri tu....kwa kifupi waandishi wengi wa Tz hawana msaada hata kidogo waendelee kusaka ugali tu...
Nchi hii ina madudu mengi sana ila waandishi wapo tu kazi kuripoti vitu cheap cheap tu...ni aibu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeuliza jee Tanzania ni hatuna uhuru wa kuandika, au ni hatuna waandishi wa kuandika habari za uchunguzi?.

Ili kuhalalisha media tunatishwa media ziandike basi mambo mazito tuone serikali inaigopa. Ripoti ya CAG imetoka ikiibua madudu kibao, media gani imekwenda deep, nakutolea mfano mdogo tuu wa Vote 20?

P
Hata wakiwepo,wataandika Nini?
Wakiandika watapotezwa....
 
Tanzania waandishi wengi ni waandishi wa kishabiki unafikiri mwandishi wa aina hiyo anaweza kuandika habari za kueleweka,habari zote anangoja apigiwe simu za udaku kuliko kwenda kuchunguza habari,lazima watambue mwandishi wa habari ni zaidi ya usalama wa taifa na zaidi ya askari wa upelelezi kuzifukua habari na nyeti zilizojificha wao kuandika Lowassa kajinyea ndio habari au kangomba hawakulipwa!
 
Kwa kuongezea leo CAG katoa report yake na ameainisha waziwazi maeneo kibao yakionesha wizi wa kutisha...eti kesho yake gazeti la Tanzanite linakuja na heading kwamba CAG AHAHA KUJINASUA....hahaha..this is stupid...sasa unajiuliza ajinasue kutoka kwenye nini ...haya mambo ni national interest..ni kodi za wananchi na mikopo..ambayo lazima ilipwe....aisee......Mungu amlinde Prof Assad.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,

Yule Mwandishi Julian Asange wa WikiLeaks, ametiwa nguvuni nchini Uingereza kwa kutakiwa na Marekani, sasa sisi Tanzania, tujifunze kwa kitachompata, tukitumie kujifanyia tathmini ya Press Freedom yetu, usikute sisi tuna press freedom kubwa kuliko UK na US, zaidi ya magazeti kufungiwa na vituo vya TV kutozwa faini, kwa hivi karibuni sijawahi kusikia Mwandishi wa habari wa Tanzania kukamatwa na kushitakiwa kwa alichoandika, ukiondoa enzi zile za Adam Mwaibabile "Mwana".

Media za Tanzania tuna kilio kikubwa cha kulakamikia kuminywa au kunyimwa uhuru, "freedom of the press", na wananchi wetu wanakosa haki ya kupata habari, "the right to information" mfano kuyajua mahela ya vote 20 ambayo kila Ripoti ya CAG ikiibuka, inaibuka nayo, na kila siku tunawaangalia waandishi wa nchi za wenzetu haswa UK na US kuwa wako huru zaidi.

Baada ya Asange kudakwa, Marekani inaitaka Uingereza iwakabidhi Asange ili wao ndio washughulike nae, somo kubwa la kujifunza hapa ni kufuatilia kwa makini, nini kitamkuta Asange, jee Uingereza itamkabidhi kwa Marekani washungulike nae au itamkingia kifua katika kulinda na kutetea uhuru wa habari?.

Kwa upande wa sisi media ya Tanzania, tunalalamika kuwa hatuko huru wakati waandishi wenyewe wa type ya Asange, wa kuibua ma vitu kama Stan Katabalo, hatuna!, sisi wengi wa waandishi wetu, tunakalia kuandika habari za mikutano, warsha, seminar, na makongamano na kuzikunja zile brown ..., badala ya kuandika investigative stories, sasa uhuru wa habari tunaoutafuta ni uhuru gani?.

Ripoti ya CAG imetoka ikiibua madudu kibao, ya matumizi mabaya ya fedha za umma, tungekuwa na serious media, by now, tungeishajua for sure ile 1.5B ilikwenda wapi na imefanyia nini!, au hata kujua tuu hizi fedha zinazochotwa kila siku hazina bila idhini ya Bunge na kutumbukizwa kwenye Vote 20, mule huwa zinakwenda kufanyia nini?. Inamaana hiyo Vote 20, wao hawana mpango kazi, kila siku wanafanya kazi kwa zimamoto, then serious media ingeonyesha basi hata huo moto uliozimwa isije kuwa ni mchwa tuu anatafunia Vote 20?.

Kama UK inayojitapa kwa Press Freedom sasa inamshikilia Asange, sisi kwetu kuna Mwandishi gani amewahi kushikiliwa kwa maandishi yake ukiondoa kifo cha Daudi Mwangosi, na kupotea kwa Azory Gwanda na Ben Saanane wetu humu jf, jee kuna Mwandishi gani au media gani inaripoti investigative stories za kuhalalisha kutaka uhuru zaidi?.

Somo la kukamatwa kwa Asange kutupe funzo usikute sisi Tanzania tuna press freedom kubwa kuliko ya UK na US ila tumekosa waandishi wa kuitumia hii freedom kikamilifu.

Jumamosi Njema
Paskali

Paskali huu uzi ni mtamu sana,wazungu ni wanafiki sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo nadhani akili zangu zimegoma kuelewa.
BTW: Nachojua, Asange alikuwa ana-leak informations ambazo ni classified.
Hapa kwetu hata zile ambazo siyo classified hutakiwi kuziandika, mfano mdogo ni hii report ya CAG, leo hii Bunge linagoma kupublish vitabu vyote, website imekuwa shut down.
Wabunge wa chama tawala hawataki hata CAG atajwe na wabunge pinzani nk.
Uzuri wewe unayeandika haya uko kwenye Media.
Nina mtu ambaye yuko kwenye print media na ni gazeti ambalo liko very prominent, anakwambia kabla hamjaprint ni lazima font ferd itumwe kwa utawala ili wakuruhusu kuiprint, kila siku.
Naamini hilo la kutuma font ferd unalijua.
Yaani ripoti ya CAG ipo wazi mitandaoni na kila kukicha magazeti yanachambua hoja dhaifu sana hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuna kipi cha kujifunza kutoka kwa nani? Asange au US na UK? Binafsi hapo umenichanganya.

Waandishi wajifunze nini kwa Asange wakati hata hakuwa mwandishi wa habari?

Unaposema tuna waandishi wa warsha na maandamano unasahau kinachowapata hao waandika maandamano?
Iko wapi "freedom of speech, expression etc" wanazosema hao wazungu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Mayalla usipige propaganda, kwa alichokifanya Assange angekua mwandishi wa habari wa kitanzania basi hata hati ya kukamatwa isingehitajika, angeokotwa tu kwenye viroba huko coco beach.
Hivyo basi wenzetu wanao uhuru wa habari na ndio maana jamaa atashtakiwa na hukumu itatolewa kwa haki mahakamani

--------
angalia baadhi tu ya tuhuma zake
"The indictment alleges that in March 2010, Assange engaged in a conspiracy with Chelsea Manning, a former intelligence analyst in the US Army, to assist Manning in cracking a password stored on US Department of Defense computers connected to the Secret Internet Protocol Network (SIPRNet), a US government network used for classified documents and communications.
"Manning, who had access to the computers in connection with his duties as an intelligence analyst, was using the computers to download classified records to transmit to WikiLeaks.
"Cracking the password would have allowed Manning to log on to the computers under a username that did not belong to him. Such a deceptive measure would have made it more difficult for investigators to determine the source of the illegal disclosures.
"During the conspiracy, Manning and Assange engaged in real-time discussions regarding Manning's transmission of classified records to Assange. The discussions also reflect Assange actively encouraging Manning to provide more information.
"During an exchange, Manning told Assange that 'after this upload, that's all I really have got left.' To which Assange replied, 'curious eyes never run dry in my experience'.
"Assange is charged with conspiracy to commit computer intrusion and is presumed innocent unless and until proven guilty beyond a reasonable doubt.
"If convicted, he faces a maximum penalty of five years in prison. Actual sentences for federal crimes are typically less than the maximum penalties. A federal district court judge will determine any sentence after taking into account the US Sentencing Guidelines and other statutory factors."
"mere allegations.."

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la sekta ya habari hapa nchini lipo katika paragraph ya nne ya bandiko lako.

Tukishafanikiwa kuwa na waandishi wa habari ambao ni professionals itaponya jamii Yetu kwa Kiwango kikubwa sana.

inasikitisha kuona namna jamii Yetu inavyolishwa mambo yasiyokuwa na tija kabisa. tunaua vizazi vya watu wenye uwezo wa kuchambua mambo ya msingi yatakayosukuma maendeleo ya Taifa letu.

kwa kuzingatia tatizo Hilo la msingi katika sekta ya habari. wengine tumeacha kuyasoma kabisa hayo magazeti.
 
Sasa mbona wewe mwenyewe ushasema kila kitu, tujadili nini?

Unaposema zaidi ya Daudi Mwangosi na Azory Gwanda halafu huyachukulii kwa uzito. Unataka tukupe mfano gani?

Au we unaona Azory kajipoteza?

Sent using my Nokia Torch
 
Fid Q alisema sio tu bongo hakuna Uhuru wa habari ila kuna Uhuru wa vyombo, mwenye chombo na mwenye Mali..Uhuru umekitwa katika misingi hiyo tu kwingine ni utumwa

Chief
 
Tatizo la sekta ya habari hapa nchini lipo katika paragraph ya nne ya bandiko lako.

Tukishafanikiwa kuwa na waandishi wa habari ambao ni professionals itaponya jamii Yetu kwa Kiwango kikubwa sana.

inasikitisha kuona namna jamii Yetu inavyolishwa mambo yasiyokuwa na tija kabisa. tunaua vizazi vya watu wenye uwezo wa kuchambua mambo ya msingi yatakayosukuma maendeleo ya Taifa letu.

kwa kuzingatia tatizo Hilo la msingi katika sekta ya habari. wengine tumeacha kuyasoma kabisa hayo magazeti.

great post
 
Back
Top Bottom