Je, Tanzania tuna Media Freedom kubwa kuliko UK na US? Tushuhudie kitachompata Julian Assange wa WikiLeaks! Tujifunze kwake

Wanabodi,

Yule Mwandishi Julian Asange wa WikiLeaks, ametiwa nguvuni nchini Uingereza kwa kutakiwa na Marekani, sasa sisi Tanzania, tujifunze kwa kitachompata, tukitumie kama shamba darasa la kujifanyia tathmini ya Press Freedom yetu, usikute sisi tuna press freedom kubwa kuliko UK na US, zaidi ya magazeti kufungiwa na vituo vya TV kutozwa faini, kwa hivi karibuni, ukiomuondoa Mkuu Maxence Melo wa jf, anayesubuliwa na kesi lukuki mahakamani, sijawahi kusikia Mwandishi mwingine yoyote wa habari wa habari wa Tanzania kukamatwa na kushitakiwa kwa alichoandika, ukiondoa enzi zile za Adam Mwaibabile "Mwana".

Japo Media za Tanzania tuna kilio kikubwa cha kulalamikia kuminywa kwa uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza, "freedom of the press" and "freedom of expression" , kiukweli ni sisi media wenyewe na waandishi wa habari, tunaoshindwa kuutumia kikamilifu uhuru tulionao, hivyo kupelekea wananchi wetu wanakosa haki ya kupata habari, "the right to information" mfano kuyajua mahela ya vote 20 ambayo kila Ripoti ya CAG ikiibuka, inaibuka nayo, na kila siku tunawaangalia waandishi wa nchi za wenzetu haswa UK na US jinsi walivyo sharp kuyaibua madudu na kuwaona kama wenzetu wako huru zaidi, sisi media zetu, nini kinatushinda?!.
MEI 3 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa vyombo vya habari, Mimi Pascal Mayalla, kwa niaba yangu kama mwanahabari na kwa niaba ya kampuni yangu ya PPR as chombo cha habari, niwatakie wanahabari wenzangu wote, maadhimisho mema ya siku hii, huku nikidurusu, niliwahi kusema nini kuhusu uhuru wa habari Kwa media za Tanzania yetu.

Nawatakia uhuru wa habari mwema.
Paskali.
 
Back
Top Bottom